Serikali yatoa tahadhari ya ugonjwa wa Chikungunya, ambao umetokea Mombasa Nchini Kenya

Hii homa imepiga sana Mombasa. Nina ndugu anaeishi huko asema mtaa wake wote, zaidi ya watu 20 waliamka siku moja wakiwa hawawezi kushuka vitandani, wanatambaa kwenye vyooni! Baadhi ya symptoms zake, mtu hunyong'onyea sana na kwa siku tatu hivi hawezi kusimama wima. Haielekei kama unauwa, pengine watu wenye complications nyingine.
Mi nadhani hii ni dalili nyingine ya majaribio ya wazungu ya silaha za kibaiolojia dhidi ya watu weusi barani Afrika, sawa na ule mlipuko wa Ebola Afrika Magharibi. Alama kuu utaona baada ya muda utapotea na usirudi tena kwa maana wamekwisha assess kiwango cha athari zake.
Ukisema hivi watu wanaojidai wana akili sana wanakuambia ni "conspiracy theory". Ukiwauliza kwa nini Ebola ya Afrika Magharibi iliuwa Waafrika tu na hakuna hata Mzungu aliyedhurika....wanakukodolea macho!
Watu wenye kuchunguza maendeleo ya mambo ya dunia hiii wanafuatilia kwamba si aghalabu kusikia milipuko ya magonjwa haya ya ajabu ajabu Marekani au Ulaya Magharibi au hata Mashariki. Haya ni majaaliwa ya Afrika, baadhi ya nchi za Asia na Latin America basi!
Nani alikwambia Ebola haikuua wazungu?
 
Hakuna cha Makunganya wala Chichidodo..

spinning tu hizi kufifisha pumba za pogba kuua elimu Tanzania na issue ya Mloganzila plus njiti kufa muhimbili..

Ujinga Ujinga tu..namfahamu personally Ummy..confidence yake yote kama mwanasheria msomi imewekwa kwapani..no wonder alikua anakomeshwa na Sofia Simba alipokua bosi wake!
Ni kweli wamepoteza credibility na hata ikitokea wanasema ukweli bado watatiliwa shaka tu
 
Katika mawaziri ambao kusema vitu vya hovyo ni huyu mama. Hata siku moja hajawah kujituma kulijua jambo kwa undan ndipo alitolee ufafanuzi.

Ukimkuta kakomaa huduma za mama mjamzito bure unadhan kweli. Sasa ww nenda Hosp eti ni mjamzito huna hela uone. Utasota kwenye benchi hatar.

Na sijui wanaona nini kusema tu mama anayeweza klinik ya ujauzito anatakiwa alipe gharama sh 16500/= kwa ajili ya vipimo vya awali.

Anajushebedua tuu huduma za mama na mtt bure kumbe hola
bestito hahaaaaaaaaaa umeniacha nicheke kwa nguvu hapa aiseee kweli huyu mama hata mm simuelewi kabisa anaropoka tu hovyo bila hata kupima
 
Chigunguja dawayake ni kulala kushusha net na kulala mapeemaaaa,hakika chigungunya haikupati ng'o
Sasa ninyi mnaosema ameharibu huko nyuma, mlitaka aharibu na hapa? Katimiza wajibu wake kama kiongozi. Ugonjwa umelipuka, mnataka akae kimya ili baadaye mje kutoa povu tena kuwa hakuwajibika? Tuwe tunachambua vya kulalamika wakati mwingine
 
View attachment 679605
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa tahadhari kuhusu ugonjwa wa homa ya Chikungunya ambao umeripotiwa na vyombo vya habari kutokea jijini Mombasa nchini Kenya.

Taarifa iliyotolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu imesema kuwa mpaka sasa Shirika la Afya Duniani (WHO) bado haijatoa taarifa rasmi lakini wao wanaotoa taadhari kuzingatia muingiliano mkubwa wa watu baina ya nchini hizi mbili Kenya na Tanzania.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya wanasema kuwa ugonjwa wa Chikungunya unasababishwa na kirusi ambacho kinaenezwa mbu wa aina ya Aedes na kusema ugonjwa huu si mgeni nchini Tanzania kwani ulishawahi kutokea.

Tiba ya ugonjwa huo bado haijagundulika, matibabu yake ni kwa ajili ya kupunguza makali ya dalili zake.

EATV

Habari zaidi soma=>Mombasa: Watu 30 walazwa hospitalini kutokana na ugonjwa wa Chikungunya
Ee Mungu mwenye rehema tunakuomba utuepushie mbali Chikungunya maana ugonjwa huu ukiingia ndani ya serikali hii siyojali raia wake hakuna atakayebaki salama.
 
Hapana hata wazungu walikufs kwa ebola tena wamarekan wengi tuu.

Ishu ni kwamba mlipuko wa magonjwa haya unachangia na vitu vingi sana ikiwemo mabadiliko ya tabia ya nchi, kuzaliwa kwa vijidudu tofauti kutokana na evolution, resistance inayojengwa na madudu dhidi ya dawa za kudhibiti hawa madudu nayo huibua magonjwa mapya, tafiti n madawa tunayotumis haya ni kwa uchache tuu.

Dunian kote kuna sheria inayokataza matumiz ya biological weapon kwan madhara yake ni makubwa zaidi ya unavyo dhani
Duh! Evolution.....yaani it's only Africa and other developing countries ndio bado zina-evolve:confused:
 
Sasa ninyi mnaosema ameharibu huko nyuma, mlitaka aharibu na hapa? Katimiza wajibu wake kama kiongozi. Ugonjwa umelipuka, mnataka akae kimya ili baadaye mje kutoa povu tena kuwa hakuwajibika? Tuwe tunachambua vya kulalamika wakati mwingine
Mkuu usipende kutetea ujinga. Huyu mama si ndiye alikuwa akipiga debe kwamba hakuna mgonjwa anayelala chini wakati wagonjwa kibao wanalala chini kila siku?
 
Jamani hebu tuache mambo ya siasa kwenye ukweli. Hii homa ikigundukiwa Tanzania mtwara mwaka 1952. Chikungunya ni jina ka kimakonde likimaanisha kujipinda...mtu anasikia maumivu makali ya viungo na anajikunja. Ni vema kusikiliza wataalamu na kuchukua tahadhari badala ya kuongela habari za mloganzila mara tundu lissu. Be serious nyie wagalatia..
 
Acha kbs Bora enzi za mkwere tulikuwa na hati punguzo kwa huyu baba hakuna cha hati punguzo wala panadol ya bure
 
Magonjwa nayo yamezidi sasa!

Kila leo Ugonjwa mpya masikioni mwangu
 
Haya msomi. Lakini nakuomba u google kwani siku hizi mamo yote yako nje kama utaondoa uvivu.
 
Hii homa imepiga sana Mombasa. Nina ndugu anaeishi huko asema mtaa wake wote, zaidi ya watu 20 waliamka siku moja wakiwa hawawezi kushuka vitandani, wanatambaa kwenye vyooni! Baadhi ya symptoms zake, mtu hunyong'onyea sana na kwa siku tatu hivi hawezi kusimama wima. Haielekei kama unauwa, pengine watu wenye complications nyingine.
Mi nadhani hii ni dalili nyingine ya majaribio ya wazungu ya silaha za kibaiolojia dhidi ya watu weusi barani Afrika, sawa na ule mlipuko wa Ebola Afrika Magharibi. Alama kuu utaona baada ya muda utapotea na usirudi tena kwa maana wamekwisha assess kiwango cha athari zake.
Ukisema hivi watu wanaojidai wana akili sana wanakuambia ni "conspiracy theory". Ukiwauliza kwa nini Ebola ya Afrika Magharibi iliuwa Waafrika tu na hakuna hata Mzungu aliyedhurika....wanakukodolea macho!
Watu wenye kuchunguza maendeleo ya mambo ya dunia hiii wanafuatilia kwamba si aghalabu kusikia milipuko ya magonjwa haya ya ajabu ajabu Marekani au Ulaya Magharibi au hata Mashariki. Haya ni majaaliwa ya Afrika, baadhi ya nchi za Asia na Latin America basi!
:eek::eek::eek:Yaani Mkuu umeziba mianya yote ya michango kinzani nawe
 
Back
Top Bottom