Baba Mkubwa
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 793
- 58
Na Reuben Kagaruki, Jijini
WAKATI walimu wanatarajia kuanza mgomo wao nchi nzima Jumatatu kushinikiza kulipwa fedha za malimbikizo yao, Serikali imetoa tamko zito ikisema mgomo huo ni batili huku ikikimbilia Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi kuomba iuzuie.
Hatua hiyo ya serikali imetangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo, alipozungumza na waandishi wa habari leo asubuhi na kutoa msimamo wa Serikali kuhusiana na mgomo uliotangazwa na Chama Cha Walimu Tanzania (CWT).
Akiwa ameongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Edna Mangesho na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Hamis Dihenga, Luhanjo amesema mgomo huo ni batili kwa sababu baadhi ya vipengele havikutekelezwa.
"Katika kusudio la mgomo wa walimu baadhi ya masharti hayakutimizwa ndio maana Serikali inapinga mgomo batili usio na kikomo,"amesisitiza Luhanjo.
Ameongeza kuwa tayari Serikali imekwishawasilisha Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi maombi ya Anuai Na:21 ya mwaka 2008 kuiomba izuie mgomo usio na kikomo unaokusudiwa kuanza Jumatatu.
"CWT imepelekewa samansi ya kuitwa mahakamani kwa ajili ya shauri hilo la maombi ya Anuai ambalo limepangwa kusikilizwa Jumatatu," amesisitiza Luhanjo.
Amesema kutokana na hatua zinazoendelea kuchukuliwa, Serikali imekitaka chama cha walimu kusitisha mgomo usio na kikomo. Luhanjo amesema mwalimu atakayeshiriki mgomo huo hatalipwa mshahara na serikali kwa sababu ya kushiriki mgomo batili.
Ametishia kuwa walimu watakaogoma, watalipwa mishahara yao na aliyeitisha mgomo huo. Amesema watakaogoma watachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria za kazi.
"Mgomo huo hauna maslahi kwa umma na hata kwa walimu wenyewe kwa sababu unakusudiwa kufanyika katika kipindi ambacho wanafunzi wanapaswa kufanya mitihani yao ya kuvuka madarasa na vidato,"amesema.
Ameikumbusha CWT kutambua kuwa suala hilo tayari lipo mahakamani hivyo kitendo cha walimu kugoma kitakuwa sawa na kuishinikiza mahakama kwenye kesi iliyofunguliwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Rais wa CWT, Gratian Mukoba, alitangaza kuwa mgomo huo usiokuwa na kikomo utaanza rasmi Jumatatu ambapo utahusisha walimu wa shule za msingi, sekondari, vyuo vya ualimu na vile vya maendeleo ya jamii ambao ndio wanachama wa CWT.
Mukoba amewataka walimu wasiogope vitisho vya Serikali kwa sababu mgomo huo ni halali. Baraza la Taifa la CWT linatarajia kukutana Januari mwakani ili kupitia utekelezaji wa madai yao.
Source: Dar leo