Serikali yatoa siku 4 kwa wafanyabiashara wa Korosho kusema tani wanazohitaji. Baada ya hapo hawataruhusiwa tena kununua

Barua za siku hizi zinakua tofauti kabisaa na zile tulizofundishwa mashuleni,za siku hizi ziko kama makala vile.
 
Magufuli mzee wa nyuma mwiko..viongozi wengi wa afrika wangekuwa na misimamo hii afrika ingekuwa mahali bora sana kwa waafrika.
Si alisema serikali itazinunua zote tunasubiri utekelezaji matamko ya nini tena.
 
Ngojea tuone sasa maana huu ndo ile gagsta republic! Mlisema hela ipo msiweke maneno mengi nunueni korosho zote na mlisema mtabanguaje sijui! This is business simple no one wants loss na nyie mnataka kiki za kisiasa! Na bado yajayo yanafurahisha zaidi.
 
Ngojea tuone sasa maana huu ndo ile gagsta republic! Mlisema hela ipo msiweke maneno mengi nunueni korosho zote na mlisema mtabanguaje sijui! This is business simple no one wants loss na nyie mnataka kiki za kisiasa! Na bado yajayo yanafurahisha zaidi.
Tulia kwenye kitu uone kitu..
 
Mbona PM hajasema hatima yake?.....Serikali hii ni ajabu sana NJE YA NCHI hawapendwi NDANI YA NCHI ndiyo hivyo tena !
Ni serikali ya nani?Ni Serikali ya Rais Magufuli na rafiki na jamaa zake au ni serikali ya MPITO?
 
Yafaa kujikumbusha maswali ya Mh Zito kabwe ktk hili pale alipomuiliza mmoja wa mawaziri akagoma kujibu

Bungeni kwanini tushtakiwe na Acacia wakati tuna mazungumzo nao?

Swali la Pili: Serikali pia ilitoa taarifa kwa umma kuwa tuliahidiwa kishika uchumba cha dola milioni 300 sawa na Tsh bilioni 700 na mpaka sasa hatujapata, na sasa sasa serikali imefungua kesi dhidi ya makampuni tanzu ya Acacia ya Bulyanhulu na Pangea kwa masuala yanayohusiana na tax avoidance, na hili ndio suala ambalo Serikali ilitakiwa kufanya tangia mwanzo na sio kadhia zote zile za makinikia. Je, serikali imejifunza kutumia maarifa kwenye kukabiliana na changamoto mbalimbali za nchi badala ya kutumia ubabe
 
Mbona anababaika? Si alisema serikali itanunua? Ukiona hivyo hakuna hela
Magu ni jeur sana. Anauwezo wa kuzinunua na kuziacha hata ziozee kwenye maghala. Kwaza yeye kma yeye hana hasara maana pesa ni za mlipa kodi. Anaweza fanya ivyo imrad tu aonekane kwasaidia wakulima ili ajinyakulie sifa lakini mwisho wa siku aitie hsra nch
 
USHAURI WA BURE;
Biashara ni Network - Kumbuka hawa wanunuzi wana Network na wanunuzi; lazima serikali ijue root cause; JUA KULE NJE TUNAUZIA PRIVATE SECTOR , AMBAYO INA SIMAMIWA NA SERIKALI ZA HUKO; IKI GOMA PRVATE SECTOR;SERIKALI YA HUKO HAINA NGUVU.
TUJUE WALE WANAYO STOCK YA MIAKA 5-10; WANAJUA MAJANGA YA KISIASA, MAGONJWA .
ISIJE SERIKALI IKANUNUA ZIKAKAA KWENYE MAGHALA NCHINI;
SERIKALI , SEKTA BINAFSI WAKAE
 
Maajabu haya!

Yaani ufutie watu usajili kisa wameshindwa kununua bidhaa/korosho? Kama bei imeporomoka, wao wafanyaje?

Hata kwenye sukari kulikuwa na vitisho vya aina hii ila mwisho wa siku yakawashinda.

Hili zao ndio limeshakufa hapa chini na sidhani kama wakulima watalima tena hili zao.
Hahahahahaa..

Try to be positive sometimes..
 
Maajabu haya!

Yaani ufutie watu usajili kisa wameshindwa kununua bidhaa/korosho? Kama bei imeporomoka, wao wafanyaje?

Hata kwenye sukari kulikuwa na vitisho vya aina hii ila mwisho wa siku yakawashinda.

Hili zao ndio limeshakufa hapa chini na sidhani kama wakulima watalima tena hili zao.



Umesoma hayo maelezo vizuri au umekurupuka?? Bei ya soko duniani ni nzuri kabisa so sio tatizo. Muwe positive sio kila kitu upinga tu kama sio watanzania. Mkulima lazima afaidike kwa kazi ya mikono yake
 
Waziri Mkuu yuko TBC Live akitoa tamko la Serikali.

Serikali imetoa muda wa siku nne pekee, kuanzia leo Ijumaa hadi Jumatatu kwa Kampuni zote 35 nchini zilizojiandikisha kununua korosho kuhakikisha zinajirodhesha katika Ofisi ya Waziri Mkuu, zikieleza kunuia kununua korosho na kueleza kiwango cha korosho zinazotarajiwa kununuliwa na kampuni hizo.

Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa amesema, watakaokuwa tayari waandike katika Ofisi ya Waziri Mkuu lakini watakaoshindwa kuomba kununua korosho, hawataruhusiwa kununua korosho.

Waziri Mkuu amesema korosho iliyozalishwa mwaka huu ni kiasi cha tani zipatazo 200,000 ambazo ni pungufu kulinganisha na za mwaka jana.
Wafanyabiashara 35 wametekwa tayari !
 
Nafurahi Sana nazidi kupata matumaini kuona serikali yangu haiyumbishwi
Safi Sana walizoea..na huu NI ujumbe tosha kwa vikundi vingine vinavyoamini vina nguvu kuliko ofisi ya Rais
Wawe wauza madawa ya kulevya,wawe Wala ruzuku,wawe wafadhili wa mashoga,wawe waaandishi mankanjanja wote wakae wakijua awamu hii iko on fire walete tu vichwa vyao uone Magufuli anavyovikata kwa shoka
Imeyumbishwa na mashoga itakuwa Korosho?
 
Tahadharini wakulima wa korosho,kumbukeni hadithi hii waliambiwa wakulima wa dengu
Mwaka mmoja baadaye wakulima wa dengu wameambiwa wazile wenyewe kuwa zina proteins nyingi
 
Back
Top Bottom