Bajeti kuu, 2023-2024: Mapendekezo ya kufutwa kwa ada kwa wanafunzi wa kidato cha nne wanaopangiwa vyuo vya kati

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,116
Waziri wa fedha, Mwigulu Nchema amesema bajeti inapendekeza kuondolewa kwa ada kwa wanafunzi wanaopangiwa vyuo vya kati na Serikali wakimaliza kidato cha nne, vyuo hivyo ni, DIT, MUST na AITC.

Waziri wa fedha amesema serikali imefikia uamuzi huo ili kuzalisha wataalamu wengi wa fani mbalimbali.

Kumekuwepo na mjadala hapa JamiiForums.com kuhusu wanafunzi wanaopangiwa vyuo na serikali kwend akusoma ufundi kuwa gharama inakuwa kubwa kwa wazazi kwani walitakiwa kuwalipia ada watoto wao katika vyo ivyo ambavyo wamepangiwa na srikali.

=====
Waziri wa Fedha na Mipango amependekeza kuondolewa Ada kwa Wanafunzi waliomaliza kidato cha 4 na kupangiwa kujiunga na Vyuo Vikuu vya DIT, MUST na Arusha Tech kwa lengo la kuongeza idadi ya Wataalamu wenye ujuzi unaohitajika katika azma hizi za Mapinduzi ya 4 ya Viwanda.

Amependekeza kuanzishwa kwa Programu ya Mikopo kwa Wanafunzi wanaochaguliwa na Serikali kujiunga na Vyuo vya Kati vya Elimu katika Fani za Kipaumbele ambazo ni Sayansi, Afya, Ufundi na Ualimu ili kuaanza na Wanafunzi wa Mwaka wa kwanza wa masomo kwa mwaka 2023/24.

Aidha, Serikali imeendelea kutenga Fedha kwa ajili ya kugharamia Programu ya Elimumsingi na Sekondari Bila Ada ambapo hadi Aprili 2023 jumla ya Tsh. bilioni 661.9 zimetolewa.


Moja ya mjadala wa kutaka kufutwa kwa ada
: DOKEZO - Hii biashara ya serikali na vyuo vya elimu vya kati mnayofanya bomu lake linakuja
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba leo June 15,2023 amewasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 Bungeni Jijini Dodoma ambapo moja ya mambo aliyoyapendekeza kwenye hotuba yake ni kuondolewa ada kwa Wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne na kupangiwa na Serikali kujiunga na Vyuo vya Ufundi vya Dar es Salaam Institute of Technology (DIT), Mbeya University of Science and Technology (MUST) na Arusha Technical College (ATC).

“Hatua hii inalenga kuongeza idadi ya Wataalamu wenye ujuzi na elimu inayohitajika katika zama hizi za mapinduzi ya nne ya viwanda (4th Industrial Revolution), MAMA yuko Kazini!”
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba leo June 15,2023 amewasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 Bungeni Jijini Dodoma ambapo moja ya mambo aliyoyapendekeza kwenye hotuba yake ni kuondolewa
Subiri sasa kodi wanayokamliwa wazazi. Ni zaidi ya hiyo ya ada.
 
Kumbe hata hayati j.pm alikataa kujengwa bandari bagamoyo. Kutokana na mashariki mabovu ya mikataba. Na wakati huu mama Samia alikua makamo wake kwahiyo Hilo sio geni kwake. Ila wameamua Tu makusudi Kwa masilai ya wachache. Kusamehe hada ya vyuo nikitu kidogo. Ila kuchezea Nchi atukubari kuna Haja ya watanzania kuamka na Sasa kusema basi. Maana wameona wakimbilie Kwa viongozi wa dini Kwa sababu wanasikilizwa na wananchi. Wameenda kuwashika msikio. Sisi tunataka uwazi wa mkataba na useme unaanza lini na kuisha lini. Na utakua na manufaa gani Kwa Taifa. Kwa Leo na siku zijazo. Mama umejishushia heshima Sana Kwa watanzania. Tunasubiri uchaguzi. Hakika huta pata Kura yangu.
 
Back
Top Bottom