Shida ya serikali yetu ni kufanya kazi kama ¬`Fire Department¬¬ yani kuibuka tu na kuanzisha kitu kama ¬¬reaction¬¬ ya jambo jingine. mambo mengi yanayoanzishwa na serikali yetu yanaishia au kutumia tu hela za watanzania, au kufutwa kwa vile inagundulika kuwa hayana tija kwa taifa. Tukumbuke tu mkakati wa kilimo kwanza ulivyaokuja kwa kasi na kuwafanya wananchi waamini kuwa kilimo ndio mkombozi wa maisha yao. Tutakumbuka kuwa serikali imetumia fedha nyingi sana kutoa kwa wananchi ili ziwasaidie kuboresha kilimo. Lakini tunachoshuhudia sasa, ni uzalishwaji mkubwa wa mahindi wakati hakuna soko. Uhalisia ule ule wa hali ya serikali unawakumba wananchi, kwani wanatumia gharama kubwa kuzalisha mazao ambayo hayawapi tija. Najiuliza, serikali haikuweza kufikiria kuandaa soko la uhakika la mazao ambayo yameongezewa uwezo ili kuboresha uzalishaji? Sasa mahindi ya wakulima yanaozea magurioni, au wengine wamekopwa na serikali hadi sasa hawajalipwa, na hao ni wananchi ambao wanategemea kilimo ili wasomeshe watoto, wanunue pembejeo mpya za kilimo na wajikimu katika maisha yao. Najiuliza, kama kweli kulikuwa na mikakati madhubuti ya kuboresha kilimo, kwanini nyanda za juu kusini mikoa kama ile ya Mbeya Njombe, Iringa na Ruvuma ambako kunazalishwa mahindi kwa wingi hakuna kiwanda kilichojengwa cha kuzalisha sembe? Soko la mahindi linapungua kwa sababu zao lenyewe halijaboreshwa. Baadala ya kuuza mahindi watu walitegemea kuona sokoni mazao ya mahindi, ambayo kiuhalisia yangeingia katika soko la ndani ya Tanzania na hata masoko ya nje, kama tungeongeza ubora.
Naunganisha suala hili na lile la kufutwa kwa JKT kwa hoja ya kwamba, bila shaka serikali iliamua kurudisha tena JKT kwa ilipata ushauri toka upande fulani, na sio kwa sababu iliona hitaji hilo. Pengine hata fungu lilitoka mahala fulani, ndio maana lilipoisha ikabidi kufuta JKT. Je hatuoni kama tumesababisha usumbufu mkubwa kwa vijana poezawetu na kuwapotezea muda bila sababu? Tujipange watanzania, ili tuje kuwapata viongozi ambao watakuwa na mwono stahiki ¬¬ Mission¬¬ ambao watakuwa na mikakati mathubuti``Strategic Leaders`` ambao watakuwa ``proactive`` na sio ``reactive`` watakaoweza kuona mbali na kuzuia madhara yasitokee na siyo kusubiri yatokee kisha kuhangaika kutafuta mbinu ya kuyazuia. Ni sisi watanzana tutaibadili nchi yetu tukiwa makini katika kuwahakiki watu tunaowapa madaraka. Pamoja sana ndugu zangu katika kutetea maslahi ya taifa letu.