Serikali yashinda rufaa, Wakurugenzi kuendelea kusimamia chaguzi

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Serikali imeshinda rufaa dhidi ya kesi iliyofunguliwa na Bob Wangwe kupinga wakurugenzi Kusimamia uchaguzi.

Mahakama ya Rufani imetengua hukumu na amri ya Mahakama Kuu kuzuia wakurugenzi wa halmashauri, manispaa, na majiji kusimamia uchaguzi mkuu kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Mahakama ya rufaa imefikia maamuzi baada ya kujiridhisha na hoja za serikali kuwa wakurugenzi hao kabla ya kuwa wasimamizi wa uchaguzi hula viapo vya kukana uanachama wao.

HUKUMU:

NYARAKA: Hukumu ya Mahakama ya Rufaa kuruhusu Wakurugenzi kusimamia Uchaguzi Mkuu

Pia soma

Serikali yabwagwa Mahakamani kesi ya kuzuia Wakurugenzi kusimamia uchaguzi

Mahakama Kuu yabatilisha Vifungu vya Sheria vinavyowapa mamlaka Wakurugenzi kusimamia Uchaguzi

Serikali kukata rufaa hukumu ya kuzuia Wakurugenzi wa Halmashauri na Jiji kusimamia uchaguzi

Baadhi ya mijadala ndani ya JamiiForums:

2016
Hatutaki wakurugenzi wasimamie uchaguzi 2020

Julai 2018:
LHRC: Asilimia 80 ya Wakurugenzi wa Halamashauri wanaopaswa kusimamia uchaguzi waliwahi kugombea uongozi kupitia CCM

NEC wenyewe walishaona haya:

NEC yatahadharisha Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi kutojihusisha na siasa maeneo ya uchaguzi wa marudio

2016
Madhara ya kuteua makada kwenye nafasi za Ukurugenzi wa Halmashauri

2014
Uchaguzi Serikali za Mitaa: Wakurugenzi waendeleza rafu

==========

Dar es Salaam. Mahakama ya Rufani nchini Tanzania imetengua hukumu na amri ya Mahakama Kuu ya kuzuia wakurugenzi wa halmashauri, manispaa na majiji kusimamia Uchaguzi Mkuu kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano Oktoba 16, 2019 na Mahakama hiyo. Kwa maana hiyo wakurugenzi wanaruhusiwa kusimamia uchaguzi.

Serikali ya Tanzania iliamua kukata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu kuwazuia Wakurugenzi hao kusimamia uchaguzi.

Uamuzi huo ulitokana na Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyotolewa na jopo la majaji watatu, Dk Atuganile Ngwala, Dk Benhajj Masoud na Firmin Matogolo ilibatilisha kifungu cha 7(1) cha Sheria ya Uchaguzi kinachoipa mamlaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwateua wakurugenzi wa majiji, manispaa na miji kuwa wasimamizi wa uchaguzi.

Pia ilibatilisha kifungu cha 7(3) kinachoipa NEC mamlaka ya kuteua mtu yeyote miongoni mwa watumishi wa umma kuwa msimamizi wa uchaguzi.

Katika hukumu hiyo mahakama hiyo ilisema kwamba vifungu hivyo ni kinyume cha Katiba ya nchi ikibainisha kuwa wakurugenzi hao huteuliwa na Rais aliyeko madarakani ambaye hutokana na chama tawala na kwamba wengine ni wanachama wa chama cha mamlaka inayowateua jambo ambalo huathiri utendaji wao katika kutenda haki.

Pia ilisema kwamba sheria haijaweka ulinzi kwa NEC kumteua mtumishi yeyote wa umma kuhakikisha kuwa anakuwa huru katika kutekeleza majukumu yake.

Uamuzi huo wa Mahakama Kuu umetokana na kesi iliyofunguliwa na mashirika kadhaa ya wanaharakati kupitia kwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bob Wangwe, akitetewa na Wakili Fatma Karume.

Mahakama Kuu imesikiliza maombi ya ACT- Wazalendo kujiunga katika kesi ya ukomo wa urais. Uamuzi wa ama wataruhusiwa au la utatolewa Oktoba 24, 2019.
 
Rekebisha andiko lako na lisomeke kuwa "Mahakama imesaidia wanainchi kutuma salaam kwa serikali na Mbowe na Zitto wadondokea pua" nashangaa watu wazima kwanini hawajieleiwi au pesa za uchaguzi wanazopewa kwa ajili ya uchaguzi kwao ni muhimu kuliko kupigania Tume huru na Katiba mpya?
hebu elekeza hapa wapiganiaje tume huru??
 
Serikali imeshinda rufaa dhidi ya kesi iliyofunguliwa na Bob Wangwe kupinga wakurugenzi Kusimamia uchaguzi.

Mahakama ya rufaa imefikia maamuzi baada ya kujiridhisha na hoja za serikali kuwa wakurugenzi hao kabla ya kuwa wasimamizi wa uchaguzi hula viapo vya kukana uanachama wao.
Safi Sana !kiapo kinakubalika kisheria, haohao wakurugenzi mbona waliwapekeka wapinzani bungeni Sasa hivi iwe nongwa kwa nini! Acheni deko upinzani tafteni agenda zenye maana wananchi wawaelewe zaidi ya hapo chaguzi zote mtakuwa watu wa kulialia kila siku
 
Back
Top Bottom