Serikali yawafutia udhamini baadhi ya viongozi wa wanafunzi Urusi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yawafutia udhamini baadhi ya viongozi wa wanafunzi Urusi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TANMO, Dec 10, 2008.

 1. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #1
  Dec 10, 2008
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,908
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Waitwa nyumbani kwenda kujibu mashitaka

  jumatatu 8/12/2008 saa 14:30

  THE THOMCOM Imepata habari zisizo rasmi kuwa kuna wanafunzi sita toka chuo kikuu cha urafiki Lumumba Moscow Russia wameitwa nyumbani kwa kosa la kuvuruga amani. Inasemekana kuwa pindi watakapofika nyumbani watakabiliwa na mkono wa sheria. Inasemekana kuwa waraka wa kuwarudisha nyumbani wanafunzi hao umesainiwa na Mh. naibu waziri na kuwasilishwa chuoni kupitia ubalozi wa Tanzania. Wanafunzi hao ambao majina yao hayakupatikana mapema kutokana na chanzo cha habari hii, watapewa taarifa za kuondoka kwao leo jumatatu saa kumi kamili na Msaidizi wa Rector wa International Relation.

  Taarifa nyingine zisizo rasmi, INASADIKIKA kwamba mkataba uliosainiwa kati ya Tanzania na Chuo cha lumumba mwaka 2005 na kuhakikiwa mwaka 2007 umevunjwa.

  Kutokana na Ofisa mmoja chuoni Lumumba, wanafunzi hao wameivamia ofisi moja chuoni hapo, na kuwatolea maafisa maneno makali na ya kutisha. Haikufahamika mara moja ni wanafunzi gani wamefika ofisini hapo leo asubuhi na ni hatua gani zitakazochukuliwa na chuo katika swala hilo.

  Kati ya wanafunzi hao sita, inasemekana mmoja kati yao ni mwanafunzi aliyejiunga na chuo kikuu cha urafiki Lumumba mwaka 2008/2009 ambapo amedumu chuoni kwa muda wa takribani mwezi mmoja na kwa kawaida, hata hajapata usajili au residence permit na huenda hata hajaanza masomo ya awali ya Lugha.

  THE THOMCOM inaahidi kufuatilia sakata hili kwa ukaribu na kuwaletea mfululizo mzima wa sakata hili kwa usahihi zaidi na uhakika.

  Baadaye ndiyo majina yakatajwa:

  habari za uhakika zilizofikia mtandao wa The THOMCOM zimetaja majina ya baadhi ya wanafunzi walioitwa home ikiwa ni pamoja na kufutiwa udhamini wa serikali kama ifuatavyo...

  (1) Kanyathare Boniphace (huyu ndiye rais wa wanafunzi)
  (2) Kwagilwa Reuben (Katibu msaidizi)
  (3) Hussein Pazi
  (4) Ally Lusesa
  (5) Busury A. Omary
  (6) Jina bado halijafahamika

  MOSCOW 2008.

  Source: 1. Tanzania High Oriented Mass COMmunication (THOMCOM): WANAFUNZI SITA CHUO KIKUU LUMUMBA WAITWA NYUMBANI. MMOJA KATI YAO AMEJIUNGA CHUONI 2008. MKATABA WAVUNJWA

  2. Tanzania High Oriented Mass COMmunication (THOMCOM): BAADHI YA WANAFUNZI WALIOFUTIWA UDHAMINI WA SERIKALI WAJULIKANA
   
 2. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #2
  Dec 10, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35  Mbona habari hii ni mix kama confusion?! Hakuna mtiririko unaeleweka zaidi ya wanafunzi kurudishwa home. Huo mkataba ni nini hasa? Na hizo fujo za nini? Sasa kama mkataba umevunjwa, ina maana gani kwa wanafunzi wanaobakia?

  THOMCOM toa maelezo kamili na si kuchanganya issues hapa
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Dec 10, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Nini chanzo cha mgomo wao ama wao kuanza vurugu unaweza kutuhabarisha ?
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Dec 10, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Wafaransa wana msemo fulani unaoelezea hali ya kuona kitu ambacho kinatokea kwa mara ya kwanza lakini kinaleta hisia kuwa tayari kimewahi kutokea namna ile ile!
   
 5. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #5
  Dec 10, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  ???!???!?!
   
 6. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #6
  Dec 10, 2008
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,908
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Chanzo cha mgomo wao ni kitendo cha Serikali kuchelewa kuwapatia fedha za kujikimu pamoja na ada wanafunzi wapya waliojiunga katika mwaka wa masomo 2008/2009. Hali hii ilipelekea migomo ya mara kwa mara ambapo wanafunzi walikuwa wanaenda kukusanyika nje ya Ubalozi baada ya kukataliwa kuingia ndani.
   
 7. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #7
  Dec 10, 2008
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  dejavu... lakini noana ka haliyahewa ka kuwaona wameonewa bila kupata facts.. Hoja - Objectivety= JF

  kwikwikwi
   
 8. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #8
  Dec 11, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Yaani Tanzania kweli tuna safari ndefu sana kwa upande wa elimu hasa kwa raia wa kawaidi ambao hawana GODFADHA.

  Juzi juzi nimeambiwa kuwa wanafunzi wa kitanzania huko marekani walilopelekwa kwa udhamini wa wizara ya mali asili na utalii ambako wamefanya kazi kwa zaidi ya miaka kumi na tano. Baada ya kusoma miaka miwili huko vyuoni waliko, wizara hiyo imedai kuwa gharama za kuwasomesha ni kubwa hivyo ikaamua kijeuri kutowalipia tena; ikawasiliana na uongozi wa vyuo vile kwa lugha ya kijeuri bila hata kuwa na chembe ya diplomacy. Nasikia wanafunzi hao wanasota sana.
   
 9. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #9
  Dec 11, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135


  I might have some characters similar to yours; and that will explain why I chose to write you this :)
  A number of times I struggle not to expect others to be the way I would like them to be - as I have learned that, that is not the easiest way to go. At times, it is the wrong way.


  Kuna post yako nyingine nimeiona leo, inafanana na hii uloweka hapo juu.
  Watakuwepo wengi wanaopenda kuona "more objectivity" humu jamvini. .....Hutashindwa kuiboresha JamiiForums japo kwa asilimia fulani, iwe vile wewe ambavyo ungependa.
   
Loading...