Serikali ya Japan yatoa mwongozo mpya kuhusu matumizi ya Akili bandia (Artificial intelligence) kwa vyuo vikuu

SNAP J

JF-Expert Member
Dec 26, 2013
7,079
7,976
Mapema mwezi huu, Serikali ya Japan ilitangaza mwongozo mpya kuhusu matumizi ya akili bandia (artificial intelligence -AI) kwa vyuo vikuu, ikilenga;
kusaidia walimu na wanafunzi kuelewa sifa za teknolojia hiyo, wakati pia ikaweka vizuizi kadhaa kutokana na hofu ya uvunjaji wa hakimiliki, kuvuja kwa taarifa za kibinafsi, na udanganyifu wa kazi za wanafunzi (plagiarism).

Mwongozo huo ambao unafafanua wazi kuwa ni makosa kwa wanafunzi kuandika ripoti, insha au kazi nyingine zilizoandaliwa na AI na kudai kuwa ni kazi zao mwenyewe.

Waziri wa elimu nchini humo Keiko Nagaoka alisema wakati wa uzinduzi wa muongozo huo mpya, serikali kupitia wizara ya elimu na vyou vikuu wanashauriwa kutumia 'generative automated writing systems AI', kama Chat GPT kwa umakini na tahadhari ya hali ya juu.

Hali kadhalika, katika muongozo huo mpya, walimu wanahimizwa kuachana na utamaduni wa zamani wa utunzi wa mitihani au uandishi wa ripoti ambazo zinaweza kufanywa kwa urahisi kwa kutumia akili bandia.

Kutokana na matumizi makubwa ya akili bandia kwa sasa nchini humo, umeibuka wasiwasi mkubwa miongoni mwa walimu, hasa wa elimu ya juu, kuhusu hatma za wanafunzi ambao hawataweza kujijengea uwezo wa kufikiri au kuwasilisha mawazo yao endapo kama akili bandia (generative AI, kama Chat GPT) itatumika visivyo na wanafunzi.


Hali kadhalika, Umoja wa vyuo vikuu vya Japan umevitaka vyuo vikuu vyote nchini humo kuhumiza matumizi chanya ya akili bandia, na sio hasi, ambayo yanaweza kupelekea kuporomoka kwa viwango vya elmu.

Kwa sasa tafiti mbali mbali zilizochapishwa zinaonyesha kuongezeka kwa matumizi yaliyikidhiri ya akili bandia hata katika uandishi wa tafiti ( writing of academic papers) miongoni mwa wanavyuo.

Mfano, mwezi Juni uliopita, vyombo vya habari nchini humo viliripoti matokeo ya utafiti wa matumizi ya AI ulioongozwa na Chuo Kikuu cha Tokyo ambao ulihusisha wanafunzi wa vyuo vikuu wapatao 4,000 wa shahada ya kwanza, ulibaini ya kuwa karibu theluthi moja ya wanafunzi hao wameshawahi tumia ChatGPT.

Asilimia 91 ya wanafunzi hao waliripoti kutegemea ChatGPT kuthibitisha na kusahihisha majibu yao kwenye kazi za masomo, huku zaidi ya asilimia 85 wakitumia AI kuhariri sentensi na mawazo yao wenyewe katika maswali wapewayo vyuoni.

Waziri wa elimu alimalizia kwa kusema ya kuwa muongozo huo utakuwa ukiboreshwa kulingana na ukuaji wa teknolojia na matokeo ya tafiti juu adhari zitokanazo na matumizi ya akili bandia nchini humo kadiri muda unavyoenda.

Rai yangu: ni wakati kwa Serikali ya Tanzania, kupitia wizara ya elimu , sayansi na teknolojia kuanza kutizama haya mambo ili tusije kumbuka shuka wakati kumeshapambazuka
 
Muhimu jinsi ambavyo wanafunzi watakavyotumia mfano kupata idea au kuingiza mawazo yake kisha kuyaingiza mle kuboresha zaidi , wale wa kukopi na kupaste ndio wapo katika njia mbaya.
 
Computer lab pale Chuo cha uhasibu nilitumia nusu ya muhula nikiwa humo tulikua watu wa google darasa zima cpat picha AI Iingekuepo
 
Back
Top Bottom