Serikali yamwaga vitanda vya wagonjwa nchi nzima

Serikali yamwaga vitanda vya wagonjwa nchi nzima

Nani amewambia shda ni vitanda? Dawa na watumishi ndo htaji la hospt! Mnagawa vitanda walalie wagonjwa bila kupata dawa? Hafu mwataka sifa kwenye hamna! Nyumbu ni nyumbu tu maana hamjui hata vipaumbele vya wananchi!
 
MAGUFULI AMWAGA VITANDA VYA WAGONJWA NCHI NZIMA.


Katika Muendelezo wa Utekelezaji wa Ahadi za Mh Rais Magufuli Kusambaza Vitanda Nchi Nzima katika Vituo vya Afya.
Wizara ya Afya ilitenga Tsh 4,000,000,000,00 katika Bajeti ya Mwaka 2016/2017, Sasa Wizara imeanza utekelezaji Huo kwa Halmashauri zote 184 Nchini.

Uzinduzi wa Zoezi hilo Umefanyika Leo 11/04/2017 katika Halmashari ya Kongwa, Ambapo Waziri wa Afya Mh Ummy Mwalimu Amemkabidhi Mh Job Ndugai Mbunge wa Kongwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sehemu ya Vifaa hivyo.
Katika Zoezo hilo kila Halmashauri nchini itapatiwa Vitanda vya Hospitali vya Kawaida (Hospital Beds) 20;
Vitanda vya Kujifungulia wajawazito (Delivery beds) 5;
Magodoro 25 na Mashuka 50.

Jumla ya Vifaa vitakavyogawiwa Halmashauri zote 184 nchini ni Vitanda vya Hospitali vya Kawaida (Hospital Beds) (3,680); Vitanda vya Kujifungulia Wajawazito (Delivery Beds) (920); Magodoro (4,600); na Mashuka (9,200).

Thamani ya Vifaa hivi ni Tsh Billion 2,933,125,600. Zoezi hili linatarajiwa kukamilika kabla ya Tarehe 30 June 2017.

Aidha Awamu ya pili ya Mgawo huu itahusisha Hospitali za Rufaa za Mikoa, Hospitali za Rufaa za Kanda na Hospitali Maalum. Ni Matarajio ya Wizara kuona vifaa hivi vinagawiwa kwenye Vituo vya kutolea Huduma za Afya vya Umma vyenye uhitaji kwa kuzingatia vipaumbele vya Halmashauri Husika.

Wizara ya Afya inapenda Kumshukuru Mh Rais Magufuli kwa Uwamuzi wake wa kuhakikisha fedha za Umma zinatumika kwa Ajili ya Kuboresha Huduma za Afya hapa Nchini.

Ameyasema nakufafanua vyema waziri wa Afya Mh Ummy Mwalimu aliwa Kongwa ktk Ugawaji wa Vifaa Hivyo.

KWA PAMOJA, TUNABORESHA AFYA ZETU!
 
Uhuru unao nyumbani kwako Mkuu unapoamua ule chukuchuku Hakuna atakayekuuliza. Huo uhuru wa kutukana viongozi au kupinga kila lililo jema alimradi limeletwa au kufanywa na usiowapenda sio uhuru ni kufuru
PUMBAVU HUJIELEWI
 
Tunahitaji uhuru si vitanda!
Eeee!! jamani kwa hiyo mkuu bora uhuru kuliko vitanda vya hospitali!! hawa vijana wetu jamani bora viroba vipigwe marufuku!!!

Yaani binadamu ni mtu wa ajabu sana hata umjengee nyumba ukamwambia bwana nyumba yako yeye atasema mbona rangi haujapaka vizuri [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Eeee!! jamani kwa hiyo mkuu bora uhuru kuliko vitanda vya hospitali!! hawa vijana wetu jamani bora viroba vipigwe marufuku!!!

Yaani binadamu ni mtu wa ajabu sana hata umjengee nyumba ukamwambia bwana nyumba yako yeye atasema mbona rangi haujapaka vizuri [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
Bora ugali kwa pilipili manga kuliko ugali kwa nyama huku ukisimangwa!!!
 
Cha msingi hapo ni Serikali kusikia na kutatua kero za muda mrefu katika sekta ya Afya za Watanzania. Chuki na Roho mbaya zitawatafuna na kuwamaliza awamu hii.
Kuna watu unaweza dhani sio RAIA wa nchi hii!!Yaan kila jema lifanywalo na Serikali ni mwiba kwako halafu wakiumwa kimbilio ni ktk hospital za serikali!!!
 
Mnapomuandika andika huyu jamaa kwa mambo ya serikali kanakwamba amefanya yeye ndio mnampakiburi zaidi!!!

Say,serikali inayoongoza na magufuli wamefanya abcd co unamtaja binafsi ndio maana anakuwa na kiburi hadi....!!
Hongera raisi wetu JPM kwa mema ututendeayo
 
Kodi ndizo zimenunua viwanda. Kwani Raisi anafanya biashara gani?. Hizi ndizo akili za Watanzania, yaani hata haki zao walipewa wanaona ni hisani.
wewe mange kimambi atakuwa mkeo siyo bure.
 
Ametoa hela yake ya mfukoni?
Vitanda 20 vinakidhi haja? Pengine ummpa sifa isiyo... Me nadhani ungesema hivi

Serkali yaanza na kupeleka vitanda 20 kwenye Halmashauri.
Au kaama lengo ni kumtaja huyo ulie mtaja basi ingesomeka hivi

******** aidhinisha vitanda 20 kila halmshauri.

Ukisema amwaga kwanza utadhi viingi kiasi kwamba hakuna sehemu ya kupita.

Au ******** katumia hela yake ya mfukon kunuunua hivyo vitanda.

Kodi zetu wenyewe hizooo mkuu, na niwanibu wa serkali kufanya hivyo.

WAJIBU SIO ZAWADI
Kwa utendaji huru wa jpm cjui ukawa watatuambia nini
 
Back
Top Bottom