Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,181
- 166,176
Kama ndivyo Hicho kilicho bakia, sio mbaya [emoji106] lazima ng'ombe umpe nyasi kwa wingi ili upate maziwa mengi [emoji4]Maana yake kati ya ile faida ya bilioni 23
Bilioni 13 zarudi Canada........
Faida inapungua hadi 10
Sent using Jamii Forums mobile app
Swali fikirishi je kununua ndege aina hizo mpya ni bei gani kwa wale wenye kujua watujuze ''A Country is Not a Company''Ni ile ndege mpya iliyonunuliwa hivi karibuni na kupokelewa kifalmeView attachment 993742
14JAN 2019
Bombardier kukarabatiwa Canada kwa bilioni 13.9/-
SERIKALI imesema ndege mbili aina ya Bombardier Dash Q400 zilizonunuliwa mwaka 2016, zitapelekwa kufanyiwa ukarabati Canada mwezi ujao. Imesema ukarabati huo unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani milioni sita (Sh. bilioni 13.860).
WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO, ISACK KAMWELWE, PICHA MTANDAO
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa kozi ya wahudumu ndani ya ndege katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Ndege hizo zilinunuliwa na serikali zikiwa na uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja na zimekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wanaozitumia kwa safari za ndani ya nchi.
“Bombadier mbili tulizozinunua tunatarajia kuzipeleka nchini Canada kwa ajili ya kufanyiwa 'service', na ndege moja itagharimu Dola za Marekani milioni tatu,” alisema Waziri Kamwelwe.
Waziri huyo alisema kuwa, baada ya kuletewa taarifa hiyo, alilazimika kumfuata Rais John Magufuli na kumshauri serikali ianze kufanya ukarabati kwa hanga lililopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ili kupunguza gharama kubwa ambazo nchi inaingia katika kuzikarabati ndege.
Alisema katika kulitekeleza hilo, serikali imeshaanza kuchukua hatua kwa kuanza kukarabati hanga hilo kwa kuweka taa na kwamba serikali imeshaingia mikataba mitatu, mmojawapo utakuwa wa kununua vifaa vya matengenezo. Alisema Rais Magufuli ameshakubali kutoa pesa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vitakavyotumika katika hanga hilo.
“Kwa hiyo, ndugu zangu tutaanza kukarabati ndege sisi wenyewe, nimeamua kusimamia 'industry' inadumu na hakuna kurudi nyuma,” alisema Waziri Kamwelwe.
Kuhusu mafunzo ya uhudumu ndani ya ndege yaliyoanzishwa na NIT, Waziri Kamwelwe, alisema yatasaidia kupata Watanzania wakaohudumia ndege zilizonunuliwa na serikali.
Aliutaka uongozi wa NIT kuhakikisha mafunzo ya kozi hiyo yanakidhi viwango vya kimataifa. Mkuu wa NIT, Prof. Zacharia Mganilwa, alisema idadi ya wahandisi wa ndege nchini inaendelea kushuka, akibainisha kuwa mwaka 2012 kulikuwa na wahandisi 172, mwaka 2016 walikuwa 74, huku asilimia 69 kati yao, wakiwa ni raia wa kigeni.
Prof. Mganiliwa pia alisema zaidi ya asilimia 70 ya matengenezo ya ndege yanafanyika nje ya nchi. “Tulikuwa na upungufu wa marubani kwa asilimia 60, mwaka 2017, idadi yao ilikuwa 743 kati ya hao 317 walikuwa ni wazawa na 425 ni raia wa kigeni,” alisema Prof. Mganilwa.
Alisema idadi ya wahudumu wa ndege waliosajiliwa nchini imekuwa ikiongezeka tangu serikali ilipoanza kununua ndege. Alisema mwaka 2013/14, idadi yao ilikuwa 43, mwaka 2014/15 walikuwa 42, mwaka 2015/16 walikuwa 50, mwaka 2016/17 walikuwa 96, mwaka 2017/18 walikuwa 143 na mwaka 2019 waliopo katika mafunzo ni 61.
Alisema kuwa mwaka 2015, NIT ilianzisha shule kuu ya usafiri wa anga ikiwa na idara mbili ya uhandisi wa ndege na wahudumu wa ndege.
Alisema NIT ilipewa ithibati ya kutoa mafunzo ya uhudumu ndani ya ndege Aprili 25, mwaka jana na ithibati ya utengenezaji wa ndege na urubani bado hawajapewa. Alisema kuwa kwa sasa wapo katika hatua ya nne ya kukamilisha matakwa ya kupewa ithibati hiyo.
Ni ndoto kwa ATC kukua na kuendelea kibiashara hata kama wangemiliki ndege kibao kama Ethiopia airline kwani kuna wajanja wengi ambao bado wanapanga njama za kupiga pesa kisayansi zaidi.
Hasa ndivyo ilivyo. Hata gari ukinunua jipya kabisa unaambiwa ulipeleke service kila mwaka au hata kabla ya mwaka kuisha kama litakuwa limetembea kilomita kadhaa.Ndege zina services schedule zake kila baada ya miaka kadhaa (ni vitu ambavyo avikwepeki) ndio maana unawasikia wakipiga kelele kufufua hangar la Arusha kupunguza hizo gharama za kupeleka ndege Canada.
Ukipata jibu nitagSwali fikirishi je kununua ndege aina hizo mpya ni bei gani kwa wale wenye kujua watujuze ''A Country is Not a Company''
kwa misukule ya Lumumba na yule spika dhaifu hili ni vigumu sana walielewe!Kukarabati ndege ni jambo la kawaida. Ila hapa ndipo tutapojifunza kuwa biashara ya ndege ni zaidi ya kununua tu ndege lukuki.
Na ndiyo maana mashirika mengi huwa hata ndege zao ni za kukodisha, eg south africa airways. Kazi ya kampuni ya ndege inatakiwa iwe ku-manage routes zenye faida na kuhakikisha ndege zinakuwa angani zikiwa zimejaa abiria kila wakati. Najua wengi hamtaelewa mpaka muone.
Tulisema sana lkn wakatokwa na mapovu kusimamia usanii wao sasa wameumbuka
Sent using Jamii Forums mobile app
Pengine ni borazaidi unejibidisha kuelewa manufacturer's technical recommendation kuhusiana na model Q400 Next G badala ya kutanguliza hitimisho la hisia zako binafsi.Hizo Bombardier tangu zimeanza rasmi kufanya safari, ni muda gani umepita? Na hiyo scheduled service huwa ni kila baada ya muda gani? Dreamliner je itagharimu kiasi gani?
Cc barafu
Kenya na Ethiopia wapo jirani ni kwa nini wasipeleke hapo? Tatizo la ATC ni wajanja wachache kujinufaisha kupitia visingizio kama hivyo
Hiyo faida itoke wapi mkuu?Jiwe ni msanii tu yule!!Maana yake kati ya ile faida ya bilioni 23
Bilioni 13 zarudi Canada........
Faida inapungua hadi 10
Sent using Jamii Forums mobile app
Mayooooooo wane !weka maelezo, hizi za juzi tu zimeshaharibka? Makopo haya yalikuwa mitumba kama ni hivyo!
Miaka kadhaa iliyopita wakati najiunga na jf niliona ni jukwaa la wasomi kweli kweli
Lakini kadiri siku zinavyokwenda naona kabisa jukwaa limevamiwa na facebook
(Vilaza)
Ndege sio basi la kwenda Tarime
Ndio maana fast jet wamepigwa pin
Ukiendesha biashara ya ndege unatakiwa uwe mchalo kweli kweli
Ndege inakwenda na kilomita zikifika kilomita kadhaa utake ,usitake hata kama magurudumu yake bado yako bomba kama ya basi la abood la kwenda moro to dar unatakiwa utowe na uweke mengine alikadharika na vifaa vingine ni mtindo wa kutoa na kuweka vipya kabisa
Service ya ndege hakuna kuweka kifaa used kama bus ni mtindo ule ule wa bandika bandua hata kama ni kizima kinachotazamwa ni kilomita zake za service kutimia ..
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwi! Kwi! Kwi!Baada ya mafanikio makubwa kwenye Uchumi wa Viwanda..
Sasa tupo kwenye Uchumi wa Ndege..
Ni kununua Ndege nyingi kadiri iwezekanavyo..
Ndege zinalipa sana.
Hili ni lile Pangaboi ambalo Zitto alitahadharisha kwamba limenunuliwa likiwa used. Jiwe ni mpigaji wa kuogopwa.