Serikali yashindwa kulipa mishahara mwezi Mei

Serikali yashindwa kulipa mishahara mwezi Mei

Status
Not open for further replies.

mumagoma

Senior Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
186
Reaction score
95
Kwa taarifa nilizopata toka vyanzo vya ndani hazina ni kwamba mpaka sasa asilimia kubwa kama si wote wanaolipwa kutokea hazina hawajalipwa mishahara yao. Na hii inatokana na serikali kutokuwa na hela mpaka Jana za kutosha kulipa mishahara.

Fedha ambazo zilitengwa kwa ajili ya kulipa mishahara zimelipwa kwa wanafunzi kama bumu yao ili wasikose kura za wanachuo maana mgomo wao ulishaanza kusambaa nchi nzima na hyo ingeathiri uchaguzi wa Oktoba kwa CCM.

Pia inasemekana naibu Waziri wa Fedha anataka kupiga kupata hela ya kampeni.


Kuna tetesi ati kuwa mshahara umetoka, jamani nithibitishieni nipo kijijini kwenda mpaka mjini nauli 30000/= kwenda tu bado kulala geust na nauli ya kurudia.

Mshahara wangu ni laki nne kasoro mimi mwalimu shule ya msingi!


 
Ni Kweli nimethibitisha hilo kwenye vitabu kutoka hazina kuwa mshahara umefika leo kwa halmashauri ya Meru ila cna uhakika km zimeshawekwa bank so kwenye jtatu Mambo yanaweza kuwa yamekamilika mkuu all the best!
 
Kurahisisha maisha juinge na SIM banking, nadhani NMB wanayo.CRDB for sure wanayo
 
jiunge na huduma za kibenki kwa njia ya simu ya mkononi uwe unapata taarifa.
 
Kwa taarifa nilizopata toka vyanzo vya ndani hazina ni kwamba mpaka sasa asilimia kubwa kama si wote wanaolipwa kutokea hazina hawajalipwa mishahara yao. Na hii inatokana na serikali kutokuwa na hela mpaka Jana za kutosha kulipa mishahara.

Fedha ambazo zilitengwa kwa ajili ya kulipa mishahara zimelipwa kwa wanafunzi kama bumu yao ili wasikose kura za wanachuo maana mgomo wao ulishaanza kusambaa nchi nzima na hyo ingeathiri uchaguzi wa Oktoba kwa CCM. Pia inasemekana naibu Waziri wa fedha anataka kupiga kupata hela ya kampeni.
 
Kama kupoteza kura walishapoteza zamani, you can't 'cheat/trick', hawa watoto wa chuo siku hizi.

Sasa ngoja uje uone watu watakavyokuwa slow huko kazini wakiichelewesha zaidi hiyo mishahara. Halafu ndiyo wanawasubiri vizuri October.
 
Shark;

Mkuu you might be right, Jana usiku kipindi cha Bunge, nilimsikia Mh. Joseph Mbilinyi aka Sugu Waziri Kivuli wa Habari vijana na michezo, akisema kwamba Watumishi wote wa serikali na Taaisisi zake hadi jana walikuwa hawajalipwa mishahara yao.

Hakuna waziri aliyekanusha taarifa hiyo Sugu, kuashiria kwamba ilikuwa kweli. Kama hii serikali imeanza kuchechemea kulipa mishahara ya wafanyakazi wake May, Je ikifika Mwezi September na October kweli itaweza kulipa mishahara ya Wafanyakazi wake.

I can see mambo yakizidi kuwa mabaya kadri tunavyoikaribia October 2015
 
Last edited by a moderator:
Bobuk hii nchi acha tu ila wacha wamalizie kipindi chao kabla UKAWA hawajachukua nchi
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom