Serikali yawaonya mashabiki wa Simba na Yanga kupokea Wageni

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Damas Ndumbaro amesema Serikali itakutana na Shirikisho la Soka nchini na klabu za Simba na Yanga ili kuona inatoa mchango gani kuhakikisha timu hizo zinafanya vizuri robo fainali na kusonga mbele.

Waziri Ndumbaro amesema pamoja na mambo mengine, amewataka mashabiki kuacha kuwapokea mashabiki na wafahamu mechi hizi za robo fainali ni kufa na kupona na kinachotakiwa ni kuhakikisha timu zetu zinashinda.

Amesema Serikali itakula sahani moja na mashabiki wa Simba na Yanga ambao wataenda kupokea wageni uwanja wa ndege na kuwasapoti.

"Wiki iliyopita tulitoa tamko, Serikali tunataka kukaa na Simba, Yanga na TFF, ili watuambie kama serikali, tunahitaji kutoa mchango gani ili timu kushinda robo fainali na ziingie nusu fainali. Tunaweza kukutana Jumanne wiki ijayo ili kupanga mikakati."

Kuhusu mashabiki amesema; "Watanzania niwaombe sana najua kuna utani wa jadi, lakini kwenye mechi hizi za robo fainali ni mechi za kufa na kupona, hatutegemei kuona Mtanzania yeyote akienda kupokea wageni uwanja wa ndege, ama kuvaa jezi za timu za wageni."

"Sisi kama Serikali hatutawaachia hili TFF wala Simba na Yanga, kwa hiyo tukihangaika na mtu ambaye tutaona ni msaliti. Tunaomba Watanzania watuelewe na watusamehe kwa sababu tunataka timu hizi zifanikiwe."

"Kwa hiyo wewe Mtanzania ambaye utaweka kimbelembele kwenda kupokea wageni uwanjani wa ndege, kuwasapoti kwa namna yeyote, hatutakuelewa na tutadili na wewe kwa vile ambavyo tunaona inafaa."

"Tumekuwa nchi pekee iliyofanikiwa kuingiza timu mbili mwaka huu, lakini ukishapata mafanikio haupaswi kutumia muda mwingi sana kushangilia hayo mafanikio, unatakiwa uangalie unafanya nini ili kuendelea kupata mafanikio zaidi." Amesema.
Kwa hiyo tunaanza kupangiwa namna ya kushangilia mpira? Mpira ni burdani, kila mtu anajua namna ya kuburudika nao. Haya yalianza, tutaua fan base ya mpira iliyopo nchini hivi hivi.
 
Kama ndiyo hivyo bora azifutilie mbali hizo clabu za Simba na Yanga tu ieleweke moja,
Yaan serikal inatutesa kwenye bei za bidhaa bado imeona watu wanafurahi kwenye mambo ya soka na utani wa jadi imeona iweke uzibe wa kumchagulia shabiki nini afanye kwa furaha yake binafsi,
 
Washabiki wa Simba muwe makini.
Yanga hawana uvumilivu kama Simba.
Yanga wanafanyaga kila kitu kuwasapoti washindani wa Simba Kimataifa ili kuwasaidia waifunge Simba.
Juzi Jwaneng walipokelewa na wao.

Wanasimba mkivaa jezi za Sundawn uwanjani halafu Yanga ikafungwa mtaweza kufanyiwa Fujo na washabiki wa Yanga.

Fujo za kuweza kudhuru afya zenu.
Take Care.
 
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Damas Ndumbaro amesema Serikali itakutana na Shirikisho la Soka nchini na klabu za Simba na Yanga ili kuona inatoa mchango gani kuhakikisha timu hizo zinafanya vizuri robo fainali na kusonga mbele.

Waziri Ndumbaro amesema pamoja na mambo mengine, amewataka mashabiki kuacha kuwapokea mashabiki na wafahamu mechi hizi za robo fainali ni kufa na kupona na kinachotakiwa ni kuhakikisha timu zetu zinashinda.

Amesema Serikali itakula sahani moja na mashabiki wa Simba na Yanga ambao wataenda kupokea wageni uwanja wa ndege na kuwasapoti.

"Wiki iliyopita tulitoa tamko, Serikali tunataka kukaa na Simba, Yanga na TFF, ili watuambie kama serikali, tunahitaji kutoa mchango gani ili timu kushinda robo fainali na ziingie nusu fainali. Tunaweza kukutana Jumanne wiki ijayo ili kupanga mikakati."

Kuhusu mashabiki amesema; "Watanzania niwaombe sana najua kuna utani wa jadi, lakini kwenye mechi hizi za robo fainali ni mechi za kufa na kupona, hatutegemei kuona Mtanzania yeyote akienda kupokea wageni uwanja wa ndege, ama kuvaa jezi za timu za wageni."

"Sisi kama Serikali hatutawaachia hili TFF wala Simba na Yanga, kwa hiyo tukihangaika na mtu ambaye tutaona ni msaliti. Tunaomba Watanzania watuelewe na watusamehe kwa sababu tunataka timu hizi zifanikiwe."

"Kwa hiyo wewe Mtanzania ambaye utaweka kimbelembele kwenda kupokea wageni uwanjani wa ndege, kuwasapoti kwa namna yeyote, hatutakuelewa na tutadili na wewe kwa vile ambavyo tunaona inafaa."

"Tumekuwa nchi pekee iliyofanikiwa kuingiza timu mbili mwaka huu, lakini ukishapata mafanikio haupaswi kutumia muda mwingi sana kushangilia hayo mafanikio, unatakiwa uangalie unafanya nini ili kuendelea kupata mafanikio zaidi." Amesema.
Hii si mara ya kwanza timu zetu kufika robo fainali

Na sijawahi kusikia haya matamko

Lakini sisemi tu if haya matamko yanatoka kuibeba yanga
 
Kisasi ni haki. Tunawapokea Mamelodi Sundowns kwa kishindo. Wakati ule MANARA, Hersi na Senzo waliungana na Kaizer Chiefs na Serikali ilikaa kimya. Hakuna kulialia Sisi ni Afrika. Tusipangiane mapenzi. Ndiaana ndumbaro anamke wake na mie ninae wangu. Nikiipenda Mamelodi usiniingilie.
 
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Damas Ndumbaro amesema Serikali itakutana na Shirikisho la Soka nchini na klabu za Simba na Yanga ili kuona inatoa mchango gani kuhakikisha timu hizo zinafanya vizuri robo fainali na kusonga mbele.

Waziri Ndumbaro amesema pamoja na mambo mengine, amewataka mashabiki kuacha kuwapokea mashabiki na wafahamu mechi hizi za robo fainali ni kufa na kupona na kinachotakiwa ni kuhakikisha timu zetu zinashinda.

Amesema Serikali itakula sahani moja na mashabiki wa Simba na Yanga ambao wataenda kupokea wageni uwanja wa ndege na kuwasapoti.

"Wiki iliyopita tulitoa tamko, Serikali tunataka kukaa na Simba, Yanga na TFF, ili watuambie kama serikali, tunahitaji kutoa mchango gani ili timu kushinda robo fainali na ziingie nusu fainali. Tunaweza kukutana Jumanne wiki ijayo ili kupanga mikakati."

Kuhusu mashabiki amesema; "Watanzania niwaombe sana najua kuna utani wa jadi, lakini kwenye mechi hizi za robo fainali ni mechi za kufa na kupona, hatutegemei kuona Mtanzania yeyote akienda kupokea wageni uwanja wa ndege, ama kuvaa jezi za timu za wageni."

"Sisi kama Serikali hatutawaachia hili TFF wala Simba na Yanga, kwa hiyo tukihangaika na mtu ambaye tutaona ni msaliti. Tunaomba Watanzania watuelewe na watusamehe kwa sababu tunataka timu hizi zifanikiwe."

"Kwa hiyo wewe Mtanzania ambaye utaweka kimbelembele kwenda kupokea wageni uwanjani wa ndege, kuwasapoti kwa namna yeyote, hatutakuelewa na tutadili na wewe kwa vile ambavyo tunaona inafaa."

"Tumekuwa nchi pekee iliyofanikiwa kuingiza timu mbili mwaka huu, lakini ukishapata mafanikio haupaswi kutumia muda mwingi sana kushangilia hayo mafanikio, unatakiwa uangalie unafanya nini ili kuendelea kupata mafanikio zaidi." Amesema.
Moja ya Mawaziri vilaza, na huyu hawezi kukosekana. Badala ya kuwashauri TFF kuwaacha wachezaji wa Yanga na simba ili wajiandae ipasavyo dhidi ya mechi zao za hatua ya Robo fainali; na hivyo kuchagua wachezaji wapya na wale wanaocheza nje kwa ajili ya lile Bonanza la FIFA!!

Yeye anaona huo ushauri una tija sana! Amesahau kwanza hao mashabiki wenyewe viherehere wanawakilisha idadi ndogo sana ya mashabiki wa timu husika! Na pia athari yake siyo kubwa kama hiyo ya kuwachukua wachezaji waandamizi kwenye timu, na kuwapeleka kucheza kwenye hilo bonanza la Fifa.
 
Huyu kwenye hii Wizara Amefeli, harakati zake zote kwenye hii wizara ni kuifurahisha serikali
 
Wakati eng Hersi anawapokea Kaizer ilikuwa wapi??😃😃 kama me chama langu mamelod kitambon tuu na lazima nikawapokee
 
Back
Top Bottom