Sh. Bilioni 700 si Haba na Wanaobeza Vibaba

Sh. Bilioni 700 si Haba na Wanaobeza Vibaba

Mkuu trilion zetu 425 ziltalipwa lini?, hilo ndo swali la msingi!
Hivi unajua kwamba Shilingi Trilion 425 ni bajeti ya nchi kwa niaka 14 bila thumni yoyote ya fedha za wahisani?. Sasa utasemaje tusiangalie fedha tu?
Hela wabongo tumezijua lini?. Tangu tupate uhuru tumeshapewa shilingi ngapi na hao wazungu?. Tumezifanyia kipi cha maana zaidi ya ufuska na ulevi?.

Halafu tambueni kuwa mnajifurahisha tu nafsi zenu mnapoamua kuongea kwa kutumia sarcasm. It won't do you no good.
 
Unaweza fikiri unamsifia Rais lakini unachofanya ni kinyume, Rais mzuri husikiliza watu, especially wale wanacritisize, ili aweze kuwaelewesha na kutetea maamuzi yake. BTW, huko kutotusikiliza sisi waoga, waongo na wanafiki ingekuwa kumeshaleta ahueni yoyote ya maisha mbona tungeona poa tu!
Sio kwamba rais hawasikilizi watu, ila anao uwezo wa kuitambua ipi ni kauli ya kiungwana na ii ni kauli ya kinafiki.

Huyo mwenye chama cha ACT kwa mfano, alishiriki katika kuizunguka wizara ya uchukuzi na mawasiliano halafu anamtumia ujumbe waziri Mbarawa kama anafahamu chochote kuhusiana na suala fulani nyeti. Usalama wa taifa wanakuwa wanamchora, mkuu JPM nae anamchora pia.

Hiyo ndio aina ya uchangiaji wa mawazo ulio katika hali ya kinafiki kutoka kwa watu ambao walitegemewa wawe na mawazo yenye lengo chanya, lakini ni aina ya watu ambao wanapata furaha wanapomuona kiongozi mkuu na serikali yake wakiwa wanakwama kwenye mambo nyeti!!.

That is bull shit....
 
View attachment 613009
(Utiaji saini wa makubaliano ya awali, Ikulu Jana. Picha na Michuzi)​

Na. M. M. Mwanakijiji

Hawakutupeleka mahakamani. Hawakuamua kukusanya virago vyao na kuondoka na kufunga shughuli zao nchini kwa vile tumewakatalia kinachodhaniwa kuwa kilikuwa ni haki yao. Tuliambiwa hatukutakiwa kuwaambia “hapana” kwani wangekasirika; wangekasirika na sisi tungelipa! Tuliambiwa ilikuwa ni mwiko kuwakatalia wawekezaji wakubwa wa kimataifa na kwa vile wao ndio “wakubwa” basi sisi “wadogo” tulitakiwa tukubali tu kufanyiwa lolote, popote, vyovyote na yeyote.

Haubezwi Mchakato Tena Sasa Yanabezwa Matokeo

Leo kinachobezwa na ndugu zetu siyo mchakato tena; kinachobezwa siyo hatua za kulazimisha “wakubwa” kuja kuzungumza nasi kwa masharti yetu sisi wenyewe chini ya miembe yetu wenyewe. Kinachobezwa siyo kwamba hatukwenda kwenye mahoteli makubwa ya kimataifa na kukabishwa kwa mbwembwe kubwa huku tunaingizwa mjini. Hawabezi tena kuwa hatukwenda kwenye chumba cha hoteli kama ilivyokuwa kwenye Buzwagi na kuingizwa mjini. Kinachobezwa ndugu zangu ni matokeo ya mchakato huo ya kwamba mbona hayakuleta makubwa tuliyoahidiwa? Kwamba, tulisema tunadai matrilioni ya shilingi sasa mbona tumepewa karanga tu?

Bilioni Mia Saba si Haba

Kwanza ndugu zangu niweke jambo moja sawa sawa. Kuziita shilingi bilioni 700 kuwa ni punje tu ni kutokuwa wa kweli kwa uzito wa kiasi hicho cha fedha. Labda kuweza kuelewa kiasi hicho kinaweza kufanya nini kwenye sekta mbalimbali kunaweza kutusaidia kujua kama kweli hiki kiasi ni punje tu na cha kubezwa. Bajeti ya afya kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 ni shilingi 1,115,608,772,090. Ni karibu trilioni 1.1. Fedha ambazo zimetolewa kama “kishika uchumba” (kuonesha nia njema) ni sawa na shilingi bilioni 700 ya fedha zetu. Hii ni sawa na asilimia 62.7 ya bajeti ya wizara ya Afya peke yake. Yaani, ni zaidi ya nusu ya fedha zote ambazo zimepangiwa bajeti kwenye wizara ya afya! Na wapo wanaosema ni za kubeza?

Labda mfano mwingine utasaidia. Bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka huu kama ilivyosomwa na Dkt. Tizeba mwezi ilikuwa ni bilioni 267.865. Kiasi hicho ni kidogo mno kama alivyokosoa Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ambaye alifichua kuwa serikali kufika wakati ule wa bajeti ilikuwa imetoa asilimia 3.31 ya fedha za maendeleo zilizotengwa kwa ajili ya sekta ya kilimo. Kiasi cha fedha ambazo zinabezwa na ndugu zetu hawa ni karibu mara tatu ya bajeti nzima ya Wizara ya Kilimo! Kweli ni punje za kupuuzia, na ni kiasi cha kubeza hiki?

Labda mfano mwingine utasaidia. Bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka huu ni shilingi bilioni 623 kiasi ambacho kililalamikiwa Bungeni kuwa ni pungufu na kwa mara nyingine Zitto Kabwe aliikosoa kwa usahihi kabisa Serikali ya Magufuli ya kwanini kiasi hicho kimepungua hivyo ukizingatia kuwa hata fedha zilizokuwa zimeombwa mwaka jana na kuudhinishwa na Bunge ni asilimia 19 hivi ambazo zilikuwa zimepokelewa hadi wakati ule wa Bajeti kusomwa. Kiasi ambacho leo Serikali imekubaliana kupatikana kutoka katika majadiliano yake na Kampuni ya Barrick kufuatia ule mgogoro wa makinikia ni shilingi bilioni 700; hii tena ni zaidi ya bajeti ya Wizara nzima ya Serikali ya Muungano. Kweli hili ni la kubeza? Kweli hizi ni fedha za kupuuzia kwamba si kitu?

Siyo Kila Kitu ni Siasa

Sasa ninaelewa siasa na ninaelewa majadiliano. Siasa inawafanya wanasiasa kuangalia mambo kisiasa ili kupata alama za juu za kisiasa. Tukumbuke kuwa wale waliokuwa wanasema tutanyolewa hadi kucha walikuwa wanasema kama watu walioingiwa na hofu. Nakumbuka kuna watu walikuwa wanatuambia kabisa kwenye mitandao kuwa hatuwezi kuwalazimisha “wazungu” hawa na kwamba wazungu wana watu waliojipanga na wenye uzoefu mkubwa. Niliwabeza wakati ule watu hawa kwa sababu walikuwa na hisia za uduni (extreme inferiority complex). Hawa ni watu ambao mzungu akiwaambia kitu wao wanakubali tu na hawana ujasiri wa kusema “hapana” kwa sababu hawafikiri kabisa kuwa wazungu wanaweza kuwa matapeli na wanaweza kuwa wajanja sana kulinda maslahi yao!

Kilichokubaliwa ni Zaidi ya Fedha

Lakini ninafahamu kuwa habari nzima siyo hizo bilioni 700 tu; jambo kubwa limetokea jana katika mazungumzo tuliyoambiwa. Kilichotokea nyingine ni makubaliano ya mambo mbalimbali ambayo yalikuwa hayajawahi kufanyika huko nyuma. Wengine wanabeza hata haya na wanasema ni bure na kuwa hayawezekani. Hawa ni wale watu wa lile kabila la Wahatuwe! Ni watu ambao wanaamini kuwa hawawezi kufanya lolote, hawawezi kujenga hoja mbele ya wazungu, hawawezi kuwabana wazungu hadi wakabadilika rangi! Lakini ukweli – na mtasikia kwa watu wengine si muda mrefu – sehemu ya makubaliano hayo yalivyotangazwa kama yatatekelezwa ipasavyo yataleta heshima mpya kwa taifa na kwa Afrika kama siyo kwa nchi nyingine zinazoendelea. Uzoefu wetu wa kukaa mezani na makampuni makubwa kama Barrick na kuwalazimisha kuzungumza nasi kwenye uwanja wetu wa nyumba yatakuja kufundishwa kwa watu wengine na mataifa mengine. Si jambo dogo hata kidogo, na wala si la kubeza.

Ni lazima basi kutoa pongeze, pongezi zinapostahili. Ni kweli mtu anaweza kukosoa mambo fulani, lakini katika hili kwa kweli ukosoaji unaonesha tu ni kuwa ndugu zetu hawataki kumpongeza Magufuli kwa sababu wanadhania (kwa makosa) wakifanya hivyo basi watakuwa wamempa ‘kiki’ asiyostahili. Wanadhania kuwa wakisema kwa kweli hatua hizi zimeleta heshima kwetu kama taifa na zimetupa mahali pa kusimamia huko mbeleni basi kutamfanya Magufuli ajione ameweza. Lakini hili si lazima liwe hivyo, ukweli ni ukweli tu hata kama haupendezi. Sifuri jumlisha Tano ni ni Tano sasa huwezi kung’ang’ania iwe sifuri tu kwa sababu tano huipendi!

Pongezi zangu:

Binafsi napenda kuipongeza Serikali kwa mwanzo huu wa kurudisha heshima ya taifa katika kusimamia na kulinda raslimali za taifa letu. Pongezi zinaenda mbele zaidi kwa timu zote ambazo zimethubutu kufanya mambo ambayo hayakudhaniwa kuwa yanawezekana kufanyika katika nchi yetu hii. Nina uhakika wakati ufike au utakapofika wajumbe wa tume ya majadiliano wajulikane wazi na kupewa heshima wanayostahili hasa kwa kuweza kusimama kidede na wakubwa hawa. Naogopa kudhania hata kwa mbali kama wapingaji wa yaliyotangazwa jana wangekuwa kwenye timu ya wajumbe taifa lingeambulia nini. Inawezekana wangebanwa na wazungu hawa wangekusanya mpira kwapani na kuondoka na kutuambia “tumeshindwa, wazungu wametubana sana”!

Kilichotangazwa jana ni jambo la kupongeza, siyo jambo la kuonea haya. Wengine wansema tulidai trilioni 400 na ushee na sasa tumepewa bilioni 700 tu kweli tushangilie? Ndugu zangu kuna msemo wa wahenga kuwa ndege mmoja mkononi ana thamani kubwa kuliko ndege tisa mtini! Na hata hayo madai yanaitwa madai kwa sababu hiyo; na imeelezwa vizuri jana kuwa hii si hatua ya mwisho. Sehemu kubwa ambayo inaonekana imebakia na labda itatuliwa muda si mrefu ujao ni suala la kodi. Kwa yeyote anayejua masuala ya kodi si mambo madogo. Serikali inaweza kudai lakini haina maana anayedaiwa hana haki ya kusema “hadaiwi chochote” au “hadaiwi kiasi chote hicho”. Baada ya Serikali kutoa madai yake tena wazi zile Barrick na Acacia walikuwa na haki ya msingi katika biashara kupinga (object) dhidi ya madai hayo na walikuwa na haki ya kutoa nyaraka mbalimbali ambazo zingepitiwa ili kuona ni madai gani ni ya kweli na yapi si ya kweli au yapi yanahitaji kupitia (adjusted). Lakini pia pande zote mbili zina haki ya kuangalia namna ya kutatua mgogoro wa kodi. Hata kwenye makampuni au wafanyabiashara wa kawaida si wana haki ya kuhoji (dispute) madai ya kodi na wakati mwingine madai yao yanabadilishwa au wanaweza wakatoa pendekezo (offer) la kulipa kiasi gani kwa mkupuo au kwa utaratibu fulani? Sasa kwanini tudhanie kuwa hilo haliwezekani? Yaani kwa vile tumesema tunadaia trilioni 400 basi ni lazima zilipwe zote na kiasi chochote chini ya hapo ni kuwa cha kupuuzia?

Hizi ni Zama Mpya

Ndugu zangu, hizi ni zama mpya; ni zama ambazo baadhi ya vitu vinaenda kubadilika na ni vizuri watu wakae kujua vinabadilika. Wajue pia kuwa zama hizi bado zinatafuta mahali pake pa kushikilia. Kweli zipo hoja mbalimbali zinazoweza kutolewa kukosoa serikali na kwa haki kabisa serikali inapaswa kukosolewa. Kuna maeneo ambayo yanastahili kukosolewa na watu wanapaswa kukosoa. Lakini ni lazima na muhimu kukosoa kufanyike siyo kwa sababu ya chuki, hasira au ubaya fulani.

Hitimisho

Tunasubiria kwa hamu kuona hatua zaidi zikiendelea kuchukuliwa si kwenye madini tu bali kwenye sekta nyingine ili kuhakikisha Watanzania wanafaidika kwa kiwango cha juu kabisa na utajiri wa mali zao za asili; kwani wao ndio wawekezaji wakubwa kwenye jambo lolote linaloenda kufanywa. Kwani hakuna mwekezaji mkubwa kuliko mwenye raslimali zake. Ni lazima tujitambue hivyo, na ni lazima tujitendee hivyo. Tusijione kama siyo ‘wawekezaji’ na hawa watu wanaokuja na fedha ndio ‘wawekezaji’. Sisi ndio wawekezaji wakubwa; Tanzania ndio mwekezaji mkubwa zaidi.

Sasa kwanini tujione duni na kutetemeka mbele ya wawekezaji wadogo hata kama ni wazungu?

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
Hawawei lipa UPFRONT. nadhani unaelewa. Kwa hiyo wata spread over yrs.Na kwa vile ni good faith KULE ULAYA JAMAA WATAKUWA VERY CLEAN kuwa wansaidia partner ktk tuta na wanaweza sogeza kiasi kikubwa mbele sana ili wakitumie kuturubuni njaa inapouma sana .Hadi wafikie mahali pa kuwapa 50/50, watawaachia mgodi unaokuwa zaidi ya nusu ya pato la taifa kisha wao wanawawekea mtamboa mtakaolipia kuchakachua kinikia kwa bei mtakimbia.
 
Katika hili, vya kupongeza vipo vingi, tuache GUBU jamani.
Huko tuendelee kukomaa, lakini tusisahau kuhamishia majeshi kwingine... mfano vyama vya ushirika vya wakulima, baba fukua kuanzia 1990's.
Hivi vya wakulima wa tumbaku, kahawa, pamba, korosho n.k,huku kuna majini watu, wamepiga balaa.
Watumishi hewa. feki na madini umeshapatifua.. tifua na huku jembe. Tunakuaminia
 
Hata kama maongezi hayataendelea, bado makubaliano mengine tuliyokubaliana nao ni makubwa mono na bora hata Mara Mia kuliko bilioni 700. Yaani kwenye mgogoro nao hawatupeleki kwenye mahakama zao. Wabongo kuajiriwa kwenye top management, kulipa ongezeko la mrahaba wa Serikali, fedha ziwekwe kwenye mabenki yaliyopo Tsnzania, ujenzi wa barabara ya lami to Mwanza na hiyo 50-50.
Ni kwa sababu hatujui tu masuala ya kiuchumi lakini hii italeta heshima kubwa sana kwa Tanzania duniani hasa kutokana kwa Waafrika wenzetu and sooner or later a Magufuli is now going to be a reference in academic fields throughout the world mostly from developing countries.
Toa pumba zako hapa, watu tuna hasira na noah zetu we unaleta story za barabara za mwanza
 
Wazee wa MIGA sijui wanafikiria vipi juu ya 16% za mrahaba, gawanyo la 50/50, maboresho maisha ya wafanyakazi migodini, na mambo kedekede yanayotarajiwa.
Mm nawaza noah yangu ya silver
 
Kwa akili yako unafikiri barick wamefikia haya makubaliano bila acacia kujua?Yani barick ajipangie na kukubali tu kuwa tutalipa USD 300million?Hizo za kwenda huko ni mbwembwe tu.Acacia na barick kitu kimoja
FB_IMG_1508504943719.jpg
 
Hao wanaitwa wazee wa kupinga. Na kwa sababu ni ushindi mkubwa tangu jana wameongeza juhudi za kukosoa kwenye mitandao.
Hawazungumzi makubwa tuliyo win kwenye mazungumzo, wanaangalia pa kukosoa wapi! Shame!
Hata wazungu kukubali kutoa bill 700 ni uthibitisho kwamba ni kweli walikuwa wanadaiwa kodi, regardless of the amount, jambo ambalo bado ni ushindi kwa hoja yetu.
Nafikiri shida hapa ni CCM kinapingwa mkuu wala Siyo JPM maana aliyetengeneza matatizo leo Ndiyo anajitutumua kuyatatua akiwa mwenyewe. Pia awali walisema wanadai trillion Mia nne na leo tunaahidiwa billion mia Saba kama zawadi ambayo Siyo lengo la majadiliano.Tunahitaji katiba mpya ayse rais apunguziwe Majukumu na kuwe na taasisi zisizo na hofu kwa nyingine TUWAJIBISHANE
 
Tunachoshangaa ni kuwa report ya awali kabisa ilisema Tril 108, baadaye kodi ikawa Tril 425, leo tunaambiwa tutasaidiwa kwa kupewa Bil 660 as a show of good faith, hatuambiwi hii good faith, tafsiri yake nini! eti tunashangilia..!

Na isitoshe, "All proposals are subject to review and approval by the Independent Committee of Acacia's Board of Directors and Shareholders".

Sasa ktk ku-review si wanaweza kubadili vipengere fulani fulani wanavyoona sio muafaka kwao? Ni mapema mno kuanza kushangilia hii game.
 
Hivi kwanini barick wametumia nguvu nyingi mfano hadi kuleta wajumbe nguli kwenye meza ya majadiliano na sio acacia?
 
Hivi kwanini barick wametumia nguvu nyingi mfano hadi kuleta wajumbe nguli kwenye meza ya majadiliano na sio acacia?
Kulinda hisa zake zisiendelee kuporomoka. Na kwao sasa hivi inaonekana ilikuwa kosa kubwa sana kuwekeza Tanzania maana imewagharimu sana. Wamepoteza mamilioni ya pesa kutokana na kuwekeza Tanzania. Hata hivyo wanafanya kila jitihada ili kuweza kuondoka.
 
Tunachoshangaa ni kuwa report ya awali kabisa ilisema Tril 108, baadaye kodi ikawa Tril 425, leo tunaambiwa tutasaidiwa kwa kupewa Bil 660 as a show of good faith, hatuambiwi hii good faith, tafsiri yake nini! eti tunashangilia..!

Na isitoshe, "All proposals are subject to review and approval by the Independent Committee of Acacia's Board of Directors and Shareholders".

Sasa ktk ku-review si wanaweza kubadili vipengere fulani fulani wanavyoona sio muafaka kwao? Ni mapema mno kuanza kushangilia hii game.
Upo sahihi. Maana yake ni kuwa hawana uwezo wa kuingilia maamuzi ya boadi ya Acacia. Barrick itabidi wakafanye jitihada ya kuishawishi bodi na bodi ione maamuzi hayo yana tija. Ni lazima bodi nzima na wanahisa wote waridhie.
 
Kulinda hisa zake zisiendelee kuporomoka. Na kwao sasa hivi inaonekana ilikuwa kosa kubwa sana kuwekeza Tanzania maana imewagharimu sana. Wamepoteza mamilioni ya pesa kutokana na kuwekeza Tanzania. Hata hivyo wanafanya kila jitihada ili kuweza kuondoka.
Kwahiyo acacia hawapat hasara na hili jambo?

posti fromu Nokia kitochi yuzingi jamii forum
 
Hivi hizi pesa za " Good faith" ambazo kimsingi siyo msingi wa madai yetu ya Trilion 425, Je wasipoitoa tunaweza kuidai mahakamani?
 
Back
Top Bottom