Serikali yasitisha masomo kwa vyuo vya kati na vyuo vikuu kuanzia tarehe 18/03/2020 ili kupambana na Corona

hamis77

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,642
19,018
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesitisha masomo kwa vyuo vikuu na vya kati nchini kuanzia leo March 18, 2020 ili kujikinga na virusi vya Corona, waliofunga wametakiwa kutorudi vyuoni “vyuo vya ualimu vilitakiwa kufanya Mitihani mwezi May, Waziri afanye marekebishisho ya ratiba yao”

















========
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa walikuwa wamesitisha masomo kwa shule za awali, msingi na sekondari zote nchini.

Lakini leo serikali imeongeza kusitisha masomo kwa vyuo vya kati na vyuo vukuu vyote nchini.

"Sasa leo tunaendelea kuongeza vyuo vya elimu ya kati na vyuo vikuu vyote nchini, navyo pia tunasitisha kuendelea na masomo.

Tunatambua vyuo vikuu wanafunzi wengi wako likizo na sasa tunawataka kutokurudi kwenye vyuo vyao, na wale wachache waliokuwa wamebaki kwa ajili ya mitihani nao waondoke mara moja ili kuondoa misongamano kwenye maeneo hayo ya vyuo.

Tunavyo zungumzia vyuo vya kati tunazungumzia vyuo vya ufundi na vyuo vya ualimu, tunatambua wanafunzi wa vyuo vya ualimu walitarajia kufanya mitihani mwezi mei mwaka huu, namwagiza waziri wa elimu kufanya marekebisho kwenye mihula yao, kama ambavyo tulimtaka kufanya marekebisho kwenye mihula ya shule za sekondari kidato cha sita."
 
Hapa ndipo naona, Kuna Jambo kubwa ambalo Bado hatujaambiwa na wasemaji. Hatua zingechukulia asubuhi na mapema, kwa ku quarantine wanaotoka nje, pengine leo kusingekuwa na haja ya kufunga Shule na Vyuo.

Ila kwakuwa tumetiwa pamba na matambala mdomoni, hakuna wakuwakumbusha wasemaji na watoa maelekezo. *Mungu iponye Tanzania yangu*

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wangefunga mipaka ya nchi kwanza.....kufunga shule na colleges naona nikama ku overate covid 19, hapa kwetu kwanza naona wanafunzi wako salama kubaki mashuleni, kuliko kuwaruhusu wazurule mitaani na kuchangamana na watu wengi......

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisa, sijui viongozi wanafeli wapi....yaan wameover-react na kuiover-rate Corona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom