Serikali yasitisha mafunzo ya JKT

Serikali yasitisha mafunzo ya JKT

Tuesday, January 27, 2015



jkt3-640x360.jpg

Baadhi ya vijana wanaochukua mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
Serikali imesitisha mafunzo ya JKT kwa mwaka huu. Kwa hiyo wale vijana waliokua wanategemea kuanza mafunzo hayo mwezi wa pili (tano) mwaka huu, mafunzo hayo hayatakuwepo tena.

jkt1-640x360.jpg

Wahitimu mafunzo ya awali ya kijeshi kenye kambi ya JKT Ruvu kikosi cha singe wakiwa katika maonyesho ya kivita kwenye sherehe za kuhitimu mafunzo hayo
Sababu ya kusitisha mafunzo hayo ni ukata unaoikabili serikali.

jkt-600x360.jpg

Vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika Kikosi cha Ruvu, Kibaha, mkoani Pwani kwa mujibu wa sheria wakionyesha umahiri wao wa kuruka moto


Chanzo: Gazeti la Jamhuri
 
Wazabuni wamegoma!hivi JKT si kwa mujibu wa sheria inakuwaje isitishwe ghafla ghafla.
 
bora wamehairisha ila serikali yetu haieleweki muda wowote utasikia waende!
 
Siyo kuwa serikali haina pesa, bali ni matokeo ya kuwa na priorities mbovu tu. Kupoteza pesa nyingi sana kwenye bunge la Katiba ilihali ikishajulikana wazi kuwa litafanya nini ilikuwa ni uamuzu mmojawapo wa kijinga sana. Tunayo maamuzi mengi ya kijinga mabayo serikali yetu hufanya ili kuhalalisha matumizi hovyo ya hela yasiyokuwa na tija.
 
Ni sababu ya ukata kweli wamesitisha mafunzo haya au wameogopa kuongeza idadi wanajeshi wa akiba uraiani kipindi hiki ?!
 
Kila kitu serikali ya ccm huwa inashindwa,hii ni laana
 
Eti kwa ajili ya uzalendo,hakuna ni ujinga tu wa serikali. Uzalendo ni tabia ya mtu. Uzalendo sio mafunzo,mbona hao hao akina Lowasa,Kikkwete,Shimbo,Chenge nk wamepitia JKT na wengine walikuwa maafisa wa jeshi(kikwete na Lowasa) ndio majizi papa hapa nchini. Tusidanganyane hapa,hakuna cha uzalendo wala nini bali ni serikali ya kipuuzi na dhaifu iliyoshindwa kusimamia sheria na kanuni mbalimbali kukamata wezi na kuwafungulia mashitaka.
 
walikuwa wanafanya mambo ya ajabu sana mtu mnahangaisha kwenda JKT halafu akitoka huko eti unamwambia Amekosa mkopo!! Sasa hiyo hela unayopotezea JKT Si ungeongezea Loan Board???

Hv kumbe na huko walikuwa wanalipia ada? Mi nilijua ni bure.
 
Back
Top Bottom