Serikali yasitisha mafunzo ya JKT

Serikali yasitisha mafunzo ya JKT


jirani yangu kamaliza form 6 kaingia huko, baada ya mafunzo kapewa ahadi hewa ya ajira, sasa hivi amejiajiri kwa mafunzo husika mtaani watu wanaibiwa mchana kweupe.

Juzi huko Tanga Polisi wa pikipiki wamenyanganywa SMG mbili na risasi kadhaa baada ya kuchapwa makofi ya kutosha sana na wababe hao walifanya shughuli hiyo wakiwa na kisu tuu.
Nadhani hao watakuwa wale waliopelekwa JKT kwa mujibu wa sheria lakini wameshindwa kwenda vyuoni kwa vile Bodi ya mikopo imewaambia haina pesa na bahati mbaya familia zao hazina uwezo. Sasa wanatumia mafunzo yao kujikimu.
 
Hakuna wakati ambao mafunzo ya JKT yanahitajika sana kama wakati huu.
Ni vyema ukatumika utaratibu wa kuunda mfuko maalum kwa ajiri ya JKT na wachangiaji wakubwa wakiwa ni JKT yenyewe,makampuni ya ulinzi na mashirika mbali mbali ya umma na binafsi.
 
Wawapeleke tu watatusaidia mbeleni kuichomoa ccm ikulu
 
binafsi naona kama ndio chanzo cha ujambazi kwani vijana wengi wakihitimu mafunzo hayo hubaki uswahilini huku wenzao wachache wakipata minoti ya ajira kunako jwtz hivyo huchochea nawao wapate faida ya mafunzo yao mi ningeomba serikali ichukue vijana wachache ambao wakihitimu wapate ajira kabisa kuwa na vijana wengi ambao mwisho wake huachwa bila ajira
 
mm naona wangesitisha hata miaka 5 mbona wanajeshi ni wengi sana harafu hawana kazi kazi yao ni kuvuta bangi na kunywa pombe na kupiga watu bila sababu za msingi

Kauli yako mbaya sana. Siku tukikutia nguvuni . nadhani utaulaumu Ulimi wako.
 
Mmeongea mengi yasiyo na mashiko kwa hofu ya wanenu eti wanatendewa mabaya wawapo jkt! mmeona ni bora kuikashifu jakata kuliko kuwaonya wanenu WA kizazi hiki cha wasapu ambao wamekuwa no kero huko kwenu.Ukweli ni hivi licha ya uhaba WA ajira jkt imeweza kupunguza takwimu ya watu wasio na ajira kupitia askari kuajiliwa na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama kama jwtz,polis,magereza,bandari,fire,tanapa,migration na usalama WA taifa.
Kwa miaka miwili2013 na 2012 vijana takrobani elfu Tisa walipata mafunZo ya awali ya kijeshi kupitia vikosi mbali mbali vya jkt Tanzania, mpaka hivi sasa zaidi ya nusu yao wamepatiwa ajira na huku baadhi yao waliobaki nao wakisubiri zali lao ,Mimi ni mmoja wapo nilikuwa821 kj nikamaliza nikapelekwa makutu nikavaa baka ,nikapangiwa tena pale pale 821 kiumeni kama mkufunzi,tanx God mkono unaenda kinywani .Hivi unajua ni kwa jinsi gani majeshi yanavyolipa vizuri nw dayz Endeleeni kuisimanga jkt kwa masimulizi ya uongo yaliyoletwa uraiani na watoto wenu waliokaa jkt miezi mitatu huku wakiishia kumwagilia bustani tu,lakini wamelichafua jakata vilivyo ,Kwa atakayehitaji maelezo anichek 0752215730
 
Nyie nani kasema kuwa mafunzo ya ahirishwa msikurupuke kutoa tarifa tupe source ya habari ako kuweni makini bhna Jf ni mtandao mkubwa oooh
 
Mm yangu hii
 

Attachments

  • 1422479350161.jpg
    1422479350161.jpg
    56.7 KB · Views: 324
naona umepakua logo ya jkt ukaamua kutunga kwamba hayajasitishwa.
 
ukiwa Jkt utaichukia ila utakapo toka au maliza mafunzo hakika ukija uraiani utaona imekubadilisha sana
 
Serikali imefilisika kweli, ndio maana imeshindwa kulipa pesa za wakulima wa mahindi kule Ruvuma na kwingineko ni billion 85 tu kwa nchi nzima, wakati mtu binafsi kama Lugemalila alichukua za escrow zaidi ya billion 70, huu ni upuuzi kweli.
 

Maoni yangu:

Mafunzo haya ya JKT yapigwe marufuku kabisa na yafutwe maana hayana faida yoyote wala tija katikaTaifa hili. Binafsi natamani serikali ifilisike kabisa ili isiweze kufadhili mafunzo hata tena.



una uwelewa mdogo kuhusu kodi, serikali haiwezi kufilisika labda wewe usinunue hata chumvi, kishikizo cha shati wala kupanda daladala hata siku moja, maana serikali inapata pesa zake wewe unaponunua kitu au huduma yoyote. Serikali inaweza kuwa na matumizi mabaya tu ya fedha lakini sio kukosa fedha.
 
Juzi huko Tanga Polisi wa pikipiki wamenyanganywa SMG mbili na risasi kadhaa baada ya kuchapwa makofi ya kutosha sana na wababe hao walifanya shughuli hiyo wakiwa na kisu tuu.
Nadhani hao watakuwa wale waliopelekwa JKT kwa mujibu wa sheria lakini wameshindwa kwenda vyuoni kwa vile Bodi ya mikopo imewaambia haina pesa na bahati mbaya familia zao hazina uwezo. Sasa wanatumia mafunezo yao kujikimu.


miaka ya nyuma nchi nzima ilienda jeshini tena mwaka mzima !
 
binafsi naona kama ndio chanzo cha ujambazi kwani vijana wengi wakihitimu mafunzo hayo hubaki uswahilini huku wenzao wachache wakipata minoti ya ajira kunako jwtz hivyo huchochea nawao wapate faida ya mafunzo yao mi ningeomba serikali ichukue vijana wachache ambao wakihitimu wapate ajira kabisa kuwa na vijana wengi ambao mwisho wake huachwa bila ajira

Jkt sio taasisi ya ajira bali ni chombo kinachochukua vijana kutoka sehemu zote nchini na kuwapa mafunzo ya kujitegemea, ukakamavu na nidhamu, suala la vijana kutokuwa na ajira sio lawama kwa jkt kwamba imeshindwa kuwaajiri bali watu hawajui sababu za kuundwa kwa jkt. Nashauri serikali iendelee kuwachukua vijana ila kwa kupunguza idadi tofauti na awamu zilizopita kwani kwa kuyasitisha kwa ghafla mafunzo hayo ni kuwakosea heshima vijana wanaotaka kwenda huko ambao unakuta kijana alijaribu mara kadhaa nyuma akakosa, serikali mwushoni mwa mwaka jana au mwezi huu mwanzoni ilitoa taarifa kwa vijana kuhusu namna ya kujiunga na jkt. Sasa kwa kusitisha kwa ghafla hivi haioni kuwa inachanganya saikolojia ya vijana na kuongeza tatizo wanalodhani wamelipunguza?
Kwa hili serikali imekurupuka, ilitakuwa itoe taarifa mapema mwaka mmoja au miwili nyuma kwamba mwaka huu hakutakuwa na mafunzo ya jkt ili watu wajipange upya.
 
Mm nasikitika sana naombea asilimia angalau 60 ya vijana wote wapite jeshi hii nchi ndio ingekaa sawa haya mambo ya kuleteana porojo na kuongozwa kisiasa mbona yangeisha.

Hawa polisi na ccm yao wangekuwa washasalender siku nyingi sana mbona
 
Back
Top Bottom