Behaviourist
JF-Expert Member
- Apr 8, 2016
- 39,902
- 95,407
Walikua na bombadier aina hyo ambazo tunazo tz tu?Ushamba mzigoAcha uongo,hiyo ni ile ndege ya pekee ambayo atcl walikuwa nayo kabla Serikali haijaanza kununua zingne.usiwe unaongea kitu bila kuchunguza
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa ndege mpya sio mwaka 1 bana tunaelewa kila kituNdege zina services schedule zake kila baada ya miaka kadhaa (ni vitu ambavyo avikwepeki) ndio maana unawasikia wakipiga kelele kufufua hangar la Arusha kupunguza hizo gharama za kupeleka ndege Canada.
Mama weee!!!!!!!! Njoo huku usikie hii, eti serikali imeanza kukarabati hanga (banda) la kutengenezea ndege kwa kuweka taa! Siyo jeki na supana.Ni ile ndege mpya iliyonunuliwa hivi karibuni na kupokelewa kifalmeView attachment 993742
14JAN 2019
Bombardier kukarabatiwa Canada kwa bilioni 13.9/-
SERIKALI imesema ndege mbili aina ya Bombardier Dash Q400 zilizonunuliwa mwaka 2016, zitapelekwa kufanyiwa ukarabati Canada mwezi ujao. Imesema ukarabati huo unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani milioni sita (Sh. bilioni 13.860).
WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO, ISACK KAMWELWE, PICHA MTANDAO
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa kozi ya wahudumu ndani ya ndege katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Ndege hizo zilinunuliwa na serikali zikiwa na uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja na zimekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wanaozitumia kwa safari za ndani ya nchi.
“Bombadier mbili tulizozinunua tunatarajia kuzipeleka nchini Canada kwa ajili ya kufanyiwa 'service', na ndege moja itagharimu Dola za Marekani milioni tatu,” alisema Waziri Kamwelwe.
Waziri huyo alisema kuwa, baada ya kuletewa taarifa hiyo, alilazimika kumfuata Rais John Magufuli na kumshauri serikali ianze kufanya ukarabati kwa hanga lililopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ili kupunguza gharama kubwa ambazo nchi inaingia katika kuzikarabati ndege.
Alisema katika kulitekeleza hilo, serikali imeshaanza kuchukua hatua kwa kuanza kukarabati hanga hilo kwa kuweka taa na kwamba serikali imeshaingia mikataba mitatu, mmojawapo utakuwa wa kununua vifaa vya matengenezo. Alisema Rais Magufuli ameshakubali kutoa pesa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vitakavyotumika katika hanga hilo.
“Kwa hiyo, ndugu zangu tutaanza kukarabati ndege sisi wenyewe, nimeamua kusimamia 'industry' inadumu na hakuna kurudi nyuma,” alisema Waziri Kamwelwe.
Kuhusu mafunzo ya uhudumu ndani ya ndege yaliyoanzishwa na NIT, Waziri Kamwelwe, alisema yatasaidia kupata Watanzania wakaohudumia ndege zilizonunuliwa na serikali.
Aliutaka uongozi wa NIT kuhakikisha mafunzo ya kozi hiyo yanakidhi viwango vya kimataifa. Mkuu wa NIT, Prof. Zacharia Mganilwa, alisema idadi ya wahandisi wa ndege nchini inaendelea kushuka, akibainisha kuwa mwaka 2012 kulikuwa na wahandisi 172, mwaka 2016 walikuwa 74, huku asilimia 69 kati yao, wakiwa ni raia wa kigeni.
Prof. Mganiliwa pia alisema zaidi ya asilimia 70 ya matengenezo ya ndege yanafanyika nje ya nchi. “Tulikuwa na upungufu wa marubani kwa asilimia 60, mwaka 2017, idadi yao ilikuwa 743 kati ya hao 317 walikuwa ni wazawa na 425 ni raia wa kigeni,” alisema Prof. Mganilwa.
Alisema idadi ya wahudumu wa ndege waliosajiliwa nchini imekuwa ikiongezeka tangu serikali ilipoanza kununua ndege. Alisema mwaka 2013/14, idadi yao ilikuwa 43, mwaka 2014/15 walikuwa 42, mwaka 2015/16 walikuwa 50, mwaka 2016/17 walikuwa 96, mwaka 2017/18 walikuwa 143 na mwaka 2019 waliopo katika mafunzo ni 61.
Alisema kuwa mwaka 2015, NIT ilianzisha shule kuu ya usafiri wa anga ikiwa na idara mbili ya uhandisi wa ndege na wahudumu wa ndege.
Alisema NIT ilipewa ithibati ya kutoa mafunzo ya uhudumu ndani ya ndege Aprili 25, mwaka jana na ithibati ya utengenezaji wa ndege na urubani bado hawajapewa. Alisema kuwa kwa sasa wapo katika hatua ya nne ya kukamilisha matakwa ya kupewa ithibati hiyo.
Naomba, kwa niaba ya wazalendo wenzangu wa Isansa Mbozi nitoe ufafanuzi kuhusu na kilichoandikwa na gazeti la *NIPASHE* la leo tarehe 14 January 2019, kwenye kichwa cha habari _"Bil 13.9 kukarabati Bombadier Canada"_
Ni kwamba tarehe 10 mwezi huu, mh waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano *Mhandidi Isack Kamwele* , alialikwa kama mgeni rasmi katika chuo cha usafirishaji( NIT) katika uzinduzi wa kozi ya wahudumu ndani ya ndege
Katika hotuba yake, alieleza changamoto katika sekta hii ya usafiri wa anga hapa nchini, mojawapo ya changamoto aliosema, ni ukosefu wa karakana( Hanga) za kukarabati ndege zenye ubora na ukubwa wa kutosha hapa nchini
Hivyo akasema kwa mfano mwakani wanapaswa kupeleka ndege zetu 2 za bombadier kwa ajili ya kuzifanyia service( Schedule service), kwa kawaida kila ndege ina muda wake maalumu wa kufanyiwa service kutokana na flying hours, ambapo kwa bombadier Q 400 hufanyiwa service kila baada ya masaa( Flying hours) 600 ya kuwa angani
Na akasema, kama watapeleka ndege hizo nchini Canada kwa ajili ya service itawagharimu serikali takribani $ 3m kwa ndege moja na $ 6m kwa ndege zote mbili
Lakini akasema, baada ya kuambiwa hilo, alimfuata mh Rais na kumuomba apewe fedha kwa ajili ya ukarabati wa hanga yetu, iliyopo katika uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro( KIA) ambapo kimsingi ombi lake lilikubaliwa na mh Rais, na serikali wameshaanza ukarabati mkubwa katika hanga hiyo na pia wameshaingia mikataba 3, ikiwemo ya kununua vifaa vya kisasa kwa ajili ya ukarabati wa ndege zetu
Na yote hii, inafanyika ili tuweze kuokoa fedha nyingi za kupeleka ndege Canada kwa ajili ya service
Binafsi kama mzalendo nitoe wito, hasa kwa vyombo vya hsbari kama magazeti, kujiepusha kuwa na vichwa vya habari vyenye kuweza kupotosha umma,
Nadhani kwa hili la NIPASHE, nina imani mamlaka husika zitachukua hatua stahiki juu ya jambo hilo
Mzalendo
_Ngamanya Kitangalala_
kilamtu na taaluma yake hilo gazeti lipo sawa kwa 100% na limefuata taratibu zote za uandishi pia kanunu ni kipi kilichokosewaaa? huo ndio uandishi wa magazeti lazima mwandishi mashuhuri ajue kuliremba kwa kichwa maridhawa ka hicho ulichokisomaNaomba, kwa niaba ya wazalendo wenzangu wa Isansa Mbozi nitoe ufafanuzi kuhusu na kilichoandikwa na gazeti la *NIPASHE* la leo tarehe 14 January 2019, kwenye kichwa cha habari _"Bil 13.9 kukarabati Bombadier Canada"_
Ni kwamba tarehe 10 mwezi huu, mh waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano *Mhandidi Isack Kamwele* , alialikwa kama mgeni rasmi katika chuo cha usafirishaji( NIT) katika uzinduzi wa kozi ya wahudumu ndani ya ndege
Katika hotuba yake, alieleza changamoto katika sekta hii ya usafiri wa anga hapa nchini, mojawapo ya changamoto aliosema, ni ukosefu wa karakana( Hanga) za kukarabati ndege zenye ubora na ukubwa wa kutosha hapa nchini
Hivyo akasema kwa mfano mwakani wanapaswa kupeleka ndege zetu 2 za bombadier kwa ajili ya kuzifanyia service( Schedule service), kwa kawaida kila ndege ina muda wake maalumu wa kufanyiwa service kutokana na flying hours, ambapo kwa bombadier Q 400 hufanyiwa service kila baada ya masaa( Flying hours) 600 ya kuwa angani
Na akasema, kama watapeleka ndege hizo nchini Canada kwa ajili ya service itawagharimu serikali takribani $ 3m kwa ndege moja na $ 6m kwa ndege zote mbili
Lakini akasema, baada ya kuambiwa hilo, alimfuata mh Rais na kumuomba apewe fedha kwa ajili ya ukarabati wa hanga yetu, iliyopo katika uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro( KIA) ambapo kimsingi ombi lake lilikubaliwa na mh Rais, na serikali wameshaanza ukarabati mkubwa katika hanga hiyo na pia wameshaingia mikataba 3, ikiwemo ya kununua vifaa vya kisasa kwa ajili ya ukarabati wa ndege zetu
Na yote hii, inafanyika ili tuweze kuokoa fedha nyingi za kupeleka ndege Canada kwa ajili ya service
Binafsi kama mzalendo nitoe wito, hasa kwa vyombo vya hsbari kama magazeti, kujiepusha kuwa na vichwa vya habari vyenye kuweza kupotosha umma,
Nadhani kwa hili la NIPASHE, nina imani mamlaka husika zitachukua hatua stahiki juu ya jambo hilo
Mzalendo
_Ngamanya Kitangalala_
Je, tunao 'Aircraft Engineers & Techicians' wa kutosha na wenye weledi kufanya "service & repair' ya hizo ndege pamoja na workshops?
Bro cha ajabu hapa nini? Unadhani ndege ni Vitz? Hiyo ni service ya kawaida na wala hakuna cha ajabu. Kama unapanda basi kwenda Moshi unalipa sh 30 elfu mwingine anakwenda Moshi huko huko analipa laki 3 hujawahi kujiuliza why? Nipashe wameandika kwa maana nyingine ya kawaida tu, lakini wewe unataka kuonyesha kama ni kitu cha ajabu saana. Acheni umbeya kwa mbo msiyoyaelewa.
Sent using Jamii Forums mobile app
hujui kitu, kaa kimya!Wacha urongo!
hela za matumizi ya serikali hazipitishwi na Rais!
Tunataka kujua hii ni service ya kawaida ama ni ukarabati wa ubovu?
Kama ndege ni mbovu hizi ni terrible teens zimeanza ku rear their ugly face on him?
Kama ni ukarabati wa kawaida kwa nini hela inaenda kuombwa nje ya ATCL, haikuwa kwenye business plan?
Na ni kwa nini Waziri Kamwele ndio ana run ATCL badala ya a professionally qualified, full time dedicated, paid and accountable CEO of the company?
TUNATAKA MAJIBU!
Acha uzembe. Kwanini hawakukarabati hilo hanger kabla ya kukimbilia kuleta hiyo mindege? Ungekuwa mzalendo kweli ungetambua kuwa hizo hela ambazo Waziri kaomba kwa Rais ni zako wewe mlipakodi hohehaheNaomba, kwa niaba ya wazalendo wenzangu wa Isansa Mbozi nitoe ufafanuzi kuhusu na kilichoandikwa na gazeti la *NIPASHE* la leo tarehe 14 January 2019, kwenye kichwa cha habari _"Bil 13.9 kukarabati Bombadier Canada"_
Ni kwamba tarehe 10 mwezi huu, mh waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano *Mhandidi Isack Kamwele* , alialikwa kama mgeni rasmi katika chuo cha usafirishaji( NIT) katika uzinduzi wa kozi ya wahudumu ndani ya ndege
Katika hotuba yake, alieleza changamoto katika sekta hii ya usafiri wa anga hapa nchini, mojawapo ya changamoto aliosema, ni ukosefu wa karakana( Hanga) za kukarabati ndege zenye ubora na ukubwa wa kutosha hapa nchini
Hivyo akasema kwa mfano mwakani wanapaswa kupeleka ndege zetu 2 za bombadier kwa ajili ya kuzifanyia service( Schedule service), kwa kawaida kila ndege ina muda wake maalumu wa kufanyiwa service kutokana na flying hours, ambapo kwa bombadier Q 400 hufanyiwa service kila baada ya masaa( Flying hours) 600 ya kuwa angani
Na akasema, kama watapeleka ndege hizo nchini Canada kwa ajili ya service itawagharimu serikali takribani $ 3m kwa ndege moja na $ 6m kwa ndege zote mbili
Lakini akasema, baada ya kuambiwa hilo, alimfuata mh Rais na kumuomba apewe fedha kwa ajili ya ukarabati wa hanga yetu, iliyopo katika uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro( KIA) ambapo kimsingi ombi lake lilikubaliwa na mh Rais, na serikali wameshaanza ukarabati mkubwa katika hanga hiyo na pia wameshaingia mikataba 3, ikiwemo ya kununua vifaa vya kisasa kwa ajili ya ukarabati wa ndege zetu
Na yote hii, inafanyika ili tuweze kuokoa fedha nyingi za kupeleka ndege Canada kwa ajili ya service
Binafsi kama mzalendo nitoe wito, hasa kwa vyombo vya hsbari kama magazeti, kujiepusha kuwa na vichwa vya habari vyenye kuweza kupotosha umma,
Nadhani kwa hili la NIPASHE, nina imani mamlaka husika zitachukua hatua stahiki juu ya jambo hilo
Mzalendo
_Ngamanya Kitangalala_
Ni kawaida lakini kwa bavicha kurukia mada bila uelewa wa kina.