Serikali yamfukuza anayefanya biashara ya binadamu nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yamfukuza anayefanya biashara ya binadamu nchini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bajabiri, Sep 4, 2011.

1. B

Bajabiri JF-Expert Member

#1
Sep 4, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 9,755
Likes Received: 27
Trophy Points: 0
Hatimaye serikali imeamua kumtimua mfanyabiashara anayejihusisha na biashara ya binadamu hapa nchini, mfanyabiashara huyo ambaye ni raia wa Pakistan anajulikana kwa jina la Altaf Hussein na pia ni mmiliki wa kampuni ya Altaf and Company.

Bwana Altaf alihusishwa na biashara ya kuuza binadamu ambapo inasadikika kuwa aliwaingiza nchini raia wa Pakistan wapatao 43, ambapo kila raia alilipa shilingi milioni 10 kwa Altaf wapakistan hao ambao waliajiriwa kwenye viwanda mbali mbali nchini nao wamefukuzwa nchini chini ya uangalizi maalum.

Wafanyakazi waliofukuzwa walikuwa wakifanya kazi kwenye viwanda vya Simba steel, IRON STEEL na Nyakato steel, kama mtakumbuka wiki moja iliyopita niliweka habari juu ya biashara ya Binadamu.

Habari hii imeripotiwa na gazeti la NIPASHE

2. AirTanzania

AirTanzania JF-Expert Member

#2
Sep 4, 2011
Joined: Mar 17, 2011
Messages: 1,127
Likes Received: 678
Trophy Points: 280
Na hivyo viwanda vilivyoajiri hao illegal immigrant vimepewa adhabu ya kulipa faini au ndio kiini macho?

3. B

Bajabiri JF-Expert Member

#3
Sep 4, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 9,755
Likes Received: 27
Trophy Points: 0
Vimekiri tu,,,,,hahahahaaaaa

4. Ndahani

Ndahani JF-Expert Member

#4
Sep 4, 2011
Joined: Jun 3, 2008
Messages: 14,325
Likes Received: 1,792
Trophy Points: 280
Mambo ya mjomba mjomba. Kila kitu kina mwisho wake

5. B

Bajabiri JF-Expert Member

#5
Sep 4, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 9,755
Likes Received: 27
Trophy Points: 0
What? Unamaanisha nin mkuu???

6. Filipo

Filipo JF-Expert Member

#6
Sep 4, 2011
Joined: Jan 6, 2011
Messages: 9,329
Likes Received: 210
Trophy Points: 160
Hapa ndio mahali natofautiana na serikali. Nilifikiri angekamatwa, ashtakiwe kisha apate hukumu. Hao aliowaleta nao kama walijua wanafanya usanii kuingizwa nchini illegally nao wapate adhabu yao.

Mwisho ni viwanda vilivyowaajiri navyo lingeshtakiwa na kupata adhabu yao! Hiyo ingetoa onyo kwa wengine wote. Sasa hii serikali inamfukuza mtu kaja hapa kafanya biashara haramu na faida keshaipata halafu unamwambia arudi kwao. Tena bila hatua zozote za kisheria.

Huo ni ujinga!

7. mikatabafeki

mikatabafeki JF-Expert Member

#7
Sep 4, 2011
Joined: Dec 29, 2010
Messages: 12,837
Likes Received: 2,101
Trophy Points: 280
Kwa hiyo kutimuliwa kwake nchini si ni sawa na kumuachia huru..............aaaaagggghh u gyz u got 2 b kiddin me, c'moooon

8. B

Bajabiri JF-Expert Member

#8
Sep 4, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 9,755
Likes Received: 27
Trophy Points: 0
Hahahahaaaa,mikatabaaaaa ndo utawala wa sheria huo

9. B

Bajabiri JF-Expert Member

#9
Sep 4, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 9,755
Likes Received: 27
Trophy Points: 0
Na hii habari iliibuliwa na gazeti si maafisa wa uhamiaji,wenyewe uhamiaji wanalishukuru gazeti,mmmmh

10. T

Tikerra JF-Expert Member

#10
Sep 4, 2011
Joined: Sep 3, 2008
Messages: 1,704
Likes Received: 7
Trophy Points: 0
Afadhali kama aliishia kuuza watu kwa ajili ya ajira.Wengine wanawauza kama kitoweo na kubebea madawa ya kulevya!

11. N

Ndinani JF-Expert Member

#11
Sep 4, 2011
Joined: Aug 29, 2010
Messages: 5,413
Likes Received: 734
Trophy Points: 280
Hao waliohusika na kuibua biashara hii ya binadamu wa kutoka huko pakistani hawaoni huu umati wa wachina waliojaa Kariakoo wanauza njugu, nao wameingiaje huku bongo? Kuna mtu lazima anawafanyizia biashara wachina hawa; hebu chunguzeni!

12. Kinyungu

Kinyungu JF-Expert Member

#12
Sep 4, 2011
Joined: Apr 6, 2008
Messages: 4,381
Likes Received: 3,341
Trophy Points: 280
Kwa nini wamemfukuza na sio kumfunga?

13. B

Bajabiri JF-Expert Member

#13
Sep 4, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 9,755
Likes Received: 27
Trophy Points: 0
Labda sheria ndo zinasema hivo

14. B

Bajabiri JF-Expert Member

#14
Sep 4, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 9,755
Likes Received: 27
Trophy Points: 0
Nadhan uhamiaji kuna wadau wanahusika maana baadhi ya watendaj wa uhamiaj ndio walowatengenezea vibal fake hawa wapakistan

15. Mulhat Mpunga

Mulhat Mpunga JF-Expert Member

#15
Sep 4, 2011
Joined: Oct 28, 2010
Messages: 25,479
Likes Received: 12,757
Trophy Points: 280

WAWEZA KUTA NI VYA HAOHAO ILLEGAL IMMAGRANTS CHEZEA MIKATABA FEKI WEWE!

16. B

Bajabiri JF-Expert Member

#16
Sep 4, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 9,755
Likes Received: 27
Trophy Points: 0
Ni kweli hivo viwanda vinamilikiwa na wageni tupu,na huyu alokua akiwaingiza yeye alikuwa ana kibali cha kuish cha DARAJA B,kimsing kilimruhusu kuwa mfanyakazi wa kawaida tu,lakin aliitumia fursa hiyo kuanzisha kampuni,serikali ilikuwa inachapa usingizi tuuuuu

17. FaizaFoxy

FaizaFoxy JF-Expert Member

#17
Sep 4, 2011
Joined: Apr 13, 2011
Messages: 58,103
Likes Received: 22,144
Trophy Points: 280
Na wale wanawatembeza mabinti zetu juu ya majukwaa wakijidai sijui ma miss na wao wamo kwenye kundi hilihili la biashara ya binaadam, Utumwa. Hawana tofauti na hivyo viwanda. Jee, tusiwazozomokee?

Huyo Mpakistan anatumwa tu akatafute manpower, wenye makosa ni hivi viwanda. Bila wao kutaka angewaleta? Awalipe nini? Na hao wamekuja na ujuzi wao wa vyuma.

18. B

Bajabiri JF-Expert Member

#18
Sep 4, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 9,755
Likes Received: 27
Trophy Points: 0
Kimsingi watanzania wanafurahia masuala ya u-miss kama wangekuwa hawayataki naiman yasingepewa nafas,KUNA MBUNGE MMOJA WA ZANZIBAR jina nimemsahau alilalamikia sana suala la mambo ya U-miss pale bungeni wakat anachangia bajet ya Nchimbi,lakin kwenye majumuisho sikusikia wazir akigusia,kuhusu hawa wahamiaj haram,kiutaratibu raia wa kigen anapaswa apewe KIBALI so hata mwajiri ana wajibu wa kuhoj hicho kibali,kosa lipo uhamiaji,baadh ya maofisa wanapewa rushwa ili watoe vibal,hii stori ni muendelezo wa stor ya last week kuhusiana na hawa jamaa

Loading...