Ni nani anasimamia Uchaguzi Tanzania?

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
2,032
3,913
Habari za wakati Huu;
Haya ni maoni ambayo pia nimeona niyalete hapa tuyaone. Moja kati ya changamoto kubwa kuliko katika Demokrasia ya Tanzania ni swala zima la Msimamizi wa Uchaguzi. Je Jukumu la Kusimamia Uchaguzi wa Rais, Wabunge n.k. Apewe nani?

Wengi wamekuwa wakifikiri kwamba Kitendo cha Wakurugenzi wa Halamashauri kuwa wasimimizi wa Uchaguzi kuna wabeba CCM Jambo ambalo mimi Pia ninakubaliana nalo.Swali ni Je Jukumu Hili Apewe nani?

Baada ya tafakari FupiNimefikiria Ifuatavyo.Jukumu la Kusimamia Uchaguzi Liwekwe Chini ya Tume ambayo Itakuwa ni Tume ya Kimahakama a bayo iko chini ya Mhimili wa Mahakama.Kwa Lugha Nyingine Tume ya Uchaguzi Yote kama Ilivyo pamoja na Sheria ya Vyama vya Siasa Yote Ihamishiwe Chini ya Usimamizi wa Jaji mkuu.

Kwa nini napendekeza Hivi? Ni kwa sababu wateule wote wa Bunge na Serikali wote wanaapa Kwa mujibu wa sheria na viapo vyao vinasimamiwa na Mahakama.

Pili mahakama na mahakamu kimsingi wanafahamika na kueleweka kama wasimamizi wa Haki na wenye uwezo wa kutafsiri sheria Hivyo basi Uchaguzi utakapokuwa Chini yao unaweza kusimamiwa Kimahakama kabisa ikiwamo mfumo wa Rufaa, Mfumo wa kuteua na kutengua n.k.


Nilikuwa safarini wakati walipokuwa wanashughulikia Suala la Sheria ya uchaguzi na sikupata kufika Dodoma ila nafikir maoni yangu hayajachelewa.

Mwisho ushauri wangu kwa Spika TULIA AKSON MWAINYEKULE. Ni wakati sasa wa BUnge kuwa na ID yake RASMI hapa JF ili kuonesha kwamba Nyie ni chombo cha kiraia chenye nia na utayari wa kusikiliza na kutoa majibu na kupokea maoni ya wananchi ambayo yanaweza kupelekwa moja kwa moja kwa wabunge husika au moja kwa moja kwa mawaziri.

Msikae peke yenu kusimamia serikali kisha wakati wa uchaguzi mnatuletea stori nyingi FEKI.
 
Back
Top Bottom