Serikali yasitisha mafunzo ya JKT

Serikali yasitisha mafunzo ya JKT

Ushenzi unaofanyika huko sitaki hata siku moja kusikia mwanangu au mdogo wangu wa kike aende huko.

Mimi nilisha apa mwanangu hawezi kwenda jkt labda kama niwe nimekufa.

Mafunzo ya jkt hayana faida yoyote zaidi ya kuiongezea serikali gharama ya matumizi. Kuunga mkono mafunzo ya jkt ni kusema kwamba huna akili,ni taahira.

Nilishawahi kuuliza humu watu wanitajie faida za jkt kwa uchumi wa nchi nikakosa majibu. Watu wakabaki kusema eti yanawafanya vijana wawe wakakamavu tu,hilo tu. Hakuna maarifa yoyote ya kukabiliana na changamoto za maisha wanazopewa zaidi ya matumizi ya siraha.
 
Wakitoka huko baada ya mateso bila ajira ndo hao unasikia panya road hizo pesa za kugharamia hayo mafunzo bora wangezingea maabara.
 
Tatizo hili nchi limekuwa la kifwara sana kila kitu tunashindwaga tu.BORA TUTAWALIWE NA WAKOLONI WA KIZUNGU.
 
hii tabia ya kuwapeleka vijana jeshini then wanakosa ajira ndio mwanzo wa kutuzalishia majambazi
 
Hivi wakiwa mafunzoni hawazalishi? Kama wanazalisha ni kwa ajili ya nani, na kama hawazalishi haina maana kutumia pesa kuwaweka makambini. Hiyo pesa ingeenda kwenye shule, vyuo na hosipitali.
 
Kwa hiyo ndio imefutwa yani

Uzalendo wetu mbona siuoni,zaidi ya chenja na vimisamiati vya Jakata

Anyway..wonders shall never end in Tanzania
 
.....mwl Nyerere alikufa na ndoto zake bwana....yote misingi ya taifa waliocha inakwenda na maji
 
Hv kumbe na huko walikuwa wanalipia ada? Mi nilijua ni bure.

Bure, nini maana ya bure ? Ina maana hakuna gharama katika kuendesha hiyo kitu, uwaweke watu wengi katika makambi, halafu useme hakuna gharama yoyote kwa taifa !!!!
 
ya hani ndio wanastuka sasa wanasitisha .vijana unawapa mafunzo makali unakuja kuwaweka mtaani.nyie mlitegemea nini kila aina ya silaa anaijua.
 
Serikal ijipange upya kwa hili, ukata ni kisingizio tu, there is hiden reason nyuma ya hili
 
Hatari iliyopo ni hawa vijana wanapoenda kufanya migomo na maandamano vyuoni unategemea polisi hawahawa wakawazuie.
 
Back
Top Bottom