.
Ndiyo, hiyo pesa ni cha juu lakini usisahau kuwa watatatoa ajira ya kudumu (kodi itapatikana), wataleta maendeleo (barabara, nyumba, maji, shule, kiwanda cha kuchakachua). Hayo yote yataongeza kukuwa kwa uchumi, kwasababu kama sehemu ina miundombinu biashara itaongezeka na ajira itaongezea zaidi, wenyewe wanaita 'snowball effect'.
Utakuta ile 400Tsh yote itakuwa imelipwa baada ya muda fulani, sasa nyinyi mlikuwa mnataka kututishia nyau na kama tungewasikiliza, sio tuu tungekosa maendeleo bali tungezidi kuibiwa.
Kuna kitu kingine ambacho wengi mnakisahau na hiki ni ile nguvu ya ushawishi wa nchi, leo Tanzania imerudi kwenye mstari kama ilivyokuwa kipindi cha nyerere. Nchi inaonekana makini, siyo shamba la bibi kama zamani. Leo hii watu hawawezi kuja kutuchezea kama zamani, inabidi wajipange, wajiulize mara mbili mbili, wawekezaji wa maana watataka kuja kwa kuwa wanajua watanzania ni watu makini.