Sh. Bilioni 700 si Haba na Wanaobeza Vibaba

Hivi ACACIA tulikuwa tunawadai pesa za good intention au deni kutokana na kutuibia?, Sasa kwa nini watulipe kwa kile tusichowadai lakini kwa kile tunachowadai ambalo ndo msingi haswaa wa madai yetu wasilipe?

Kwa hii asilimia 0.158% waliyotupa, ni sawa na mtu umdai shilingi milioni moja halafu yeye aweke mezani shilingi 1580 kujenga Imani!. Utajenga imani kwa buku jero out of a million shilling unayodaiwa?, angalau wangetoa 10% ya Trilion zetu 425 ili kujenga imani!!
 
  • Thanks
Reactions: SDG
.
Ndiyo, hiyo pesa ni cha juu lakini usisahau kuwa watatatoa ajira ya kudumu (kodi itapatikana), wataleta maendeleo (barabara, nyumba, maji, shule, kiwanda cha kuchakachua). Hayo yote yataongeza kukuwa kwa uchumi, kwasababu kama sehemu ina miundombinu biashara itaongezeka na ajira itaongezea zaidi, wenyewe wanaita 'snowball effect'.

Utakuta ile 400Tsh yote itakuwa imelipwa baada ya muda fulani, sasa nyinyi mlikuwa mnataka kututishia nyau na kama tungewasikiliza, sio tuu tungekosa maendeleo bali tungezidi kuibiwa.

Kuna kitu kingine ambacho wengi mnakisahau na hiki ni ile nguvu ya ushawishi wa nchi, leo Tanzania imerudi kwenye mstari kama ilivyokuwa kipindi cha nyerere. Nchi inaonekana makini, siyo shamba la bibi kama zamani. Leo hii watu hawawezi kuja kutuchezea kama zamani, inabidi wajipange, wajiulize mara mbili mbili, wawekezaji wa maana watataka kuja kwa kuwa wanajua watanzania ni watu makini.

Lugha za kujifariji hizi.
 
View attachment 613009
(Utiaji saini wa makubaliano ya awali, Ikulu Jana. Picha na Michuzi)​

Na. M. M. Mwanakijiji

Hawakutupeleka mahakamani. Hawakuamua kukusanya virago vyao na kuondoka na kufunga shughuli zao nchini kwa vile tumewakatalia kinachodhaniwa kuwa kilikuwa ni haki yao. Tuliambiwa hatukutakiwa kuwaambia “hapana” kwani wangekasirika; wangekasirika na sisi tungelipa! Tuliambiwa ilikuwa ni mwiko kuwakatalia wawekezaji wakubwa wa kimataifa na kwa vile wao ndio “wakubwa” basi sisi “wadogo” tulitakiwa tukubali tu kufanyiwa lolote, popote, vyovyote na yeyote.

Haubezwi Mchakato Tena Sasa Yanabezwa Matokeo

Leo kinachobezwa na ndugu zetu siyo mchakato tena; kinachobezwa siyo hatua za kulazimisha “wakubwa” kuja kuzungumza nasi kwa masharti yetu sisi wenyewe chini ya miembe yetu wenyewe. Kinachobezwa siyo kwamba hatukwenda kwenye mahoteli makubwa ya kimataifa na kukabishwa kwa mbwembwe kubwa huku tunaingizwa mjini. Hawabezi tena kuwa hatukwenda kwenye chumba cha hoteli kama ilivyokuwa kwenye Buzwagi na kuingizwa mjini. Kinachobezwa ndugu zangu ni matokeo ya mchakato huo ya kwamba mbona hayakuleta makubwa tuliyoahidiwa? Kwamba, tulisema tunadai matrilioni ya shilingi sasa mbona tumepewa karanga tu?

Bilioni Mia Saba si Haba

Kwanza ndugu zangu niweke jambo moja sawa sawa. Kuziita shilingi bilioni 700 kuwa ni punje tu ni kutokuwa wa kweli kwa uzito wa kiasi hicho cha fedha. Labda kuweza kuelewa kiasi hicho kinaweza kufanya nini kwenye sekta mbalimbali kunaweza kutusaidia kujua kama kweli hiki kiasi ni punje tu na cha kubezwa. Bajeti ya afya kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 ni shilingi 1,115,608,772,090. Ni karibu trilioni 1.1. Fedha ambazo zimetolewa kama “kishika uchumba” (kuonesha nia njema) ni sawa na shilingi bilioni 700 ya fedha zetu. Hii ni sawa na asilimia 62.7 ya bajeti ya wizara ya Afya peke yake. Yaani, ni zaidi ya nusu ya fedha zote ambazo zimepangiwa bajeti kwenye wizara ya afya! Na wapo wanaosema ni za kubeza?

Labda mfano mwingine utasaidia. Bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka huu kama ilivyosomwa na Dkt. Tizeba mwezi ilikuwa ni bilioni 267.865. Kiasi hicho ni kidogo mno kama alivyokosoa Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ambaye alifichua kuwa serikali kufika wakati ule wa bajeti ilikuwa imetoa asilimia 3.31 ya fedha za maendeleo zilizotengwa kwa ajili ya sekta ya kilimo. Kiasi cha fedha ambazo zinabezwa na ndugu zetu hawa ni karibu mara tatu ya bajeti nzima ya Wizara ya Kilimo! Kweli ni punje za kupuuzia, na ni kiasi cha kubeza hiki?

Labda mfano mwingine utasaidia. Bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka huu ni shilingi bilioni 623 kiasi ambacho kililalamikiwa Bungeni kuwa ni pungufu na kwa mara nyingine Zitto Kabwe aliikosoa kwa usahihi kabisa Serikali ya Magufuli ya kwanini kiasi hicho kimepungua hivyo ukizingatia kuwa hata fedha zilizokuwa zimeombwa mwaka jana na kuudhinishwa na Bunge ni asilimia 19 hivi ambazo zilikuwa zimepokelewa hadi wakati ule wa Bajeti kusomwa. Kiasi ambacho leo Serikali imekubaliana kupatikana kutoka katika majadiliano yake na Kampuni ya Barrick kufuatia ule mgogoro wa makinikia ni shilingi bilioni 700; hii tena ni zaidi ya bajeti ya Wizara nzima ya Serikali ya Muungano. Kweli hili ni la kubeza? Kweli hizi ni fedha za kupuuzia kwamba si kitu?

Siyo Kila Kitu ni Siasa

Sasa ninaelewa siasa na ninaelewa majadiliano. Siasa inawafanya wanasiasa kuangalia mambo kisiasa ili kupata alama za juu za kisiasa. Tukumbuke kuwa wale waliokuwa wanasema tutanyolewa hadi kucha walikuwa wanasema kama watu walioingiwa na hofu. Nakumbuka kuna watu walikuwa wanatuambia kabisa kwenye mitandao kuwa hatuwezi kuwalazimisha “wazungu” hawa na kwamba wazungu wana watu waliojipanga na wenye uzoefu mkubwa. Niliwabeza wakati ule watu hawa kwa sababu walikuwa na hisia za uduni (extreme inferiority complex). Hawa ni watu ambao mzungu akiwaambia kitu wao wanakubali tu na hawana ujasiri wa kusema “hapana” kwa sababu hawafikiri kabisa kuwa wazungu wanaweza kuwa matapeli na wanaweza kuwa wajanja sana kulinda maslahi yao!

Kilichokubaliwa ni Zaidi ya Fedha

Lakini ninafahamu kuwa habari nzima siyo hizo bilioni 700 tu; jambo kubwa limetokea jana katika mazungumzo tuliyoambiwa. Kilichotokea nyingine ni makubaliano ya mambo mbalimbali ambayo yalikuwa hayajawahi kufanyika huko nyuma. Wengine wanabeza hata haya na wanasema ni bure na kuwa hayawezekani. Hawa ni wale watu wa lile kabila la Wahatuwe! Ni watu ambao wanaamini kuwa hawawezi kufanya lolote, hawawezi kujenga hoja mbele ya wazungu, hawawezi kuwabana wazungu hadi wakabadilika rangi! Lakini ukweli – na mtasikia kwa watu wengine si muda mrefu – sehemu ya makubaliano hayo yalivyotangazwa kama yatatekelezwa ipasavyo yataleta heshima mpya kwa taifa na kwa Afrika kama siyo kwa nchi nyingine zinazoendelea. Uzoefu wetu wa kukaa mezani na makampuni makubwa kama Barrick na kuwalazimisha kuzungumza nasi kwenye uwanja wetu wa nyumba yatakuja kufundishwa kwa watu wengine na mataifa mengine. Si jambo dogo hata kidogo, na wala si la kubeza.

Ni lazima basi kutoa pongeze, pongezi zinapostahili. Ni kweli mtu anaweza kukosoa mambo fulani, lakini katika hili kwa kweli ukosoaji unaonesha tu ni kuwa ndugu zetu hawataki kumpongeza Magufuli kwa sababu wanadhania (kwa makosa) wakifanya hivyo basi watakuwa wamempa ‘kiki’ asiyostahili. Wanadhania kuwa wakisema kwa kweli hatua hizi zimeleta heshima kwetu kama taifa na zimetupa mahali pa kusimamia huko mbeleni basi kutamfanya Magufuli ajione ameweza. Lakini hili si lazima liwe hivyo, ukweli ni ukweli tu hata kama haupendezi. Sifuri jumlisha Tano ni ni Tano sasa huwezi kung’ang’ania iwe sifuri tu kwa sababu tano huipendi!

Pongezi zangu:

Binafsi napenda kuipongeza Serikali kwa mwanzo huu wa kurudisha heshima ya taifa katika kusimamia na kulinda raslimali za taifa letu. Pongezi zinaenda mbele zaidi kwa timu zote ambazo zimethubutu kufanya mambo ambayo hayakudhaniwa kuwa yanawezekana kufanyika katika nchi yetu hii. Nina uhakika wakati ufike au utakapofika wajumbe wa tume ya majadiliano wajulikane wazi na kupewa heshima wanayostahili hasa kwa kuweza kusimama kidede na wakubwa hawa. Naogopa kudhania hata kwa mbali kama wapingaji wa yaliyotangazwa jana wangekuwa kwenye timu ya wajumbe taifa lingeambulia nini. Inawezekana wangebanwa na wazungu hawa wangekusanya mpira kwapani na kuondoka na kutuambia “tumeshindwa, wazungu wametubana sana”!

Kilichotangazwa jana ni jambo la kupongeza, siyo jambo la kuonea haya. Wengine wansema tulidai trilioni 400 na ushee na sasa tumepewa bilioni 700 tu kweli tushangilie? Ndugu zangu kuna msemo wa wahenga kuwa ndege mmoja mkononi ana thamani kubwa kuliko ndege tisa mtini! Na hata hayo madai yanaitwa madai kwa sababu hiyo; na imeelezwa vizuri jana kuwa hii si hatua ya mwisho. Sehemu kubwa ambayo inaonekana imebakia na labda itatuliwa muda si mrefu ujao ni suala la kodi. Kwa yeyote anayejua masuala ya kodi si mambo madogo. Serikali inaweza kudai lakini haina maana anayedaiwa hana haki ya kusema “hadaiwi chochote” au “hadaiwi kiasi chote hicho”. Baada ya Serikali kutoa madai yake tena wazi zile Barrick na Acacia walikuwa na haki ya msingi katika biashara kupinga (object) dhidi ya madai hayo na walikuwa na haki ya kutoa nyaraka mbalimbali ambazo zingepitiwa ili kuona ni madai gani ni ya kweli na yapi si ya kweli au yapi yanahitaji kupitia (adjusted). Lakini pia pande zote mbili zina haki ya kuangalia namna ya kutatua mgogoro wa kodi. Hata kwenye makampuni au wafanyabiashara wa kawaida si wana haki ya kuhoji (dispute) madai ya kodi na wakati mwingine madai yao yanabadilishwa au wanaweza wakatoa pendekezo (offer) la kulipa kiasi gani kwa mkupuo au kwa utaratibu fulani? Sasa kwanini tudhanie kuwa hilo haliwezekani? Yaani kwa vile tumesema tunadaia trilioni 400 basi ni lazima zilipwe zote na kiasi chochote chini ya hapo ni kuwa cha kupuuzia?

Hizi ni Zama Mpya

Ndugu zangu, hizi ni zama mpya; ni zama ambazo baadhi ya vitu vinaenda kubadilika na ni vizuri watu wakae kujua vinabadilika. Wajue pia kuwa zama hizi bado zinatafuta mahali pake pa kushikilia. Kweli zipo hoja mbalimbali zinazoweza kutolewa kukosoa serikali na kwa haki kabisa serikali inapaswa kukosolewa. Kuna maeneo ambayo yanastahili kukosolewa na watu wanapaswa kukosoa. Lakini ni lazima na muhimu kukosoa kufanyike siyo kwa sababu ya chuki, hasira au ubaya fulani.

Hitimisho

Tunasubiria kwa hamu kuona hatua zaidi zikiendelea kuchukuliwa si kwenye madini tu bali kwenye sekta nyingine ili kuhakikisha Watanzania wanafaidika kwa kiwango cha juu kabisa na utajiri wa mali zao za asili; kwani wao ndio wawekezaji wakubwa kwenye jambo lolote linaloenda kufanywa. Kwani hakuna mwekezaji mkubwa kuliko mwenye raslimali zake. Ni lazima tujitambue hivyo, na ni lazima tujitendee hivyo. Tusijione kama siyo ‘wawekezaji’ na hawa watu wanaokuja na fedha ndio ‘wawekezaji’. Sisi ndio wawekezaji wakubwa; Tanzania ndio mwekezaji mkubwa zaidi.

Sasa kwanini tujione duni na kutetemeka mbele ya wawekezaji wadogo hata kama ni wazungu?

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
Katika WATU wanafiki na siwaelewi ni MZEE mwanakijiji mnafiki kabisa katika thread zake nyingi
 
Kama sio final, bado tunawadai Acacia pesa ngapi? Kwa nini Prof. Kabudi na/au Pres. Magufuli hawakutuambia jana kiasi cha deni lililobaki? Msingi wa 'good faith' ya US$ 300 million ni nini? Kwa nini hawakulipa 'good faith' ya US$ 500 million au US$ 100 million?
Umeambiwa kutakuwa na maongezi zaidi kuhusiana na hiyo dola milioni 300 pamoja na kodi za miaka ya nyuma.

Huwezi kuwapangia kiasi cha kulipa. Wangeamua kulipa dola bilioni moja mngesema kwanini hawajaamua kulipa dola bilioni 50!!.

Hamna na hamjawahi kuwa na mioyo yenye shukrani, mnaona mna haki sana ya kupata mambo fulani kana kwamba hapa duniani mpo nyinyi tu. Thankless human beings.
 
Hivi siku hizi kodi imekuwa ni negotiable? Mbona huku mtaani hawatupi mwanya wa ku-negotiate? BTW, hoa unatuambia tuwe na shukrani kwao si juzi Rais alikuwa anawasema kwamba wametufanya shamba la Bibi kwa muda mrefu, yani kutulipa 0.15 percent ya tunachowadai Leo ndo inaokuwa tunastahili kuwashukuru?
 
Wameshagoma leo HAWANA HELA YA KULIPA
 
Hivi ACACIA tulikuwa tunawadai pesa za good intention au deni kutokana na kutuibia?, Sasa kwa nini watulipe kwa kile tusichowadai lakini kwa kile tunachowadai ambalo ndo msingi haswaa wa madai yetu wasilipe?

Kwa hii asilimia 0.158% waliyotupa, ni sawa na mtu umdai shilingi milioni moja halafu yeye aweke mezani shilingi 1580 kujenga Imani!. Utajenga imani kwa buku jero out of a million shilling unayodaiwa?, angalau wangetoa 10% ya Trilion zetu 425 ili kujenga imani!!
Ngoja Prof CarBood atalitolea ufafanuz hili
 
Hivi siku hizi kodi imekuwa ni negotiable? Mbona huku mtaani hawatupi mwanya wa ku-negotiate? BTW, hoa unatuambia tuwe na shukrani kwao si juzi Rais alikuwa anawasema kwamba wametufanya shamba la Bibi kwa muda mrefu, yani kutulipa 0.15 percent ya tunachowadai Leo ndo inaokuwa tunastahili kuwashukuru?
Mbona mnaongelea pesa tu?. Kuna vipengele vingapi kwenye makubaliano ya serikali na barrick?.

Mmeshajiuliza kuhusu mabadiliko mazima kwenye sekta ya madini?. Tatizo akili zenu mmezitune kwenye ushabiki maandazi wa mitandaoni pasipo kuangalia mabadiliko makubwa ambayo yatailetea faida nchi.

Mwenye upeo mkubwa atajiuliza ni kwanini mheshimiwa JPM anataka na kwenye tanzanite pafanyike mabadiliko makubwa.

Mmekamatwa kabisa mawazo yenu na hizi bilioni za kodi, poleni sana.
 
Wameshagoma leo HAWANA HELA YA KULIPA
Kwa hiyo nyinyi ndio mtakaolipa kwa niaba yao??.

Serikali imeongea na wakubwa wao ambao ni barrick. Nyinyi kazi yenu ni kushirikiana nao katika kuandika barua zinazodai kuwa tutashtakiwa huko Ulaya. Bei yenu ni ndogo sana aisee.
 
Pesa ndo the main issue, ili zije chini huku kupunguza Makali ya maisha. Hizo story nyingine mbona zipo siku nyingi na haziwahi Saidia?
 
Kwani alosema halipi ni sisi au akashia?
 
Wamepunguziwa deni la kodi kwa zaidi ya 99% (maana wanayotulipa haifiki hata 1% ya kodi ya 425T tuliyokuwa tunadai). Basi kama hicho ni cha kupongezwa, tuombe na wafanya biashara wetu pale kariakoo wanao-struggle kulipa kodi wapunguziwe kodi kwa 99%.
Kariakoo thubutu acha waendelee kuishi kama mashetani
 
Mkuu Chige ujuha mzigo mzito sana halafu mtu anasifia kwamba kuambulia .15% au sawa na $3,434 kwa siku kwa miaka 20 baada ya mazungumzo ya miezi mitatu si kitu cha KUBEZA!!! Wakati kwa siku hao ACACIA walikuwa wanavuna dhahabu yenye thamani ya mamilioni.

Kweli si haba... 0.15% ya kile tulichosema tuna haki nacho!!!! Kweli si haba, manake tumekubali in other way round kwamba, mahesabu ya Acacia yapo right for at least 99% or else, kwanini tukubali kupata less than 1% ya kile tulichoambiwa tunadai?! Or it's all political stunt?!!

And look, katika kulazimisha mambo ionekane we're the winner tunaambiwa 700 billion wakati ni $300 Million!

Lini selling rate for non-cash imefikia sh. 2330?! For what I know, selling rate for non cash is less than TZS 2,200 lakini ili ionekane we're the winners, wametumia zaidi ya TZS 2300!

For actual selling rate for non cash, 300 million USD ni less than 660 Billion!! Sasa mkituambia ni 700 Billion, mjiandae kutuambia over 40 Billion zimepotelea wapi pale vitabu vitakaposoma 660 Billion
 
View attachment 613009
(Utiaji saini wa makubaliano ya awali, Ikulu Jana. Picha na Michuzi)​

Na. M. M. Mwanakijiji

Hawakutupeleka mahakamani. Hawakuamua kukusanya virago vyao na kuondoka na kufunga shughuli zao nchini kwa vile tumewakatalia kinachodhaniwa kuwa kilikuwa ni haki yao. Tuliambiwa hatukutakiwa kuwaambia “hapana” kwani wangekasirika; wangekasirika na sisi tungelipa! Tuliambiwa ilikuwa ni mwiko kuwakatalia wawekezaji wakubwa wa kimataifa na kwa vile wao ndio “wakubwa” basi sisi “wadogo” tulitakiwa tukubali tu kufanyiwa lolote, popote, vyovyote na yeyote.

Haubezwi Mchakato Tena Sasa Yanabezwa Matokeo

Leo kinachobezwa na ndugu zetu siyo mchakato tena; kinachobezwa siyo hatua za kulazimisha “wakubwa” kuja kuzungumza nasi kwa masharti yetu sisi wenyewe chini ya miembe yetu wenyewe. Kinachobezwa siyo kwamba hatukwenda kwenye mahoteli makubwa ya kimataifa na kukabishwa kwa mbwembwe kubwa huku tunaingizwa mjini. Hawabezi tena kuwa hatukwenda kwenye chumba cha hoteli kama ilivyokuwa kwenye Buzwagi na kuingizwa mjini. Kinachobezwa ndugu zangu ni matokeo ya mchakato huo ya kwamba mbona hayakuleta makubwa tuliyoahidiwa? Kwamba, tulisema tunadai matrilioni ya shilingi sasa mbona tumepewa karanga tu?

Bilioni Mia Saba si Haba

Kwanza ndugu zangu niweke jambo moja sawa sawa. Kuziita shilingi bilioni 700 kuwa ni punje tu ni kutokuwa wa kweli kwa uzito wa kiasi hicho cha fedha. Labda kuweza kuelewa kiasi hicho kinaweza kufanya nini kwenye sekta mbalimbali kunaweza kutusaidia kujua kama kweli hiki kiasi ni punje tu na cha kubezwa. Bajeti ya afya kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 ni shilingi 1,115,608,772,090. Ni karibu trilioni 1.1. Fedha ambazo zimetolewa kama “kishika uchumba” (kuonesha nia njema) ni sawa na shilingi bilioni 700 ya fedha zetu. Hii ni sawa na asilimia 62.7 ya bajeti ya wizara ya Afya peke yake. Yaani, ni zaidi ya nusu ya fedha zote ambazo zimepangiwa bajeti kwenye wizara ya afya! Na wapo wanaosema ni za kubeza?

Labda mfano mwingine utasaidia. Bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka huu kama ilivyosomwa na Dkt. Tizeba mwezi ilikuwa ni bilioni 267.865. Kiasi hicho ni kidogo mno kama alivyokosoa Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ambaye alifichua kuwa serikali kufika wakati ule wa bajeti ilikuwa imetoa asilimia 3.31 ya fedha za maendeleo zilizotengwa kwa ajili ya sekta ya kilimo. Kiasi cha fedha ambazo zinabezwa na ndugu zetu hawa ni karibu mara tatu ya bajeti nzima ya Wizara ya Kilimo! Kweli ni punje za kupuuzia, na ni kiasi cha kubeza hiki?

Labda mfano mwingine utasaidia. Bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka huu ni shilingi bilioni 623 kiasi ambacho kililalamikiwa Bungeni kuwa ni pungufu na kwa mara nyingine Zitto Kabwe aliikosoa kwa usahihi kabisa Serikali ya Magufuli ya kwanini kiasi hicho kimepungua hivyo ukizingatia kuwa hata fedha zilizokuwa zimeombwa mwaka jana na kuudhinishwa na Bunge ni asilimia 19 hivi ambazo zilikuwa zimepokelewa hadi wakati ule wa Bajeti kusomwa. Kiasi ambacho leo Serikali imekubaliana kupatikana kutoka katika majadiliano yake na Kampuni ya Barrick kufuatia ule mgogoro wa makinikia ni shilingi bilioni 700; hii tena ni zaidi ya bajeti ya Wizara nzima ya Serikali ya Muungano. Kweli hili ni la kubeza? Kweli hizi ni fedha za kupuuzia kwamba si kitu?

Siyo Kila Kitu ni Siasa

Sasa ninaelewa siasa na ninaelewa majadiliano. Siasa inawafanya wanasiasa kuangalia mambo kisiasa ili kupata alama za juu za kisiasa. Tukumbuke kuwa wale waliokuwa wanasema tutanyolewa hadi kucha walikuwa wanasema kama watu walioingiwa na hofu. Nakumbuka kuna watu walikuwa wanatuambia kabisa kwenye mitandao kuwa hatuwezi kuwalazimisha “wazungu” hawa na kwamba wazungu wana watu waliojipanga na wenye uzoefu mkubwa. Niliwabeza wakati ule watu hawa kwa sababu walikuwa na hisia za uduni (extreme inferiority complex). Hawa ni watu ambao mzungu akiwaambia kitu wao wanakubali tu na hawana ujasiri wa kusema “hapana” kwa sababu hawafikiri kabisa kuwa wazungu wanaweza kuwa matapeli na wanaweza kuwa wajanja sana kulinda maslahi yao!

Kilichokubaliwa ni Zaidi ya Fedha

Lakini ninafahamu kuwa habari nzima siyo hizo bilioni 700 tu; jambo kubwa limetokea jana katika mazungumzo tuliyoambiwa. Kilichotokea nyingine ni makubaliano ya mambo mbalimbali ambayo yalikuwa hayajawahi kufanyika huko nyuma. Wengine wanabeza hata haya na wanasema ni bure na kuwa hayawezekani. Hawa ni wale watu wa lile kabila la Wahatuwe! Ni watu ambao wanaamini kuwa hawawezi kufanya lolote, hawawezi kujenga hoja mbele ya wazungu, hawawezi kuwabana wazungu hadi wakabadilika rangi! Lakini ukweli – na mtasikia kwa watu wengine si muda mrefu – sehemu ya makubaliano hayo yalivyotangazwa kama yatatekelezwa ipasavyo yataleta heshima mpya kwa taifa na kwa Afrika kama siyo kwa nchi nyingine zinazoendelea. Uzoefu wetu wa kukaa mezani na makampuni makubwa kama Barrick na kuwalazimisha kuzungumza nasi kwenye uwanja wetu wa nyumba yatakuja kufundishwa kwa watu wengine na mataifa mengine. Si jambo dogo hata kidogo, na wala si la kubeza.

Ni lazima basi kutoa pongeze, pongezi zinapostahili. Ni kweli mtu anaweza kukosoa mambo fulani, lakini katika hili kwa kweli ukosoaji unaonesha tu ni kuwa ndugu zetu hawataki kumpongeza Magufuli kwa sababu wanadhania (kwa makosa) wakifanya hivyo basi watakuwa wamempa ‘kiki’ asiyostahili. Wanadhania kuwa wakisema kwa kweli hatua hizi zimeleta heshima kwetu kama taifa na zimetupa mahali pa kusimamia huko mbeleni basi kutamfanya Magufuli ajione ameweza. Lakini hili si lazima liwe hivyo, ukweli ni ukweli tu hata kama haupendezi. Sifuri jumlisha Tano ni ni Tano sasa huwezi kung’ang’ania iwe sifuri tu kwa sababu tano huipendi!

Pongezi zangu:

Binafsi napenda kuipongeza Serikali kwa mwanzo huu wa kurudisha heshima ya taifa katika kusimamia na kulinda raslimali za taifa letu. Pongezi zinaenda mbele zaidi kwa timu zote ambazo zimethubutu kufanya mambo ambayo hayakudhaniwa kuwa yanawezekana kufanyika katika nchi yetu hii. Nina uhakika wakati ufike au utakapofika wajumbe wa tume ya majadiliano wajulikane wazi na kupewa heshima wanayostahili hasa kwa kuweza kusimama kidede na wakubwa hawa. Naogopa kudhania hata kwa mbali kama wapingaji wa yaliyotangazwa jana wangekuwa kwenye timu ya wajumbe taifa lingeambulia nini. Inawezekana wangebanwa na wazungu hawa wangekusanya mpira kwapani na kuondoka na kutuambia “tumeshindwa, wazungu wametubana sana”!

Kilichotangazwa jana ni jambo la kupongeza, siyo jambo la kuonea haya. Wengine wansema tulidai trilioni 400 na ushee na sasa tumepewa bilioni 700 tu kweli tushangilie? Ndugu zangu kuna msemo wa wahenga kuwa ndege mmoja mkononi ana thamani kubwa kuliko ndege tisa mtini! Na hata hayo madai yanaitwa madai kwa sababu hiyo; na imeelezwa vizuri jana kuwa hii si hatua ya mwisho. Sehemu kubwa ambayo inaonekana imebakia na labda itatuliwa muda si mrefu ujao ni suala la kodi. Kwa yeyote anayejua masuala ya kodi si mambo madogo. Serikali inaweza kudai lakini haina maana anayedaiwa hana haki ya kusema “hadaiwi chochote” au “hadaiwi kiasi chote hicho”. Baada ya Serikali kutoa madai yake tena wazi zile Barrick na Acacia walikuwa na haki ya msingi katika biashara kupinga (object) dhidi ya madai hayo na walikuwa na haki ya kutoa nyaraka mbalimbali ambazo zingepitiwa ili kuona ni madai gani ni ya kweli na yapi si ya kweli au yapi yanahitaji kupitia (adjusted). Lakini pia pande zote mbili zina haki ya kuangalia namna ya kutatua mgogoro wa kodi. Hata kwenye makampuni au wafanyabiashara wa kawaida si wana haki ya kuhoji (dispute) madai ya kodi na wakati mwingine madai yao yanabadilishwa au wanaweza wakatoa pendekezo (offer) la kulipa kiasi gani kwa mkupuo au kwa utaratibu fulani? Sasa kwanini tudhanie kuwa hilo haliwezekani? Yaani kwa vile tumesema tunadaia trilioni 400 basi ni lazima zilipwe zote na kiasi chochote chini ya hapo ni kuwa cha kupuuzia?

Hizi ni Zama Mpya

Ndugu zangu, hizi ni zama mpya; ni zama ambazo baadhi ya vitu vinaenda kubadilika na ni vizuri watu wakae kujua vinabadilika. Wajue pia kuwa zama hizi bado zinatafuta mahali pake pa kushikilia. Kweli zipo hoja mbalimbali zinazoweza kutolewa kukosoa serikali na kwa haki kabisa serikali inapaswa kukosolewa. Kuna maeneo ambayo yanastahili kukosolewa na watu wanapaswa kukosoa. Lakini ni lazima na muhimu kukosoa kufanyike siyo kwa sababu ya chuki, hasira au ubaya fulani.

Hitimisho

Tunasubiria kwa hamu kuona hatua zaidi zikiendelea kuchukuliwa si kwenye madini tu bali kwenye sekta nyingine ili kuhakikisha Watanzania wanafaidika kwa kiwango cha juu kabisa na utajiri wa mali zao za asili; kwani wao ndio wawekezaji wakubwa kwenye jambo lolote linaloenda kufanywa. Kwani hakuna mwekezaji mkubwa kuliko mwenye raslimali zake. Ni lazima tujitambue hivyo, na ni lazima tujitendee hivyo. Tusijione kama siyo ‘wawekezaji’ na hawa watu wanaokuja na fedha ndio ‘wawekezaji’. Sisi ndio wawekezaji wakubwa; Tanzania ndio mwekezaji mkubwa zaidi.

Sasa kwanini tujione duni na kutetemeka mbele ya wawekezaji wadogo hata kama ni wazungu?

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com

Nadhani Mwanakijiji mtizamo wako unaegemea upande mmoja. Kama kweli tulikuwa tunadai matrilioni kadhaa na baadae tukaishia kupewa vibilioni kadhaa, na tukakubaliana navyo, basi maana yake inaweza kuwa hizi zifuatazo:
1) Hatukuwa na uhakika na madai yetu na baada ya kueleweshwa tukafikia kukubaliana na ukweli wa muwekezaji
2) Taratibu zilizotumika katika sakata hili hazikuwa sahihi upande wetu na hivyo kutuweka katika hatari ya kushtakiwa na kulipa gharama kubwa. Hili matokeo yake ni kufikia makubaliano ya kutoiaibisha serikali na kuendelea kujenga mahusiano mazuri ya kibiashara na wawekezaji kwa kupata japo kifuta mcahozi (wewe umekiita kifunga uchumba, sijui kwa nani).

Hivyo kutokana na kwamba hili limeonyesha kanuru kutokea mbali sana, ni busara kutafakari kwa kina ni wapi tulipaswa na tunapaswa kufanya bora zaidi ili tuweze kutemebea kifua mbele tofauti na ilivyo sasa.

Tindu Lisu alipendekeza kujitoa MIGA kabla ya kulikabili hili, je ingekuwa na msaada wowote? Nini kingeweza kufanyika tofauti japo kiwezeshe kupata mapato yaliyoibiwa na hii kampuni kwa miaka yote hiyo? Miezi zaidi ya miweili kujadili hili suala sio michache kufikia makubaliano ya kupewa 0.1% na ahadi ya majadiliano baadae ambaye ukomo wake na utayari wake hauwezi kuwa bayana.
 
Yaani MTU unamdai sh. Laki moja na mnafanya kikao cha miezi 3 nyumbani kwako ukimhudumia, halafu mwisho wa siku anakupa sh 150/= kuonyesha "nia njema" halafu unashangilia sana na kusema si haba!
 
Pesa ndo the main issue, ili zije chini huku kupunguza Makali ya maisha. Hizo story nyingine mbona zipo siku nyingi na haziwahi Saidia?
Uzuri wa JPM ni mtu asiyetishwa na chochote kinachokuja mbele yake. Angewasikiliza watu waoga, waongo na wanafiki kama nyinyi, hata haya majadiliano yaliyochukua miezi miwili yasingefanyika.
 
Mkuu trilion zetu 425 ziltalipwa lini?, hilo ndo swali la msingi!
Hivi unajua kwamba Shilingi Trilion 425 ni bajeti ya nchi kwa niaka 14 bila thumni yoyote ya fedha za wahisani?. Sasa utasemaje tusiangalie fedha tu?
 
Uzuri wa JPM ni mtu asiyetishwa na chochote kinachokuja mbele yake. Angewasikiliza watu waoga, waongo na wanafiki kama nyinyi, hata haya majadiliano yaliyochukua miezi miwili yasingefanyika.
Unaweza fikiri unamsifia Rais lakini unachofanya ni kinyume, Rais mzuri husikiliza watu, especially wale wanacritisize, ili aweze kuwaelewesha na kutetea maamuzi yake. BTW, huko kutotusikiliza sisi waoga, waongo na wanafiki ingekuwa kumeshaleta ahueni yoyote ya maisha mbona tungeona poa tu!
 
Hongera sana na pole kwa kujifariji. Kama haujui acacia wameshasema hawana pesa ya kuchezea kuwalipa mlitaka nendeni kisutu
 
Back
Top Bottom