Sh. Bilioni 700 si Haba na Wanaobeza Vibaba

Sh. Bilioni 700 si Haba na Wanaobeza Vibaba

Kwahiyo acacia hawapat hasara na hili jambo?

posti fromu Nokia kitochi yuzingi jamii forum
Acacia kiasilimia wamepata hasara kubwa zaidi kuliko Barrick lakini kwa uwingi wa fedha Barrick wamepata hasara kubwa zaidi. Sikumbuki capitalization ya Barrick na Acacia kwenye stock markets. Lakini Barrick ina zaidi ya mara 10 ya Acacia. Ufahamu pia ndani ya Acacia Barrick wana karibu 64% ya umiliki. Kwa hiyo Barrick wanapata hasara mara mbili.
 
View attachment 613009
(Utiaji saini wa makubaliano ya awali, Ikulu Jana. Picha na Michuzi)​

Na. M. M. Mwanakijiji

Hawakutupeleka mahakamani. Hawakuamua kukusanya virago vyao na kuondoka na kufunga shughuli zao nchini kwa vile tumewakatalia kinachodhaniwa kuwa kilikuwa ni haki yao. Tuliambiwa hatukutakiwa kuwaambia “hapana” kwani wangekasirika; wangekasirika na sisi tungelipa! Tuliambiwa ilikuwa ni mwiko kuwakatalia wawekezaji wakubwa wa kimataifa na kwa vile wao ndio “wakubwa” basi sisi “wadogo” tulitakiwa tukubali tu kufanyiwa lolote, popote, vyovyote na yeyote.

Haubezwi Mchakato Tena Sasa Yanabezwa Matokeo

Leo kinachobezwa na ndugu zetu siyo mchakato tena; kinachobezwa siyo hatua za kulazimisha “wakubwa” kuja kuzungumza nasi kwa masharti yetu sisi wenyewe chini ya miembe yetu wenyewe. Kinachobezwa siyo kwamba hatukwenda kwenye mahoteli makubwa ya kimataifa na kukabishwa kwa mbwembwe kubwa huku tunaingizwa mjini. Hawabezi tena kuwa hatukwenda kwenye chumba cha hoteli kama ilivyokuwa kwenye Buzwagi na kuingizwa mjini. Kinachobezwa ndugu zangu ni matokeo ya mchakato huo ya kwamba mbona hayakuleta makubwa tuliyoahidiwa? Kwamba, tulisema tunadai matrilioni ya shilingi sasa mbona tumepewa karanga tu?

Bilioni Mia Saba si Haba

Kwanza ndugu zangu niweke jambo moja sawa sawa. Kuziita shilingi bilioni 700 kuwa ni punje tu ni kutokuwa wa kweli kwa uzito wa kiasi hicho cha fedha. Labda kuweza kuelewa kiasi hicho kinaweza kufanya nini kwenye sekta mbalimbali kunaweza kutusaidia kujua kama kweli hiki kiasi ni punje tu na cha kubezwa. Bajeti ya afya kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 ni shilingi 1,115,608,772,090. Ni karibu trilioni 1.1. Fedha ambazo zimetolewa kama “kishika uchumba” (kuonesha nia njema) ni sawa na shilingi bilioni 700 ya fedha zetu. Hii ni sawa na asilimia 62.7 ya bajeti ya wizara ya Afya peke yake. Yaani, ni zaidi ya nusu ya fedha zote ambazo zimepangiwa bajeti kwenye wizara ya afya! Na wapo wanaosema ni za kubeza?

Labda mfano mwingine utasaidia. Bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka huu kama ilivyosomwa na Dkt. Tizeba mwezi ilikuwa ni bilioni 267.865. Kiasi hicho ni kidogo mno kama alivyokosoa Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ambaye alifichua kuwa serikali kufika wakati ule wa bajeti ilikuwa imetoa asilimia 3.31 ya fedha za maendeleo zilizotengwa kwa ajili ya sekta ya kilimo. Kiasi cha fedha ambazo zinabezwa na ndugu zetu hawa ni karibu mara tatu ya bajeti nzima ya Wizara ya Kilimo! Kweli ni punje za kupuuzia, na ni kiasi cha kubeza hiki?

Labda mfano mwingine utasaidia. Bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka huu ni shilingi bilioni 623 kiasi ambacho kililalamikiwa Bungeni kuwa ni pungufu na kwa mara nyingine Zitto Kabwe aliikosoa kwa usahihi kabisa Serikali ya Magufuli ya kwanini kiasi hicho kimepungua hivyo ukizingatia kuwa hata fedha zilizokuwa zimeombwa mwaka jana na kuudhinishwa na Bunge ni asilimia 19 hivi ambazo zilikuwa zimepokelewa hadi wakati ule wa Bajeti kusomwa. Kiasi ambacho leo Serikali imekubaliana kupatikana kutoka katika majadiliano yake na Kampuni ya Barrick kufuatia ule mgogoro wa makinikia ni shilingi bilioni 700; hii tena ni zaidi ya bajeti ya Wizara nzima ya Serikali ya Muungano. Kweli hili ni la kubeza? Kweli hizi ni fedha za kupuuzia kwamba si kitu?

Siyo Kila Kitu ni Siasa

Sasa ninaelewa siasa na ninaelewa majadiliano. Siasa inawafanya wanasiasa kuangalia mambo kisiasa ili kupata alama za juu za kisiasa. Tukumbuke kuwa wale waliokuwa wanasema tutanyolewa hadi kucha walikuwa wanasema kama watu walioingiwa na hofu. Nakumbuka kuna watu walikuwa wanatuambia kabisa kwenye mitandao kuwa hatuwezi kuwalazimisha “wazungu” hawa na kwamba wazungu wana watu waliojipanga na wenye uzoefu mkubwa. Niliwabeza wakati ule watu hawa kwa sababu walikuwa na hisia za uduni (extreme inferiority complex). Hawa ni watu ambao mzungu akiwaambia kitu wao wanakubali tu na hawana ujasiri wa kusema “hapana” kwa sababu hawafikiri kabisa kuwa wazungu wanaweza kuwa matapeli na wanaweza kuwa wajanja sana kulinda maslahi yao!

Kilichokubaliwa ni Zaidi ya Fedha

Lakini ninafahamu kuwa habari nzima siyo hizo bilioni 700 tu; jambo kubwa limetokea jana katika mazungumzo tuliyoambiwa. Kilichotokea nyingine ni makubaliano ya mambo mbalimbali ambayo yalikuwa hayajawahi kufanyika huko nyuma. Wengine wanabeza hata haya na wanasema ni bure na kuwa hayawezekani. Hawa ni wale watu wa lile kabila la Wahatuwe! Ni watu ambao wanaamini kuwa hawawezi kufanya lolote, hawawezi kujenga hoja mbele ya wazungu, hawawezi kuwabana wazungu hadi wakabadilika rangi! Lakini ukweli – na mtasikia kwa watu wengine si muda mrefu – sehemu ya makubaliano hayo yalivyotangazwa kama yatatekelezwa ipasavyo yataleta heshima mpya kwa taifa na kwa Afrika kama siyo kwa nchi nyingine zinazoendelea. Uzoefu wetu wa kukaa mezani na makampuni makubwa kama Barrick na kuwalazimisha kuzungumza nasi kwenye uwanja wetu wa nyumba yatakuja kufundishwa kwa watu wengine na mataifa mengine. Si jambo dogo hata kidogo, na wala si la kubeza.

Ni lazima basi kutoa pongeze, pongezi zinapostahili. Ni kweli mtu anaweza kukosoa mambo fulani, lakini katika hili kwa kweli ukosoaji unaonesha tu ni kuwa ndugu zetu hawataki kumpongeza Magufuli kwa sababu wanadhania (kwa makosa) wakifanya hivyo basi watakuwa wamempa ‘kiki’ asiyostahili. Wanadhania kuwa wakisema kwa kweli hatua hizi zimeleta heshima kwetu kama taifa na zimetupa mahali pa kusimamia huko mbeleni basi kutamfanya Magufuli ajione ameweza. Lakini hili si lazima liwe hivyo, ukweli ni ukweli tu hata kama haupendezi. Sifuri jumlisha Tano ni ni Tano sasa huwezi kung’ang’ania iwe sifuri tu kwa sababu tano huipendi!

Pongezi zangu:

Binafsi napenda kuipongeza Serikali kwa mwanzo huu wa kurudisha heshima ya taifa katika kusimamia na kulinda raslimali za taifa letu. Pongezi zinaenda mbele zaidi kwa timu zote ambazo zimethubutu kufanya mambo ambayo hayakudhaniwa kuwa yanawezekana kufanyika katika nchi yetu hii. Nina uhakika wakati ufike au utakapofika wajumbe wa tume ya majadiliano wajulikane wazi na kupewa heshima wanayostahili hasa kwa kuweza kusimama kidede na wakubwa hawa. Naogopa kudhania hata kwa mbali kama wapingaji wa yaliyotangazwa jana wangekuwa kwenye timu ya wajumbe taifa lingeambulia nini. Inawezekana wangebanwa na wazungu hawa wangekusanya mpira kwapani na kuondoka na kutuambia “tumeshindwa, wazungu wametubana sana”!

Kilichotangazwa jana ni jambo la kupongeza, siyo jambo la kuonea haya. Wengine wansema tulidai trilioni 400 na ushee na sasa tumepewa bilioni 700 tu kweli tushangilie? Ndugu zangu kuna msemo wa wahenga kuwa ndege mmoja mkononi ana thamani kubwa kuliko ndege tisa mtini! Na hata hayo madai yanaitwa madai kwa sababu hiyo; na imeelezwa vizuri jana kuwa hii si hatua ya mwisho. Sehemu kubwa ambayo inaonekana imebakia na labda itatuliwa muda si mrefu ujao ni suala la kodi. Kwa yeyote anayejua masuala ya kodi si mambo madogo. Serikali inaweza kudai lakini haina maana anayedaiwa hana haki ya kusema “hadaiwi chochote” au “hadaiwi kiasi chote hicho”. Baada ya Serikali kutoa madai yake tena wazi zile Barrick na Acacia walikuwa na haki ya msingi katika biashara kupinga (object) dhidi ya madai hayo na walikuwa na haki ya kutoa nyaraka mbalimbali ambazo zingepitiwa ili kuona ni madai gani ni ya kweli na yapi si ya kweli au yapi yanahitaji kupitia (adjusted). Lakini pia pande zote mbili zina haki ya kuangalia namna ya kutatua mgogoro wa kodi. Hata kwenye makampuni au wafanyabiashara wa kawaida si wana haki ya kuhoji (dispute) madai ya kodi na wakati mwingine madai yao yanabadilishwa au wanaweza wakatoa pendekezo (offer) la kulipa kiasi gani kwa mkupuo au kwa utaratibu fulani? Sasa kwanini tudhanie kuwa hilo haliwezekani? Yaani kwa vile tumesema tunadaia trilioni 400 basi ni lazima zilipwe zote na kiasi chochote chini ya hapo ni kuwa cha kupuuzia?

Hizi ni Zama Mpya

Ndugu zangu, hizi ni zama mpya; ni zama ambazo baadhi ya vitu vinaenda kubadilika na ni vizuri watu wakae kujua vinabadilika. Wajue pia kuwa zama hizi bado zinatafuta mahali pake pa kushikilia. Kweli zipo hoja mbalimbali zinazoweza kutolewa kukosoa serikali na kwa haki kabisa serikali inapaswa kukosolewa. Kuna maeneo ambayo yanastahili kukosolewa na watu wanapaswa kukosoa. Lakini ni lazima na muhimu kukosoa kufanyike siyo kwa sababu ya chuki, hasira au ubaya fulani.

Hitimisho

Tunasubiria kwa hamu kuona hatua zaidi zikiendelea kuchukuliwa si kwenye madini tu bali kwenye sekta nyingine ili kuhakikisha Watanzania wanafaidika kwa kiwango cha juu kabisa na utajiri wa mali zao za asili; kwani wao ndio wawekezaji wakubwa kwenye jambo lolote linaloenda kufanywa. Kwani hakuna mwekezaji mkubwa kuliko mwenye raslimali zake. Ni lazima tujitambue hivyo, na ni lazima tujitendee hivyo. Tusijione kama siyo ‘wawekezaji’ na hawa watu wanaokuja na fedha ndio ‘wawekezaji’. Sisi ndio wawekezaji wakubwa; Tanzania ndio mwekezaji mkubwa zaidi.

Sasa kwanini tujione duni na kutetemeka mbele ya wawekezaji wadogo hata kama ni wazungu?

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com

Wmuyabi joseph:

Kuna mambo umeyaandika hapa ambayo hayapo kwenye sheria yoyote, nq hayapo sawa. Yawezekana kuna mahali hukuelewa au hukusikia vizuri:

1) Hakuna mrabaha (royalty) wa 16%, iwe kwa sheria ya zamani au iliyopitishwa hivi karibuni. Sheria iliyopitishwa hivi karibuni mrabaha ni 6%.

2) Kuhusu ofisi, nadhani alimaanisha operations offices.

3) dola million 300 zitalipwa in good faith ina maana hakuna kosa lililothibituka kufanywa na Acacia. Siyo sahihi kusema ni malipo ya kuanzia.

3) Hilo la ujenzi wa barabara halipo. Lakini kama sehemu ya social responsibility, kampuni itaendelea kusaidia jamii zinazowazunguka

4) Hilo la kusema watahusika na dhahabu, copper na silver pekee yaliyobakia yatakuwa mali ya Tanzania, tunataka kujiridhisha kwa ambacho hakipo. Nimefanya kazi katika migodi hiyo, zaidi ya hayo madini hakuna mengine ambayo yapo katika economic concentrations. Sharti hilo Barrick wamekubali kwa sababu halina athari yoyote kwao

5) Kuajiri na kuwafundisha watanzania, tangu makampuni haya yaanze, imekuwa ndiyo sera inanyoyaongoza. Hayo yamekuwepo wakati wote, ndiyo maana sasa hivi kuna watanzania kwenye senior managent positions. Mimi nilianza kwenye makampuni haya nikiwa junior geologist, nikapanda mpaka kuwa country manager. Nikaenda kufanya nje, nikiwa project manager, na chini yangu kukiwa na expatriates 71. Kwa hiyo ni kitu ambacho kimekuwepo. Na watanzania wengi walio na uwezo na nidhamu, wamepanda, na wengi wapo nje ya Tanzania.

6) Kutolala kwenye premises za kampuni sioni kama ni kitu cha kumsaidia mfanyakazi. Hiyo inamsaidia mwajiri. Inampunguzia gharama za kumhudumia. Pale Buly Barrick walitaka sana wafanyakazi wote wakae nje ya mgodi, tulio wengi, hasa tuliokuwa kwenye senior positions tulikataa.

7) Kazi zote kufanywa na kampuni za kitanzania. Hilo limekuwepo wakati wote. Sera inayoongoza kwenye makampuni haya kufuatia sera ya madini 2010 ni kwamba kunapokuwa na kazi, priority ya kwanza ni kampuni zilizomo ndani ya wilaya, kama hakuna unatafuta kampuni iliyomo ndani ya mkoa, kama hakuna, kazi inakuwa open kwa kampuni yoyote iliyopo Tanzania, ikishindikana unatoka nje ya Tanzania.

Mengi yaliyotajwa kwa wasiofahamu wataona ni mapya, lakini yalikuwepo siku zote. Jipya ni hilo la kugawana faida 50/50. Nalo hilo siyo la kupigia vigelegele. Huko Mwadui tulikuwa na 50/50 lakini mpaka leo tumepata nini.

Wengi wasichofahamu, makampuni haya hayapati faida kubwa kutoka kwenye mauzo ya dhahabu bali wanapata faida kubwa kutrade shares. Production inalenga kuwapa confidence shareholders ili shares ziweze kupanda. Mathalani kabla ya Brexit hisa za Acacia zilikuwa na thamani kama ya dola 2.5 hivi. Baada ya Brexit zilipanda mpaka kufikia dola 5. Walioamua kuuza hisa zao walipata faida ya 100%. Wewe kama unasubiria faida ya 50/50 unaweza kusubiri mpaka uchoke. Serikali itamiliki 16%, je tutakuwa tunauza hisa na kununua?
 
Acacia kiasilimia wamepata hasara kubwa zaidi kuliko Barrick lakini kwa uwingi wa fedha Barrick wamepata hasara kubwa zaidi. Sikumbuki capitalization ya Barrick na Acacia kwenye stock markets. Lakini Barrick ina zaidi ya mara 10 ya Acacia. Ufahamu pia ndani ya Acacia Barrick wana karibu 64% ya umiliki. Kwa hiyo Barrick wanapata hasara mara mbili.
Nani muathirika sana wa huu mgogoro?na nini kitatokea endapo acacia atakataa mapendekezo yaliyofikiwa kati ya SERIKALI na barick?

posti fromu Nokia kitochi yuzingi jamii forum
 
Umeambiwa kutakuwa na maongezi zaidi kuhusiana na hiyo dola milioni 300 pamoja na kodi za miaka ya nyuma.

Huwezi kuwapangia kiasi cha kulipa. Wangeamua kulipa dola bilioni moja mngesema kwanini hawajaamua kulipa dola bilioni 50!!.

Hamna na hamjawahi kuwa na mioyo yenye shukrani, mnaona mna haki sana ya kupata mambo fulani kana kwamba hapa duniani mpo nyinyi tu. Thankless human beings.

I see. Kumbe sasa mambo yamegeuka na itategemea na maamuzi yao. Si kwamba tunawadai US$ 190 billion? Kwamba tumeacha kuwadai kwa kuwa tukiwadai tutakuwa tunawapangia na tutakuwa 'thankless human beings'? Kwamba mtu akikuibia na akakurudishia sehemu ndogo ya alichokuibia unapaswa kuwa na shukrani? Nimemsikiliza Kabudi na Magufuli na hakuna mahali wamesema kwamba mazungumzo yanayoendelea ni kuhusu malipo ya US$190 billion. Lugha sasa imebadilika na kuwa 'kuhusiana na kodi za nyuma'. Kumbuka US$ 300 million inalipwa in 'good faith' - kwamba we are still committed to resolving this matter amicably so as to protect our business. Haijathibitishwa kwamba Acacia walikwepa kodi au walidanganya kiasi cha madini walichouza (Labda kama unaamini ripoti ya Prof. Mruma ni final. Ila kwenye majadiliano haiwezi kuwa final maana Barick na Acacia wataipinga).

By the way, why should I have moyo wa shukrani? Tangu tumeambiwa madini yanachimbwa hapa nchini kwetu, hapa kijijini kwetu Kwa Mpiga Miti hatujaona mabadiliko yoyote. Hata wakilipa hayo mabilioni, we won't even feel it. Nina uhakika maisha yetu hapa Kijijini Mpiga Miti yatabaki vile vile. Wala hatutajua kama pesa zimelipwa tayari. Tuwe na shukrani kwa lipi? Wewe Kijijini kwenu hizo pesa zitafika? Na hata wakisema tumepata mafuta mengi kiasi gani, kwa uzoefu wa tulikotoka, nina uhakika watu wa Mpiga Miti hatutaona tofauti yoyote. We have absolutely nothing to celebrate about.
 
Wmuyabi joseph:

Kuna mambo umeyaandika hapa ambayo hayapo kwenye sheria yoyote, nq hayapo sawa. Yawezekana kuna mahali hukuelewa au hukusikia vizuri:

1) Hakuna mrabaha (royalty) wa 16%, iwe kwa sheria ya zamani au iliyopitishwa hivi karibuni. Sheria iliyopitishwa hivi karibuni mrabaha ni 6%.

2) Kuhusu ofisi, nadhani alimaanisha operations offices.

3) dola million 300 zitalipwa in good faith ina maana hakuna kosa lililothibituka kufanywa na Acacia. Siyo sahihi kusema ni malipo ya kuanzia.

3) Hilo la ujenzi wa barabara halipo. Lakini kama sehemu ya social responsibility, kampuni itaendelea kusaidia jamii zinazowazunguka

4) Hilo la kusema watahusika na dhahabu, copper na silver pekee yaliyobakia yatakuwa mali ya Tanzania, tunataka kujiridhisha kwa ambacho hakipo. Nimefanya kazi katika migodi hiyo, zaidi ya hayo madini hakuna mengine ambayo yapo katika economic concentrations. Sharti hilo Barrick wamekubali kwa sababu halina athari yoyote kwao

5) Kuajiri na kuwafundisha watanzania, tangu makampuni haya yaanze, imekuwa ndiyo sera inanyoyaongoza. Hayo yamekuwepo wakati wote, ndiyo maana sasa hivi kuna watanzania kwenye senior managent positions. Mimi nilianza kwenye makampuni haya nikiwa junior geologist, nikapanda mpaka kuwa country manager. Nikaenda kufanya nje, nikiwa project manager, na chini yangu kukiwa na expatriates 71. Kwa hiyo ni kitu ambacho kimekuwepo. Na watanzania wengi walio na uwezo na nidhamu, wamepanda, na wengi wapo nje ya Tanzania.

6) Kutolala kwenye premises za kampuni sioni kama ni kitu cha kumsaidia mfanyakazi. Hiyo inamsaidia mwajiri. Inampunguzia gharama za kumhudumia. Pale Buly Barrick walitaka sana wafanyakazi wote wakae nje ya mgodi, tulio wengi, hasa tuliokuwa kwenye senior positions tulikataa.

7) Kazi zote kufanywa na kampuni za kitanzania. Hilo limekuwepo wakati wote. Sera inayoongoza kwenye makampuni haya kufuatia sera ya madini 2010 ni kwamba kunapokuwa na kazi, priority ya kwanza ni kampuni zilizomo ndani ya wilaya, kama hakuna unatafuta kampuni iliyomo ndani ya mkoa, kama hakuna, kazi inakuwa open kwa kampuni yoyote iliyopo Tanzania, ikishindikana unatoka nje ya Tanzania.

Mengi yaliyotajwa kwa wasiofahamu wataona ni mapya, lakini yalikuwepo siku zote. Jipya ni hilo la kugawana faida 50/50. Nalo hilo siyo la kupigia vigelegele. Huko Mwadui tulikuwa na 50/50 lakini mpaka leo tumepata nini.

Wengi wasichofahamu, makampuni haya hayapati faida kubwa kutoka kwenye mauzo ya dhahabu bali wanapata faida kubwa kutrade shares. Production inalenga kuwapa confidence shareholders ili shares ziweze kupanda. Mathalani kabla ya Brexit hisa za Acacia zilikuwa na thamani kama ya dola 2.5 hivi. Baada ya Brexit zilipanda mpaka kufikia dola 5. Walioamua kuuza hisa zao walipata faida ya 100%. Wewe kama unasubiria faida ya 50/50 unaweza kusubiri mpaka uchoke. Serikali itamiliki 16%, je tutakuwa tunauza hisa na kununua?

Umeeleza vizuri. Na utaona kwa maelezo uliyotoa hapa, wanasiasa na serikali yetu inategemea zaidi ujinga wa Watanzania kutawala.
 
Nani muathirika sana wa huu mgogoro?na nini kitatokea endapo acacia atakataa mapendekezo yaliyofikiwa kati ya SERIKALI na barick?

posti fromu Nokia kitochi yuzingi jamii forum
Kama mgogoro hautapata suluhu, in long term, Tanzania tutapata hasara kubwa zaidi. Fikiria kuwa Acacia ndiyo mtumiaji mkubwa wa umeme kuliko makampuni yote. Acacia ndiye mtumiaji mkubwa wa cement kuliko wote. Acacia inaajiri wafanyakazi wengi kuliko kampuni yoyote. Acacia ndiyo mchangiaji mkubwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kuliko mwajiri yeyote. Dhahabu inaingiza 54% ya pesa yote ya kigeni.

Ifahamike kuwa tukiwaondoa Acacia hakuna kampuni nyingine ya madini itakayokuja kuwekeza Tanzania. Ni dhahiri kwa matokeo ya majadiliano, inaonekana kwa kadiri ya mikataba na sheria yetu ya madini, Acacia hawakutuibia wala hawakudanganya kiasi cha madini kwenye makinikia. Na kama ndiyo hivyo, ina maana tumetumia nguvu kuwanyanyasa. Na kama tukifunga migodi yao ina maana tutakuwa tumetumia nguvu kuchukua mali zao. Na ikiwa hivyo, ni nani atakayekuja katika nchi ambayo serikali ikitaka, inaweza kukunyang'anya mradi wako wakati wowote?

Nionavyo mimi, serikali itafanya kila jitihada kuhakikisha hatufiki huko. Kama Acacia watagoma kuridhia yaliyokubaliwa kati ya serikali na Barrick, italazimu serikali kuisikiliza Acacia hata kama itamaanisha kuondoa baadhi ya mambo iliyokubaliana na Barrick. Kwa mfano kwaajili ya kulinda heshima ya serikali, Acacia wanaweza kukubali yafanyike malipo ya dola milioni 300 ndani ya miaka 20, na malipo yatokane na uzalishaji wakati inajulikana kabisa katika kipindi cha miaka 20 chochote kinaweza kutokea na kuyafanya makubaliano hayo kutokuwa na maana tena. Kwenye 50/50 wanaweza kukubaliana itajumuisha na kodi za serikali.

Tufahamu pia mgodi wa Bulyanhulu mpaka wakati unajengwa ulikuwa ndio mgodi pekee wa underground katika kipindi cha miaka 10 ukitumia teknolojia ya kisasa kabisa. Ni kazi ngumu sana kuuendesha mgodi wa Bulyanhulu. Kosa dogo, ni maafa makubwa.

Baadhi ya watu wanawataja wachina, wasichojua ni kuwa wachina wapo chini sana katika teknolojia ya uchimbaji madini. Ndiyo maana kule kwao wamelazimika kuukubali uwekezaji wa Wamarekani, wakanada na Waustralia. Ni migodi ya hao wageni ndiyo inayoifanya China kuwa mzalishaji mkubwa wa dhahabu Duniani. Uwezo wa wachina kwenye utaalam wa uchimbaji madini unazidiwa kwa mbali na utaalam wa Watanzania kwenye sekta hii.

Siyo suala la hiari lakini tunalazimika kuhakikisha hawa wawekezaji hatuwaondoi japo tutajitutumua kwaajili ya kulinda hadhi ya serikali na nchi. Ni dhahiri serikali nayo imekwishachoka na huu mgogoro, ingependa sana uishe haraka lakini bila ya kupoteza credibility, hasa kwa wananchi walioaminishwa kuwa tunaibiwa sana kwenye madini, na kuwa kuna pesa nyingi kwenye madini inayoweza kutufanya sisi sote tukaishi kwa raha hata bila ya kufanya kaxì
 
I see. Kumbe sasa mambo yamegeuka na itategemea na maamuzi yao. Si kwamba tunawadai US$ 190 billion? Kwamba tumeacha kuwadai kwa kuwa tukiwadai tutakuwa tunawapangia na tutakuwa 'thankless human beings'? Kwamba mtu akikuibia na akakurudishia sehemu ndogo ya alichokuibia unapaswa kuwa na shukrani? Nimemsikiliza Kabudi na Magufuli na hakuna mahali wamesema kwamba mazungumzo yanayoendelea ni kuhusu malipo ya US$190 billion. Lugha sasa imebadilika na kuwa 'kuhusiana na kodi za nyuma'. Kumbuka US$ 300 million inalipwa in 'good faith' - kwamba we are still committed to resolving this matter amicably so as to protect our business. Haijathibitishwa kwamba Acacia walikwepa kodi au walidanganya kiasi cha madini walichouza (Labda kama unaamini ripoti ya Prof. Mruma ni final. Ila kwenye majadiliano haiwezi kuwa final maana Barick na Acacia wataipinga).

By the way, why should I have moyo wa shukrani? Tangu tumeambiwa madini yanachimbwa hapa nchini kwetu, hapa kijijini kwetu Kwa Mpiga Miti hatujaona mabadiliko yoyote. Hata wakilipa hayo mabilioni, we won't even feel it. Nina uhakika maisha yetu hapa Kijijini Mpiga Miti yatabaki vile vile. Wala hatutajua kama pesa zimelipwa tayari. Tuwe na shukrani kwa lipi? Wewe Kijijini kwenu hizo pesa zitafika? Na hata wakisema tumepata mafuta mengi kiasi gani, kwa uzoefu wa tulikotoka, nina uhakika watu wa Mpiga Miti hatutaona tofauti yoyote. We have absolutely nothing to celebrate about.
Mtanzania katika ubora wake. Nyinyi si ndio mliosema kwamba barrick hawawezi kupoteza muda wao na kuja bongo?.

Walipokuja mkasema hawawezi kukaa na serikali wakajadiliana jambo lolote lile?.

Sasa hivi mnashikia bango bilioni 190 wakati msingi mkuu wa maongezi ulikuwa ni kupitia sheria mpya za madini zilizopitishwa na bunge.

Mtu makini anaangalia sababu ya kwanini anaibiwa, udhaifu unaomfanya aibiwe na sio kuishia kutazama pesa tu.

Pesa sio msingi wa maendeleo, kama akili kichwani ni zero hata bilioni moja leo hii utaishia kufanya mambo ya kipuuzi na kubakia na ulofa wako.

Mnavyoongea kana kwamba Tanzania inayo migodi hiyo michache tu ambayo barrick na acacia wanachimba dhahabu.

Mnasahau kabisa, kwamba yapo madini ambayo bado hayajaguswa, na kwa sababu hiyo msingi wa sisi kufaidika umewekwa kupitia sheria mpya za madini, ambazo zimewekwa kwenye hali ambayo sisi tutafaidika na rasilimali tulizonazo.

Anachokifany mheshimiwa JPM hakiwezi kuthaminiwa na watu kama nyinyi, kwa sababu usaliti wenu sio wa kificho.

Ni watoto wa vizazi vijavyo ndio watakaokuja kufahamu kwa undani umuhimu wa michakato inayofanyika ndani ya awamu hii ya tano.
 
Mbona unakuwa kama watoto wa shule ya msingi? Mara nimekushinda. Mara ninyi mlisema. Mara mbona Barick wamekuja. Unhelpful. Hata Kabudi anapenda kweli kutumia ujio wa bosi wa Barick kama ushindi as if all we wanted ni huyo bosi kuja. Meaning, Kabudi na bosi wake are more into politics than anything else.

We all want the best for the country. Na Lissu aliposema tunaibiwa kwenye sheria, Mkuu wa Nchi alisema nini? Na Lissu sasa yuko wapi? Ni nini kilimtokea? Na wakati wa JK na Mkapa Lissu aliposema sheria zinazotungwa ni mbovu, wewe ulisema nini then? And why do you expect our praise now?

Nakubaliana na wewe. Hata tulipwe hizo Trilioni 450 tutabakia na ulofa wetu. Unafikiri hizo pesa zitafika kijijini kwetu kwa Mpiga Miti?
 
Back
Top Bottom