Serikali yaondoa zuio kuuza mazao nje ya Nchi

Serikali yaondoa zuio kuuza mazao nje ya Nchi

Waziri wa kilimo wa Tanzania Charles Tizeba amelitangazia bunge mjini Dodoma kuwa serikali imeondoa zuio LA kuuza mazao nje nchi na hivyo mipaka ya Tanzania sasa iko wazi kwa wafanyabiashara na wadau wote wa kilimo kusafirisha mazao nje ya nchi kutafuta masoko na hivyo kuiletea nchi fedha za kigeni. Kilio cha wananchi kimesikika rasmi
Wamefanya la maana, ila mda mwingine maamuzi yao yawe na tija sio kwa ajili ya kuwakomoa wananchi.
 
Wamefanya la maana
Ila mda mwingine maamuzi yao yawe na tija sio kwa ajili ya kuwakomoa wananchi
Serikali iwakomoe wananchi ili ifaidike kwa lipi kinachotokea uwa ni uhaba wa taarifa na utaratibu sahihi katika kufanya maamuzi na si kukomoana!
 
BIASHARA NI DIPLOMASIA!

So far, ingependeza kama mheshimiwa angemtuma waziri mkuu kwenda Kenya 'kutafuta masoko' ya mahindi. Yani kuwaomba wakenya wanunue mahindi toka Tanzania maana wakenya walisusa kununua mahindi. Hata ukifungua mipaka kama wanunuzi wamesusa ni kazi bure. So PM akaongee na Kenyata amweleze siuation tuliyokuwa nayo mwaka jana kabla ya kupiga marufuku export ya mahindi kwa kuwa sisi wenyewe tulikuwa na sintofahamu juu ya uhakika wa chakula.
Akitoka hapo PM asafiri kwenda India akaongee na waziri mkuu, amweleze jinsi livelyhood ya wakulima wa Tanzania inavyotegemea soko la mbaazi la uhakika la India, hivyo PM wa India afanye kila analoweza kuhakikisha mbaazi za Tanzania zinapata soko.
Mwisho kabisa PM aongee na major exportes wa mbaazi wa hapa Tanzania na wale wa nje ya nchi ili 'wawezeshwe' kuexport mbaazi kama ilivyokuwa mwazo.
PM akimaliza hii task achukue na likizo ya mwezi mmoja kwenda kula bata Hawaii!
Unaijua njaa mkuu?

Kifupi hakuna mwenye jeuri ya kususa chakula Dunia hii.
 
..serikali dhalimu hii unafanya mambo kwa upuuzi Mkubwa...mara leo mafuta ya kula wamezuia mara mazao wanazuia kuuzwa nje...wakati wao wamekaa watakula kodi za RAIA wakati RAIA wanapta hasara kila kukicha...
 
Mnawaomba Swiss wawekeze kwenye Mifugo?

Yaani serikali inashindwa kuweka Budget ya kutosha wizara ya Mifugo, wataalamu wetu wa SUA wafanye kazi?
Kilimo ni UTI wa mgongo wa nchi hii 70% ya watanzania wanategemea kilimo na 30% ya pato la nchi linatoka na kilimo Lkn huwezi amini barget yake imetengewa tsh 178 billion tu ktk mwaka huu wa fedha[emoji20] wakati huo huo wizara ya ulinzi imetengewa kiasi Cha tsh 1.9 tillioni sijui tunataka kuingia vitani[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kenya huu ndo Mpango wao
FB_IMG_1525683356621.jpg
 
BIASHARA NI DIPLOMASIA!

So far, ingependeza kama mheshimiwa angemtuma waziri mkuu kwenda Kenya 'kutafuta masoko' ya mahindi. Yani kuwaomba wakenya wanunue mahindi toka Tanzania maana wakenya walisusa kununua mahindi. Hata ukifungua mipaka kama wanunuzi wamesusa ni kazi bure. So PM akaongee na Kenyata amweleze siuation tuliyokuwa nayo mwaka jana kabla ya kupiga marufuku export ya mahindi kwa kuwa sisi wenyewe tulikuwa na sintofahamu juu ya uhakika wa chakula.
Akitoka hapo PM asafiri kwenda India akaongee na waziri mkuu, amweleze jinsi livelyhood ya wakulima wa Tanzania inavyotegemea soko la mbaazi la uhakika la India, hivyo PM wa India afanye kila analoweza kuhakikisha mbaazi za Tanzania zinapata soko.
Mwisho kabisa PM aongee na major exportes wa mbaazi wa hapa Tanzania na wale wa nje ya nchi ili 'wawezeshwe' kuexport mbaazi kama ilivyokuwa mwazo.
PM akimaliza hii task achukue na likizo ya mwezi mmoja kwenda kula bata Hawaii!
Nyie ndio mnaopiga kelele tu mitandaoni, utawezaji kuishauri Serikali kitu cha kipuuzi hicho. Yaani Wakenya walituchokoza kwa kuanza kuzuia mitungi yetu ya gesi na sisi tukawajibu kupitia kwa Rais wetu asiye na mzaha, halafu leo sisi ndio tuwaombe wanunue mahindi yetu kana kwamba ni sisi wenye njaa?
Hivi nani mwenye shida hapa, Tanzania ambayo ina chakula cha kutosha imekosa pa kuuza ama Kenya wasio na chakula ila wakakosa pa kununua? Nani anapaswa kumuanza mwenzake?
Katika kumbukumbu zako nchi gani iliyowahi kuiomba Tanzania ili inunue chakula chake? Nimezoea tu kuona Tanzania ndio tunaomba chakula cha msaada ikiwa ni pamoja na kununua nje.
Waambieni wao ndio waje msitufanye sisi wote ni duni kama mlivyo nyie.
 
Unaijua njaa mkuu?

Kifupi hakuna mwenye jeuri ya kususa chakula Dunia hii.
Kwani mkulima uko peke yako? Mbona hata Zambia wanalima mahindi mengi tu? Kwani tulivyozuia kuuza mahindi nje walikuwa wananunua wapi?
 
Next year watarudisha tena zuio. Hizi fikra za kijamaa hazitatuoa kama nchi hata kidogo.
Wameruhusu lakini too late. Sasa hivi Uganda ndiyo exporter mkubwa. Tutauza wapi? Kenya, Rwanda na DRC wote wananunua Uganda.
 
Njoeni uku mahindi yapo gunia 15000 elfu, yani debe tsh 2500. Ata kg moja ya sukari haijafika. Kufunguliwa mipaka ni fursa kwa mkulima kuvuna jasho lake sasa
 
Sasa wamepata nini kama siyo kutuongezea umaskini!
 
Mm nasubiri iruhusu fao la kujitoa ili nistaafu mapema nifanye mambo yangu.

Siipendi hii serikali kwa mengi ila hili ni kati ya yale mabaya kabisa.
 
Mi nashauri tungeanzisha soko la pamoja la chakula la afrika mashariki. Yaani kwenda kuuza mahindi uganda au kenya iwe kama kutoa Mbeya kupeleka Dar. Kwenye hili Tanzania itafaidika sana. Samaki , Vitunguu , nyama na misosi yote iwe inapita free kwenye mipaka ya EA.
 
Kufunguliwa mipaka kuendane na ufikishwaji wa pembejeo kwa wakati , malipo ya haraka kwa wakulima na utatuzi wa migogoro ya ardhi .

Wanasiasa mmezoea kupayuka payuka tu. Na ole wenu muongeze ushuru wa mazao mipakani tutahamia zetu kulima Zambia.
 
Back
Top Bottom