SGR wajenzi wa Ureno wamepotelea wapi?

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
2,239
2,000
Jamani tulizoea kuona wa portugese kambi yao ngerengere wakijenga reli sasa hivi hata mmoja haonekani mbona hatuambiwi wamepotelea wapi?mwenye taarifa anaweza kutuelewesha?
Binafsi mfatiliaji mzuri sana wa huu mradi wa SGR lakini nilisikia tu kuwa Yapi Merkezi na Motor Engine ya Ureno ndiyo wanajenga lakini sijawahi kuwaona Motor Engine tangia mradi uanze wala kuona gari lao au kifaa chochote kile naona Yapi Markezi ya Uturuki tu na nafikiri wao ndiyo wamechukua sehemu kubwa ya ujenzi na hata phase 2 ni Yapi Merkezi pekee watajenga labda tu Motor engine wao wanadili na issue nyingine.
 
PseudoDar186

Member
Mar 18, 2017
77
150
Wareno waliuacha mradi muda mrefu sana. Ila ipo chini ya mkeka. Kwa sasa wanaopiga mzigo ni waturuki peke yao. Inasemekana wareno hawakulipwa stahiki zao kama walivyokubaliana - wakafungasha kila kitu na kuondoka nchini.

Yapi Merkezi wanaweza kuwa wamepata guarantee kutoka kwa serikali yao (Uturuki) kwamba wasipolipwa na serikali yetu basi serikali yao itawalipa na kutudai sisi. Sidhani kama wareno walipata uhakika huo.
 
bababikko

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
2,390

asante kwa taarifa hizo zilizofichwa na jiwe
 
Midevu

Senior Member
Feb 11, 2012
157
500
Wareno waliuacha mradi muda mrefu sana. Ila ipo chini ya mkeka. Kwa sasa wanaopiga mzigo ni waturuki peke yao. Inasemekana wareno hawakulipwa stahiki zao kama walivyokubaliana - wakafungasha kila kitu na kuondoka nchini.

Yapi Merkezi wanaweza kuwa wamepata guarantee kutoka kwa serikali yao (Uturuki) kwamba wasipolipwa na serikali yetu basi serikali yao itawalipa na kutudai sisi. Sidhani kama wareno walipata uhakika huo.
Kama ni kweli basi hali ni mbaya zaidi ya tunavyofikiri.
Pia inawezekana mleta hoja anafahamu tayari nini kinaendelea ila anatupima tu.
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
6,925
2,000
sasa mabasi yetu tutapeleka wapi?
malori yetu ya mizigo itakuwaje?
Magu hafwai kabsaaa :D
Usidanganywe na mtu. Malori hayaendi popote; na yataendelea tu kupiga mzigo kama kawa.

Naomba tusibishane juu ya hili. Natoa ushahidi wa SGR ya jirani zetu Kaskazini na SGR yao ya mChina. Malori yapo na yanaendelea, licha ya kuwekewa mizengwe wanyimwe mizigo!

Sasa hivi unaambiwa kusafirisha kontena toka bandarini hadi Nairobi la futi 20 ni Ksh 142,,000/; na lile la futi 40 ni Ksh 212000/ , na bado kontena hilo hujalifikisha nyumbani au kiwandani maanake inabidi ukachukue mzigo wako kituoni.

Kusafirisha mizigo hiyo kwa lori gharama zake ni Ksh.65,000/ kwa kontena la futi 20; na Ksh.85000/ kwa lile la futi 40, na tena linafikishwa hadi nyumbani au kiwandani kwako.

Hebu niambie kama wewe ni mfanya biashara, utaachaje kwenda na lori.

Serikali ikiacha pawepo na ushindani wa kibiashara huru bila ya mizengwe ya kulazimisha baadhi ya mizigo isafirishwe kwa reli ili deni la ujenzi liweze kulipwa, reli hiyo ingekuwa ni mzigo kama ile aliyojenga Mwingereza.

Sasa sijui hapa kwetu tofauti yake itakuwaje! Lakini nina hakika malori hayatapotea barabarani; maana hata kule kwa mabeberu, kwa waChina, kwa waJapan hatuoni malori yakipotea barabarani.

Themagufulianz, imenibidi nikujibu kwa kirefu hivi, kwa sababu naona ushabiki wa kushangilia kila kitu umepungua. Tujaribu kupima mambo kwa uhalisi wake, na sio kwa misingi ya kushabikia tu!.

Tuendelee kujenga taifa letu kwa utulivu.
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
6,925
2,000
Wareno waliuacha mradi muda mrefu sana. Ila ipo chini ya mkeka. Kwa sasa wanaopiga mzigo ni waturuki peke yao. Inasemekana wareno hawakulipwa stahiki zao kama walivyokubaliana - wakafungasha kila kitu na kuondoka nchini.

Yapi Merkezi wanaweza kuwa wamepata guarantee kutoka kwa serikali yao (Uturuki) kwamba wasipolipwa na serikali yetu basi serikali yao itawalipa na kutudai sisi. Sidhani kama wareno walipata uhakika huo.
Na hakuna mwandishi wa habari yeyote anayeweza thubutu kufuatilia habari kama hii, labda awe hajipendi! Eeeh, yaani huko ndiko tulikofikia sasa. Kila jambo ni siri.
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,795
2,000
Usidanganywe na mtu. Malori hayaendi popote; na yataendelea tu kupiga mzigo kama kawa.

Naomba tusibishane juu ya hili. Natoa ushahidi wa SGR ya jirani zetu Kaskazini na SGR yao ya mChina. Malori yapo na yanaendelea, licha ya kuwekewa mizengwe wanyimwe mizigo!

Sasa hivi unaambiwa kusafirisha kontena toka bandarini hadi Nairobi la futi 20 ni Ksh 142,,000/; na lile la futi 40 ni Ksh 142000/ , na bado kontena hilo hujalifikisha nyumbani au kiwandani maanake inabidi ukachukue mzigo wako kituoni.

Kusafirisha mizigo hiyo kwa lori gharama zake ni Ksh.65,000/ kwa kontena la futi 20; na Ksh.85000/ kwa lile la futi 40, na tena linafikishwa hadi nyumbani au kiwandani kwako.

Hebu niambie kama wewe ni mfanya biashara, utaachaje kwenda na lori.

Serikali ikiacha pawepo na ushindani wa kibiashara huru bila ya mizengwe ya kulazimisha baadhi ya mizigo isafirishwe kwa reli ili deni la ujenzi liweze kulipwa, reli hiyo ingekuwa ni mzigo kama ile aliyojenga Mwingereza.

Sasa sijui hapa kwetu tofauti yake itakuwaje! Lakini nina hakika malori hayatapotea barabarani; maana hata kule kwa mabeberu, kwa waChina, kwa waJapan hatuoni malori yakipotea barabarani.

Themagufulianz, imenibidi nikujibu kwa kirefu hivi, kwa sababu naona ushabiki wa kushangilia kila kitu umepungua. Tujaribu kupima mambo kwa uhalisi wake, na sio kwa misingi ya kushabikia tu!.

Tuendelee kujenga taifa letu kwa utulivu.
Mkuu Kalamu1, Asante kwa hii. hapa umesema jambo moja la maana sana kuhusu ujio wa SGR na hatma ya malori.

Kenya walipoanza, ili deni la SGR lilipike, Kenya waliyapakia kwenye SGR kwa lazima all containers bound to Nairobi, makosa yakawa mengi kujikuta kuna containers za Mombasa zinapelekwa Nairobi, na bado SGR haishibi.

Kwa Tanzania, SGR ni Central Corridor tuu, wakati the busiest route ni Southern Corridor, hivyo hata SGR ikianza, bado wenye malori watabeba mizigo ya Tunduma.

Na ili SGR ilipe, inahitaji mzigo wa kushiba haswa, hivyo ikianza ni lazima kulazimisha containers zote za Morogoro Rd, zipelekwe kwa SGR hadi Moro Dry Port na safari sasa zitaanzia Moro. Ikifika Dodoma, vivyo hivyo.

Maadam jirani zetu wametangulia, na SGR yao imeanza kuwa a white elephant, hakuna ubaya kujifunza kwa wenzetu, ili sisi yasitukute yaliyowakuta wenzetu hawa.

Reli ya SGR: Je, Tujifunze kwa wenzetu Kenya kuepusha SGR yetu kuwa ‘A White Elephant’? Wenzetu yameshawakuta... - JamiiForums

P.
 
Lamsheku

JF-Expert Member
Jan 14, 2019
207
500
Wareno waliuacha mradi muda mrefu sana. Ila ipo chini ya mkeka. Kwa sasa wanaopiga mzigo ni waturuki peke yao. Inasemekana wareno hawakulipwa stahiki zao kama walivyokubaliana - wakafungasha kila kitu na kuondoka nchini.

Yapi Merkezi wanaweza kuwa wamepata guarantee kutoka kwa serikali yao (Uturuki) kwamba wasipolipwa na serikali yetu basi serikali yao itawalipa na kutudai sisi. Sidhani kama wareno walipata uhakika huo.
Nipe tofauti kati ya ureno na uturuki. Mbona kama umechanganya madesa.

Ureno=Portugal (uturuki).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom