Shabiki Wa Simba Kuishabikia Yanga, Wa Yanga Kuishabikia Simba ni Uzalendo Wa Kipuuzi

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,250
15,116
Hii kampeni bila shaka imeasisiwa na wanasiasa wasio fahamu utani wa jadi uliopo kati ya simba na yanga.

Ukiwa shabiki wa timu mojawapo ya hizi timu huwezi kuiombea mema timu ya upande wa pili hata siku moja. Nashangaa kuona wapuuzi wakianzisha harakati za kuweka uzalendo kwenye kuzishabikia hizi timu.

Wanasiasa wa bongo wanapenda sana kudandia mafanikio ya kundi lolote ktk anga la michezo. Mara nyingi huwa hawahusiki na hawapendi kuhusishwa ktk maandalizi ya mafanikio, bali wao hupenda kudandia basi kwa mbele.

Uzalendo wa kumshabikia mpinzani wako wa jadi hautofanya mpinzani wako wa jadi afanye vyema. Bali litakalo muwezesha afanye vyema ni maandalizi mazuri na uwekezaji bora ktk klabu.

Nashauri kila mtu ashabikie timu yake, na ikiwezekana amtakie mabaya jirani yake kwa sababu upinzani wetu wa jadi umejengwa ktk misingi hiyo.

Simba na Yanga haziwakilishi Tanzania ktk michuano ya afrika, Simba sc itawakilisha mashabiki wa simba na Yanga atawakilisha mashabiki wa Yanga.

Hizi timu haziwakilishi Taifa la Tanzania, Timu pekee inayowakilisha Taifa la Tanzania ni TAIFA STARS. Taifa Stars ndio timu pekee ambayo simba na yanga wako tayari kuiunga mkono. Kama mnataka uzalendo basi jitihada zenu zipelekeni katika kuijenga Taifa Stars.

Shubamitt. Kila mtu ashabikie timu yake. Fuvk SOLIDARITY FOREVER.
 
Haitatokea hata sekunde 1 kuishabikia kolokolo fc
Ni upuuzi hata kuanzisha hamasa kudhani kuwa hizi timu zitafanya vizuri tu ikiwa watani zao watawaunga mkono kuwashangilia.
 
Ukishabikia sanaaaa Simba na Yanga. kichwani lazima zipungue.

KUNA VIJANA WENGI MNO AKILI ZIMEWARUKA KABISA, HAWANA FUTURE WAO NI KUWAZA SIMBA NA YANGA TU.....

MSIPOTEZE MUDA NA UPUUZI WA SIMBA NA YANGA.
HIZO TIMU NI VYOMBO VYA PROPAGANDA VYA SELIKALI KUWAPOTEZA MABOYA.

MY MESSAGE
MWENYE MASIKIO NA ASIKIE
 
images (1)-1.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom