Huu uzi sizani kama utapata wachangiaji, watanzania tushazoe vitu vibaya, wapiga ramli kibao, kila siku wanaomba mabaya yatokee, kwenye kukosoa tunasifia na kwenye kusifia tunakosoa , sijui uzalendo wetu upo wapi, wanasiasa wanatugawa wametugeuza misukule yao kila kitu ndio ndio, tumekuwa kama chuma (conductor) kwenye joto tunakuwa wamoto kwenye baridi tunakuwa wabaridi, tumekuwa watu wakuendeshwa na matukio, sometimes hata uwezo wa kureason out, yapi maneno ya msingi yapi ya kipumbavu tunashindwa tunaendeshwa na mitandao ya jamii, mwisho wa siku inatugawa . Hongera rais wewe fanya kazi, hii mitandao ya kijamii na maneno ya baadhi ya wanasiasa yasikuchoshe kwani sisi tunayaona mambo mazuri unayoyafanya.