Serikali yaondoa zuio kuuza mazao nje ya Nchi

hugochavez

JF-Expert Member
Mar 1, 2013
1,907
1,009
Waziri wa kilimo wa Tanzania Charles Tizeba amelitangazia bunge mjini Dodoma kuwa serikali imeondoa zuio LA kuuza mazao nje nchi na hivyo mipaka ya Tanzania sasa iko wazi kwa wafanyabiashara na wadau wote wa kilimo kusafirisha mazao nje ya nchi kutafuta masoko na hivyo kuiletea nchi fedha za kigeni. Kilio cha wananchi kimesikika rasmi.

 
BIASHARA NI DIPLOMASIA!

So far, ingependeza kama mheshimiwa angemtuma waziri mkuu kwenda Kenya 'kutafuta masoko' ya mahindi. Yani kuwaomba wakenya wanunue mahindi toka Tanzania maana wakenya walisusa kununua mahindi.

Hata ukifungua mipaka kama wanunuzi wamesusa ni kazi bure. So PM akaongee na Kenyata amweleze siuation tuliyokuwa nayo mwaka jana kabla ya kupiga marufuku export ya mahindi kwa kuwa sisi wenyewe tulikuwa na sintofahamu juu ya uhakika wa chakula.

Akitoka hapo PM asafiri kwenda India akaongee na waziri mkuu, amweleze jinsi livelihood ya wakulima wa Tanzania inavyotegemea soko la mbaazi la uhakika la India, hivyo PM wa India afanye kila analoweza kuhakikisha mbaazi za Tanzania zinapata soko.

Mwisho kabisa PM aongee na major exportes wa mbaazi wa hapa Tanzania na wale wa nje ya nchi ili 'wawezeshwe' kuexport mbaazi kama ilivyokuwa mwazo.

PM akimaliza hii task achukue na likizo ya mwezi mmoja kwenda kula bata Hawaii!
 
Wakulima wangekula mahindi kila siku bila mboga

Wakulima wangekosa pesa ya kununua hata sukari na mafuta ya kula

Wakati mwingine acheni kukurupuka na kuumiza wananchi,mwaka jana wakulima walipata hasara sana

Kukurupuka sukari ikapanda bei

Je, na hili tuwapongeze? Labda vilaza

Yaani ulete matatizo, halafu uyatatue then upongezwe.
 
Mnawaomba Swiss wawekeze kwenye Mifugo?

Yaani serikali inashindwa kuweka Budget ya kutosha wizara ya Mifugo, wataalamu wetu wa SUA wafanye kazi?
 
Hii ni habari njema kwa wakulima na uchumi wa Tanzania.Asante Mh.Tzeba.Sorry Mh.JPM kwanza.
 
Waziri wa kilimo wa Tanzania Charles Tizeba amelitangazia bunge mjini Dodoma kuwa serikali imeondoa zuio LA kuuza mazao nje nchi na hivyo mipaka ya Tanzania sasa iko wazi kwa wafanyabiashara na wadau wote wa kilimo kusafirisha mazao nje ya nchi kutafuta masoko na hivyo kuiletea nchi fedha za kigeni. Kilio cha wananchi kimesikika rasmi
Kama hili litafanyika bila "mizengwe" basi itakuwa heri sana kwa wakulima na sasa wataanza kufaidika na kilimo chao. Hasa hasa wakulima wa mahindi. Kenya na Sudani Kusini wanahitaji sana mahindi.
 
Back
Top Bottom