Haya pia bado si sababu ya udikiteta na ufisadi uliofanywa na Mkandara kwenye hii issue ya wanafunzi.
Si kweli kwamba haya yanatokea kila siku. Mambo ya ngono yapo hata Harvard na sio sababu tu ya kudiscrediti wanafunzi nakisha kuwapiga mabomu.
Ngabu hapa inabidi kweli usemi wako utumike tena.
Yaani huuyu Mkandara na wenzake hapo wamefanya kitu ambacho wanajua kuwa wanafunzi hawatakubali hata kidogo na inakuwa kama vile wamefanya makusudi au kwenye usemi wako - ndivyo walivyo.
Utashangaa kusikia kuwa huyu Mkandara ni rafiki ya karibu wa Kikwete na mshauri wake wa kisiasa. No wonder nchi inakwenda kuzimu.
Yaani wanakimbilia kupiga wanafunzi, kuwafukuza chuo, na kuwaweka ndani wakati richmonduli bado wanalipwa mabilioni ya pesa na kina Chenge na Karamagi wakidunda mtaani kama hawana akili nzuri vile.
Ni wakati mwingine tena na pia fursa nyingine tena ambayo wana UDSM hawatakiwi kuichezea!Sasa mwendo ni mbele na hakuna kurudi nyuma! Nyie ndio chachu ya mabadiliko nchini mwetu! Historia ya dunia inaonyesha hivyo!Wanafunzi wa UDSM simamieni haki yenu bila woga. Na labda hamjui tu, lakini nguvu yenu na ushawishi wenu katika jamii ni mkubwa ajabu. Wanafunzi wa vyuo vikuu huko Indonesia waliweza kuuondoa madarakani utawala wa kifisadi miaka ya 80/90.
Huu ubeberu ungekuwapo pia katika kufuta mikataba mibovu..........mbona pangekuwa hapakaliki??
Prof Maghembe.........hatua uliyochukua ni ya Kipumbavu........kumbuka mzee wa VIJSENTI amesema.........wewe hukuzaliwa kuwa Waziri........na huu ndio ulikuwa mtihani wako mzuri kuonyesha kwamba wewe ni tofauti na majuza waliopita ku-approach masuala kama haya.
Chuo Kikuu sio shule ya msingi kusema watu wote wanaingia madarasani masaa yanayofanana........kuna watu wanafanya research....kuna wengine siku hiyo hawana darasa.......in short masaa ya wanfunzi chuoni hutofautiana.........wewe unatoa amri kufikia saa fulani wote muwe darasani.....kwani imekuwa shule ya msingi Rufiji ile.......damn!
Wanafunzi wana matatizo yao...hatukatai.....vile vile wana haki zao..........yaani NYIE MIJITU MLIO NA MIWAZO ISIYOBADILIKA BADO MNAFIKIRIA ENZI ZA CHAMA KIMOJA..........amri amri..........ni hatari na wa kuogopwa kama UKOMA
Shame on You......Maghembe
Nyani, alipoteuliwa kuwa Waziri wa Elimu ya Juu miongoni mwa mambo ya kwanza ambayo angetakiwa kushughulikia ni suala la Mlimani. Ni rahisi kutumia nguvu kuliko kutumia akili!
Nadhani wakati mwingine sisi tulioko kwenye sidelines ni rahisi kukosoa na kusema mtu afanye hivi au vile au angefanya hivi au vile. It may no be that easy. Put your self in his shoes and walk a mile....then probably you'll see how difficult it is. Kila mtu anaweza kukosoa....kutenda ni jambo jingine...
tusiwe na majibu rahisi kama Kikwete alipokuwa anajaribu kuiponda filamu ya Hauper maarufu kama "mapanki" aliposema ukahaba uko dunina nzima. Mimi sihalalishi wanafunzi kupigwa marungu wala mkandara kuwa fisadi, hoja yangu hapa tupunguze ushabiki kwenye mambo yanayogusa uhai wa taifa letu.
kama hata Havard kuna digrii za "chupi" jee sababu zake zinafanana vyanzo vyake na za hapa kwetu? wanafunzi wetu naamini kabisa wana mambo yanayofanana hata na vyuo vingine vikuu duniani,lakini vyanzo vyake ni vilevile?
Na Watashitakiwa Kama Watu Huru Na Sio Kama Wanafunzi Wa Udsm
Na Watashitakiwa Kama Watu Huru Na Sio Kama Wanafunzi Wa Udsm
Maghembe mnamuonea bure tu. Hata ingekuwa wewe tatizo hili lingekuwepo. Kuweni fair kidogo ktk ukosoaji wenu
Katika maelezo yake, Prof Maghembe alisema kuwa wanafunzi hao wametimuliwa baada ya kukaidi amri ya uongozi wa chuo iliyowataka warejee madarasani.
Nadhani wakati mwingine sisi tulioko kwenye sidelines ni rahisi kukosoa na kusema mtu afanye hivi au vile au angefanya hivi au vile. It may no be that easy. Put your self in his shoes and walk a mile....then probably you'll see how difficult it is. Kila mtu anaweza kukosoa....kutenda ni jambo jingine...
Tangu lini mwanafunzi wa Chuo Kikuu anaamuriwa kuingia darasani? Halafu unamfukuza kwa kutokuingia darasani? Kama uprofesa ni huu, nashukuru mungu sikuzigusa hizo anga tukufu nikabakia fundi mchundo.
Chuo Kikuu gani ambacho hakina wavuta bangi? Clinton alivuta, Obama alitumia mpaka cocaine inasema george W naye haukwa nyuma kwenye haya masuala! Wangapi tumewaona wakitumia hayo majani wakati wa ujana wao na sasa ni viongozi wa kuaminika dunia nzima? Chuo Kikuu kinazuia kubusiana wanafunzi! Hiki ni Chuo Kikuu au shule ya msingi? Ni lazima tuanze kuwa'treat' wanafunzi wa Chuo kikuu kama watu wazima na kuwapa heshima wanayozstahili. Ni lazima tuanze kuheshimu sacrifice na gharama ambayo jamii imeingia kumfikisha huyo mwanafunzi mahali pale. Ni lazima tuanze kutambua kuwa pale na sehemu nyingine kama zile ndiyo font ya vichwa vyetu vya baadae na ni lazima tuwape uhuru wa kutafakhari na kudadisi mambo bila kuwaingilia. Wakitoka hapo, dunia itawaweka sawa lakini wakati wako pale waachiwe waweze kufikia their full potential.