Serikali yawadanganya wahisani kuhusu bajeti! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yawadanganya wahisani kuhusu bajeti!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WikiLeaks, Dec 6, 2010.

 1. W

  WikiLeaks Member

  #1
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wahisani wanaochangia bajeti kuu ya Tanzania (GBS) wameikataa bajeti waliyopelekewa na serikali ya Tanzania kuwa ni tofauti na iliyopitishwa na bunge Julai mwaka huu.

  Jamani hii si aibu na kashfa kwa serikali ya Tanzania.

  Nani ameibua kashfa hii? Stay tuned.

  UPDATE:

  Tuesday, 07 December 2010
  By The Citizen Reporter

  Tanzania’s development partners have said the deficits that are complicating implementation of the 2010/11 Budget are a consequence of both the lack of adequate consultations between the government and donors and poor budget processes.

  Speaking in Dar es Salaam yesterday at the ongoing National Policy Dialogue meeting, a representative of donors who support Tanzania’s budget, Mr Svein Baera, said the 2010/11 Budget was prepared on the basis of over optimistic revenue forecasts matched with high expenditures.

  He noted that the government also failed to put in place a strategy that would facilitate prioritisation of expenditures in the event of revenue shortfalls as it is happening now.

  “There are differences between the budget presented to the IMF executive board and the one approved by Parliament in July 2010
  , with much more optimistic revenue forecasts and a higher level of domestic financing used to justify sharply higher expenditures,” said Mr Baera, a minister counselor at the Royal Norwegian embassy in Dar es Salaam.

  He noted that poor budget preparations that do not take care of possible future revenue shortfalls “undermine the credibility of the budget as an effective policy and planning tool.”

  He noted further that deliberate avoidance of dialogue with donors by the government “calls into question the quality of our policy dialogue and partnership.” Donors contribute about 36 per cent of Tanzania’s the budget resources.

  The 14 GBS development partners under, the chairmanship of Norway, are expected to give Tanzania $534 million (Sh748 billion) this financial year.

  The amount is $220 million less than the $754 million given during the last financial year
  . The government tabled a Sh11.6 trillion Budget in Parliament in June, promising to finance over half of it (Sh6 trillion) from revenue collections.

  The Finance and Economic Affairs minister, Mr Mustafa Mkulo, who was also present as donors laid blame on the government, declined to respond.

  When pressed by The Citizen, he said he would only offer clarification on Wednesday when issues specific to the Budget would be discussed in the ongoing meeting.

  Mr Mkulo invited Mr Baera to his office for discussions, noting, however, that the government would deal with all the issues raised by development partners at the meeting.

  Following the donors’ accusations, the MP for Kigoma North, Mr Kabwe Zitto, said he would pursue the matter further to know exactly what happened.

  “It’s very shocking….I’ve launched investigations into this so that the truth may be known… normally, one expects the government to present to development partners what has been passed by the National Assembly,” the firebrand opposition MP, who is participating in the meeting, told The Citizen.

  In his investigations, Mr Zitto stated, he would first aim to get hold of the budget that was handed to development partners and outline differences between it and the one that Parliament passed.

  “Our aim will be to see to it that the government explains which of the two it is implementing... is it the one passed by Parliament or the one that was presented to donors?” he said.

  In order to sort out the revenue gap in the Budget, donors yesterday urged the government to consider reducing tax exemptions so that they are at par with those granted in other countries.

  “This could contribute significantly to increased domestic revenue and close the fiscal gap over the medium to longer term,” Mr Baera said.

  A recent analysis by Uwazi-Twaweza reveals that Tanzania has granted tax exemptions amounting to $3.8 billion during the past ten years, even as the country grapples with failure to meet revenue collection targets.

  In 2008/09 and 2009/10, tax exemptions were 2.8 and 2.3 per cent respectively, of the country’s GDP. According to Uwazi, in Kenya and Uganda tax exemptions amounted to one per cent and 0.4 per cent of the countries’ GDPs respectively.
   
 2. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  tupe news
   
 3. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  id yako ya mwanzo ipi vile?
   
 4. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  JK, RA, AC na EL ndiyo waliochakachua bajeti ili wafidie gharama za uchaguzi wa 31.10.2010!!! Kuna jamaa amewatonya wenye pesa!!!! Nadhani yule mkuu wa waangalizi wa kimataifa, yule David Martin naye amechangia,maana alizuiliwa na kiravu na makame asichungulie kwenye chumba cha kuchakachulia na kutengeneza matokeo hewa!!!! We subiri ripoti yake utaamini haya nisemayo!!!!!!!!
   
 5. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa hili Zitto tuko pamoja ila tatizo lako huwa hukawii kutugeuka ukionjeshwa kitu kidogo.
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,895
  Likes Received: 416,601
  Trophy Points: 280
  Monday, 06 December 2010
  Mwandishi Wetu (Exuper Kachenje)

  KUNDI la wahisani wanaochangia bajeti kuu ya Tanzania (GBS) limeibua kashfa baada ya kueleza kuwa serikali iliwapelekea bajeti tofauti na ile iliyopitishwa na Bunge Julai mwaka huu.

  Taarifa za kashfa hiyo ziliwekwa hadharani jana asubuhi na mwenyekiti wa wahisani hao, Svein Baera wa Sweden katika mkutano wa kitaifa wa mwaka wa majadiliano ya kisera na bajeti uliofanyika jijini Dar es salaam.

  Sweden ndiyo inayoshikilia uenyekiti wa kundi hilo linalojumuisha taasisi za kimataifa na nchi mbalimbali zilizoendelea.

  Kuibuliwa kwa kashfa hiyo kunakuja wakati wahisani hao wakiwa wamezuia theluthi moja ya zaidi ya dola 800 milioni za Kimarekani ambazo zinatakiwa zichangie kwenye bajeti kuu ya 2010/11, wakiishinikiza serikali iharakishe utekelezaji wa programu ya mageuzi, yakiwemo ya mfumo wa usimamizi wa fedha za seikali.

  Akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo wa siku tatu, Baera aliainisha maeneo sita kuwa ndiyo mhimili wa mjadala wao na serikali.

  "Napenda kuainisha maeneo sita ya ujumbe wetu ili kuweka sawa jukwaa la majadiliano yetu haya ya mwaka. Kuna tofauti kati ya bajeti iliyowasilishwa kwa bodi ya (Shirika la Kimataifa la Fedha) IMF na ile iliyopitishwa na Bunge Julai 2010," alisema Baera.

  Alisema bajeti ambayo serikali iliwasilisha kwa wahisani hao ilibeba "matumaini makubwa ya kuzaa matokeo mazuri na kufanywa kama sababu ya kupitisha matumizi makubwa ya fedha zitokanazo na mapato ya ndani".

  Baera alisema kuwa kukosekana kwa uwazi katika matumizi, vipaumbele, mapato na mfumo mzima wa fedha kunapunguza kuaminika kwa bajeti hiyo mbele ya wafadhili.

  Kwa mujibu wa wahisani hao, kumekuwepo na mtiririko wa athari katika bajeti katika miaka ya karibuni huku ikionyesha ongezeko kubwa la matumizi ya kawaida kuliko yale ya maendeleo.

  Kwa mujibu wa bajeti ya mwaka 2010/11 ambayo ni ya Sh11.1 trilioni, matumizi ya kawaida ya serikali ni Sh7.8 trilioni wakati fedha zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo ni Sh3.2 trilioni.

  Bajeti hiyo inaonyesha kuwa kati ya Sh11.1 trilioni, serikali ilitarajia kupata Sh6 trilioni kutoka katika vyanzo vya ndani, wakati inatarajia Sh2.8 trilioni kutoka kwa wahisani na mikopo. Fedha nyingine zinatarajiwa kutoka mikopo ya ndani, masharti ya kibiashara na ubinafsishaji.

  "Matumaini makubwa kupindukia katika bajeti hii na kutokuwepo kwa mikakati inayoeleweka ya kipaumbele katika matumizi katika hali inayoweza kutokea ya mapato madogo na ukosefu wa fedha, yanaweza kuondoa kuaminika kwa bajeti kama chombo cha ufanisi wa sera na mipango," alisema Baera.

  Zaidi ya hapo, ukweli kwamba bajeti hii tofauti ilipitishwa bila ya kuwepo mawasiliano ya awali na wabia wa maendeleo inaweka maswali kwenye ubora wa mazungumzo yetu ya sera na ubia. Tunatarajia kujadili suala hili kwenye sehemu muhimu ya bajeti.

  "Zaidi ya hapo, bajeti iliyotumiwa kuanzia mwaka jana iliendeleza mwenendo wa miaka ya karibuni ambako matumizi ya kawaida yanaendelea kupanda kwa kasi kuliko matumizi kwenye maendeleo."

  Kutokana na hali hiyo GBS imeitaka serikali kujipanga upya na kuweka mkazo katika kupunguza misamaha ya kodi ili kuweka uwiano na ufanisi sawa na nchi za kundi lake katika uchumi, hatua ambayo Baera alisema itapunguza pengo la bajeti linaloikabili Tanzania kila mwaka.

  Tayari GBS imebainisha kuwa bajeti ijayo inaweza kuwa na nakisi ya hadi Sh1 bilioni.

  Hata hivyo, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo ambaye alishiriki mkutano huo, alipatwa na kigugumizi kujibu madai hayo ya GBS, akimkaribisha mwenyekiti huyo wa kundi la nchi wahisani aende ofisini kwake ili wazungumzie masuala hayo.

  "Kuna mengine yanazungumzika; Baera ninakukaribisha ofisini kwangu; mengine yanazungumzika ofisini," alisema Mkulo.

  Naibu kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Zitto Kabwe alizungumzia kasoro hiyo jana akieleza kuwa imemshtua na kwamba ataifuatilia.

  Zitto, ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kaskazini na ambaye alihudhuria mkutano huo jana, alisema kambi ya upinzani itaunda kamati kulifuatilia suala hilo.

  Alisema pia watahoji suala hilo bungeni na kuitaka serikali iweke wazi kwa Watanzania ni bajeti ipi inayotumika kati ya iliyopitishwa na Bunge na ile iliyopelekwa IMF.

  "Huu ni mshtuko kwangu; hili limenishtua. Tutaunda timu ya kulifuatilia; tutalifikisha bungeni na kuihoji serikali ieleze ni bajeti ipi inayotumika. Ni ile iliyopitishwa na Bunge au iliyopelekwa IMF," alisema Zitto.

  Kundi hilo la nchi wahisni limesema kuwa linaunga mkono mkakati wa serikali wa Kilimo Kwanza na wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) kuhusu maendeleo ya kilimo, hifadhi ya chakula na kupunguza umasikini.
   
 7. M

  Mtukufu Member

  #7
  Dec 7, 2010
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi nimeshindwa kuchangia wamenichosha ila najua siku sio nyingi hawapo
   
 8. A

  August JF-Expert Member

  #8
  Dec 7, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Hii paragraph 6 ndio ilionivutia kwamba waliwakimbia Donors katika kuitairisha kabla ya uchaguzi, sasa mambo yamewazidi ndio wanawa fuata donor
  "He noted further that deliberate avoidance of dialogue with donors by the government "calls into question the quality of our policy dialogue and partnership." Donors contribute about 36 per cent of Tanzania's the budget resources"
   
 9. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #9
  Dec 7, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,499
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  Wahisani waiumbua serikali Send to a friend Monday, 06 December 2010 22:45

  0diggsdigg

  Mwandishi Wetu (Exuper Kachenje)

  KUNDI la wahisani wanaochangia bajeti kuu ya Tanzania (GBS) limeibua kashfa baada ya kueleza kuwa serikali iliwapelekea bajeti tofauti na ile iliyopitishwa na Bunge Julai mwaka huu.Taarifa za kashfa hiyo ziliwekwa hadharani jana asubuhi na mwenyekiti wa wahisani hao, Svein Baera wa Sweden katika mkutano wa kitaifa wa mwaka wa majadiliano ya kisera na bajeti uliofanyika jijini Dar es salaam.

  Sweden ndiyo inayoshikilia uenyekiti wa kundi hilo linalojumuisha taasisi za kimataifa na nchi mbalimbali zilizoendelea.

  Kuibuliwa kwa kashfa hiyo kunakuja wakati wahisani hao wakiwa wamezuia theluthi moja ya zaidi ya dola 800 milioni za Kimarekani ambazo zinatakiwa zichangie kwenye bajeti kuu ya 2010/11, wakiishinikiza serikali iharakishe utekelezaji wa programu ya mageuzi, yakiwemo ya mfumo wa usimamizi wa fedha za seikali.

  Akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo wa siku tatu, Baera aliainisha maeneo sita kuwa ndiyo mhimili wa mjadala wao na serikali.

  "Napenda kuainisha maeneo sita ya ujumbe wetu ili kuweka sawa jukwaa la majadiliano yetu haya ya mwaka. Kuna tofauti kati ya bajeti iliyowasilishwa kwa bodi ya (Shirika la Kimataifa la Fedha) IMF na ile iliyopitishwa na Bunge Julai 2010," alisema Baera.

  Alisema bajeti ambayo serikali iliwasilisha kwa wahisani hao ilibeba "matumaini makubwa ya kuzaa matokeo mazuri na kufanywa kama sababu ya kupitisha matumizi makubwa ya fedha zitokanazo na mapato ya ndani".

  Baera alisema kuwa kukosekana kwa uwazi katika matumizi, vipaumbele, mapato na mfumo mzima wa fedha kunapunguza kuaminika kwa bajeti hiyo mbele ya wafadhili.

  Kwa mujibu wa wahisani hao, kumekuwepo na mtiririko wa athari katika bajeti katika miaka ya karibuni huku ikionyesha ongezeko kubwa la matumizi ya kawaida kuliko yale ya maendeleo.

  Kwa mujibu wa bajeti ya mwaka 2010/11 ambayo ni ya Sh11.1 trilioni, matumizi ya kawaida ya serikali ni Sh7.8 trilioni wakati fedha zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo ni Sh3.2 trilioni.

  Bajeti hiyo inaonyesha kuwa kati ya Sh11.1 trilioni, serikali ilitarajia kupata Sh6 trilioni kutoka katika vyanzo vya ndani, wakati inatarajia Sh2.8 trilioni kutoka kwa wahisani na mikopo. Fedha nyingine zinatarajiwa kutoka mikopo ya ndani, masharti ya kibiashara na ubinafsishaji.

  "Matumaini makubwa kupindukia katika bajeti hii na kutokuwepo kwa mikakati inayoeleweka ya kipaumbele katika matumizi katika hali inayoweza kutokea ya mapato madogo na ukosefu wa fedha, yanaweza kuondoa kuaminika kwa bajeti kama chombo cha ufanisi wa sera na mipango," alisema Baera.

  Zaidi ya hapo, ukweli kwamba bajeti hii tofauti ilipitishwa bila ya kuwepo mawasiliano ya awali na wabia wa maendeleo inaweka maswali kwenye ubora wa mazungumzo yetu ya sera na ubia. Tunatarajia kujadili suala hili kwenye sehemu muhimu ya bajeti.

  "Zaidi ya hapo, bajeti iliyotumiwa kuanzia mwaka jana iliendeleza mwenendo wa miaka ya karibuni ambako matumizi ya kawaida yanaendelea kupanda kwa kasi kuliko matumizi kwenye maendeleo."

  Kutokana na hali hiyo GBS imeitaka serikali kujipanga upya na kuweka mkazo katika kupunguza misamaha ya kodi ili kuweka uwiano na ufanisi sawa na nchi za kundi lake katika uchumi, hatua ambayo Baera alisema itapunguza pengo la bajeti linaloikabili Tanzania kila mwaka.

  Tayari GBS imebainisha kuwa bajeti ijayo inaweza kuwa na nakisi ya hadi Sh1 bilioni.

  Hata hivyo, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo ambaye alishiriki mkutano huo, alipatwa na kigugumizi kujibu madai hayo ya GBS, akimkaribisha mwenyekiti huyo wa kundi la nchi wahisani aende ofisini kwake ili wazungumzie masuala hayo.

  "Kuna mengine yanazungumzika; Baera ninakukaribisha ofisini kwangu; mengine yanazungumzika ofisini," alisema Mkulo.

  Naibu kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Zitto Kabwe alizungumzia kasoro hiyo jana akieleza kuwa imemshtua na kwamba ataifuatilia.

  Zitto, ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kaskazini na ambaye alihudhuria mkutano huo jana, alisema kambi ya upinzani itaunda kamati kulifuatilia suala hilo.
  Alisema pia watahoji suala hilo bungeni na kuitaka serikali iweke wazi kwa Watanzania ni bajeti ipi inayotumika kati ya iliyopitishwa na Bunge na ile iliyopelekwa IMF.

  "Huu ni mshtuko kwangu; hili limenishtua. Tutaunda timu ya kulifuatilia; tutalifikisha bungeni na kuihoji serikali ieleze ni bajeti ipi inayotumika. Ni ile iliyopitishwa na Bunge au iliyopelekwa IMF," alisema Zitto.

  Kundi hilo la nchi wahisni limesema kuwa linaunga mkono mkakati wa serikali wa Kilimo Kwanza na wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) kuhusu maendeleo ya kilimo, hifadhi ya chakula na kupunguza umasikini.

  Source: Mwananchi
   
 10. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Jamani udanganyifu wa Bajeti siyo kwa donors tu, wabunge na mawaziri hudanganywa kila mwaka. Wabunge hupitisha bajeti ambayo hawaijui na mawaziri hutetea bungeni bajeti ambayo hawaijui. ukitaka ushahidi wa hili uchukue hotuba ya bajeti ya waziri yoyote kisha uchukue MTEF utaona siyo kila anachosema waziri bungeni kiko kwenye MTEF.

  Undanganyifu unatokeaje? Mtakumbuka lile sakata la ujenzi wa nyumba za gavana ambalo zitto aliliundia tume. matumizi ya pesa zile yalikuwa yamepitishwa na Bunge, kisha wakaja kushangaa kwamba serikali imetumia pesa nyingi mno katika huo ujenzi. Hii inatokea kwa sababu wabunge wetu huwa hawajadili bajeti, wanajadili hotuba ya waziri husika ambayo imeandaliwa kimtego ili wabunge wapitishe bajeti husika.

  Sababu ya pili wabunge wanapitisha bajeti mbovu ya serikali bila kujua ni kwa sababu kila mbunge (hasa wa ccm) hutumia muda mrefu kuzungumzia matatizo ya jimbo lake na kuwasifu viongozi wa chama na serikali (kujikomba).

  Namna nyingine ni pale mbunge anapodai serikali ifanye jambo fulani bila kukita madai yake kwenye bajeti aliyopewa kupitisha. Kwa mfano, mbunge anadai serikali iunganishe vijiji vya jimbo lake kwenye grid ya umeme ya taifa badala ya kuonesha ni vipi hiyo pesa inaweza kupatikana kutoka na bajeti ya wizara iliyowasilishwa. Kazi ya waziri hapo inakuwa ni rahisi kabisa "Mh. Spika, serikali yetu inajitahidi kuhakikisha katika mwaka huu wa fedha upembuzi yakinifu utafanyika ili mwaka ujao wa fedha tuhakikishe vijiji hivi vinaunganishwa katika grid ya taifa" (makofi). Pesa kiasi gani zimetengwa kufanya huo upembuzi? ziko kwenye vote gani katika bajeti?
   
 11. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Leteni vitu:
  1. Dowans kulipwa kwa kasi zaidi.
  2. Mgao wa umeme kuwa mkali kwa kasi zaidi.
  3. Mfumuko wa bei kwa kasi zaidi.
  4. Bajeti feki.

  Ni uchakachuaji kwa kwenda mbele.
   
 12. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #12
  Dec 7, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Nina hakika walichakachua fedha hizi kwa ajili ya Ucahaguzi....wabishe! Kama kawa Mwananchi pekee ndilo limeandika inamaana waandishi wengine hawakuwepo au hawakusikia?
   
 13. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #13
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Serikali ya kiwiziwizi tuuuuuuuuu.
   
 14. N

  Nightangale JF-Expert Member

  #14
  Dec 7, 2010
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 261
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Halafu PM anajifanya kukataa shangingi
  What difference does that make anyway!
   
 15. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #15
  Dec 7, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,499
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  Matapeli Kazini!!
   
 16. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #16
  Dec 7, 2010
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Kama kweli wanataka kutuaminisha kuwa wanaweka maslahi ya taifa mbele..... tuone mkulo na genge la wezi wenzie ama wajiuzuru wenyewe au wawajibishwe na bosi wao(naota tu jamani)
   
 17. D

  Dick JF-Expert Member

  #17
  Dec 7, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Waziri wa Fedha na Uchumi aachie ngazi/awajibike.
   
 18. C

  Chief JF-Expert Member

  #18
  Dec 7, 2010
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Watu kujipa mahope bwana, basi tu.
   
 19. N

  Nightangale JF-Expert Member

  #19
  Dec 7, 2010
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 261
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 20. N

  Nightangale JF-Expert Member

  #20
  Dec 7, 2010
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 261
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Just like that? Hapa hapa Tz?
   
Loading...