Serikali yamwaga vitanda vya wagonjwa nchi nzima

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
Kila Halmashauri kupewa Vitanda vya Hospitali vya kawaida 20, Vitanda vya kujifungulia wajawazito 5, Magodoro 25 na Mashuka 50.
----

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO​

TAARIFA KWA UMMA

USAMBAZAJI WA VIFAA VYA HOSPITALI KWA HALMASHAURI
ZOTE 184 NCHINI

Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuboresha huduma za Afya nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za Afya kwa kiwango kinachotakiwa na hivyo kuweza kushiriki kikamilifu katika kujiletea maendeleo yao sambamba na kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa viwanda. Baadhi ya maeneo yaliyofanyiwa uwekezaji mkubwa ni upatikanaji wa dawa ambapo Bajeti ya dawa imeongezeka kutoka shilingi bilioni 31 mwaka 2015/16 hadi shilingi bilioni 251 mwaka 2016/17. Hatua hii imeleta mapinduzi makubwa katika upatikanaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba kwenye vituo vya umma vya kutolea huduma za afya.

Aidha, kufuatia ahadi ya Mhe. Rais ya kununua na kusambaza vitanda kwenye vituo vya umma vya kutolea huduma za afya nchini, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ilitenga kiasi cha shilingi 4,000,000,000.00 katika bajeti ya mwaka 2016/17, ili kuwezesha ununuzi na usambazaji wa Vifaa vya Hospitali katika Vituo vya kutolea huduma za afya. Tunapenda kuutaarifu umma kuwa, Wizara imeanza rasmi zoezi la kitaifa la kusambaza Vifaa vya Hospitali kwa Halmashauri zote 184 nchini. Uzinduzi wa zoezi hili unafanyika leo tarehe 11/4/2017 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, ambapo Mhe. Ummy Ally Mwalimu (Mb), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto atamkabidhi Mhe. Job Ndugai (Mb), Mbunge wa Kongwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sehemu ya vifaa hivyo. Katika zoezi hili, kila Halmashauri nchini itapatiwa Vitanda vya Hospitali vya kawaida (Hospital beds) (20); Vitanda vya kujifungulia wajawazito (Delivery beds) (5), Magodoro (25) na Mashuka 50.

Jumla ya Vifaa vya Hospitali vitakavyogawiwa kwa Halmashauri zote 184 nchini ni Vitanda vya Hospitali vya kawaida (Hospital beds) (3,680); Vitanda vya kujifungulia Wajawazito (Delivery beds) (920); Magodoro (4,600); na Mashuka (9,200). Thamani ya vifaa hivi ni shilingi Bilioni 2,933,125,600. Zoezi hili linatarajiwa kukamilika kabla ya tarehe 30 Juni 2017.

Aidha, napenda kuchukua fursa hii kuutaarifu umma kuwa awamu ya pili ya mgao huu wa Vifaa vya Hospitali itahusisha Hospitali za Rufaa za Mikoa, Hospitali za Rufaa za Kanda na Hospitali maalum. Ni matarajio ya Wizara kuwa vifaa hivi vitagawanywa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vya umma vyenye uhitaji kwa kuzingatia vipaumbele vya Halmashauri husika.

Wizara ya Afya inapenda kumshukuru Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uamuzi wake wa kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa ajili ya kuboresha huduma za afya hapa nchini.

KWA PAMOJA, TUNABORESHA AFYA ZETU!

Imetolewa na;
Catherine Sungura,
Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikali - Afya,
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Chuo Kikuu cha DODOMA,
S.L.P. 743,
DODOMA.

11 Aprili 2017

IMG-20170411-WA0034.jpg
IMG-20170411-WA0027.jpg
 
Cha msingi hapo ni Serikali kusikia na kutatua kero za muda mrefu katika sekta ya Afya za Watanzania. Chuki na Roho mbaya zitawatafuna na kuwamaliza awamu hii.

Jibu swali sio unajiongelesha ovyo.
 
Mnapomuandika andika huyu jamaa kwa mambo ya serikali kanakwamba amefanya yeye ndio mnampakiburi zaidi!!!

Say,serikali inayoongoza na magufuli wamefanya abcd co unamtaja binafsi ndio maana anakuwa na kiburi hadi....!!
 
Kodi ndizo zimenunua viwanda. Kwani Raisi anafanya biashara gani?. Hizi ndizo akili za Watanzania, yaani hata haki zao walipewa wanaona ni hisani.
Ewaaaa! watanzania wajinga. Mtu anshukuru haki yake!
 
Ametoa hela yake ya mfukoni?
Vitanda 20 vinakidhi haja?.

Pengine umempa sifa isiyo...

Me nadhani ungesema hivi

"Serkali yaanza na kupeleka vitanda 20 kwenye Halmashauri".

Au kaama lengo ni kumtaja huyo ulie mtaja basi ingesomeka hivi

"******** aidhinisha vitanda 20 kila halmshauri".

Ukisema amwaga kwanza utadhani viingi kiasi kwamba hakuna sehemu ya kupita.

Au ******** katumia hela yake ya mfukon kunuunua hivyo vitanda.

Kodi zetu wenyewe hizooo mkuu, na niwajibu wa serkali kufanya hivyo.

WAJIBU SIO ZAWADI
 
Hapa Serikali inastahiki pongezi japo ni wajibu wao ila kwa kawaida serikali za waafrika wakifanya jambo kama hili huwa wanastahiki pongezi sio kwa sifa ya ufisadi walizonazo hao viongozi.

Hapo tu kwenye hivyo vitanda ukute havijanunuliwa vile exactly vilvyotolewa hela na kuna watu wamepiga % zao kama kawaida.

Tusiwe wachoyo wa shukrani japo ni kodi zetu ila inahitaji moyo kuyafanya haya kwa viongozi wetu wa Tanzania. Tunasubiri dawa sasa maana tukienda kulala kule hospital bila dawa ni kazi bure.
 
Kitu unique katika huu utawala ni kutumia nguvu kubwa kupromote "AWAMU HII CHINI YA JPM....."....Yani sasa hivi kusema tu serikali huwa haitoshi lazma uweke wazi kuwa ni awamu ya tano tena chini ya JPM...Hahahah

By the way, at least kuna good news wiki hii....Hongera wahusika
 
Back
Top Bottom