Serikali yakana hukumu ya kuilipa ESCROW dola Mil 185. Dk. Abbasi asema Serikali haidaiwi

Aiseee siasa bana ni ushenzi ushenzi fulani.
Huoni kwanini elimu haichukuliwi kwa uzito mkubwa ni sababu watu wakielimika huwezi msumbua unless aamue tu yeye kujitoa ufahamu, ndio mana illiteracy rate ndio kundi kubwa la wanaokua manipulated haswa na hizi fafanuzi
 
Serkali hawahusiki hapo ufafanuzi mzuri sana


Yalipe yale mafisadi yaliyojificha nyuma ya IPTL
Akili za kuambiwa changanya na za kwako,IPTL walipo enda kukopa Malaysia mdhamini wao aLlikuwa serikali ya Tanzania , Benk ya standard charter asingetoa pesa Kama hakuna mdhamini, IPTL iko chali kwa Hiyo mdhamini lazima aingizwe kwenye deni .Mwansheria mkuu usitufanye wote wajinga
 
Reactions: MTK
Tusiumize vichwa hapo, Mdhamini WA Haya makampuni ya IPTL yalikopa standard chartered bank ni serikali ya Tanzania , Kama mdaiwa halipi deni unamkunja mdhamini, hapo ndio serikali ya Tanzania inapoingia , Tujiandae tena Ndege yetu kukamatwa
 
Yu
Yu wapi Praise singer "extraordinary and plenipotentiary" Paskali Mayallah aunge mkono hoja hii mujarabu kwamba serikali haidaiwi hata kidogo na hukumu hii ya ICSID ni ya kutungwa na mabeberu wakiongozwa na Tundu Lissu???!!!
 
Abbas kasahau doctrine isemayo kwamba "Unaweza kuwahadaa baadhi ta watu kwa muda lakini huwezi kuwadanganya watu wote kwa wakati wote"!!; sooner rather than later the devil aka (pepo la udanganyifu) will catch up with you, big time!
 
Acheni uzwazwa. Nini maana ya kudhamini?
1. Mdhaminiwa asipotimiza matakwa ya makubaliano kati pande mbili za mkataba, mdhamini anawajibika, na
2. Serikali ya JMT haijabadilika. Viongozi wa kitaifa (marais) ndio wamekuwa wakipokezana nafasi.
Elewewaeni hilo. Madeni yaliyokopwa tangu enzi za Mwl Ñyerere ambayo bado kulipwa ni ya Tanzania. Rejeeni sakata la kushikiliwa ndege Afrika Kusini kufuatia Settler mdai kukazia hukumu mahakamani.
 
Waandishi wa habari wa Tanzania ni makanjanja kweli na ndio chanzo cha kupotosha jamii wakati kila kitu kimewekwa wazi au labda lugha shida.

Hakuna mahala serikari ilitoa udhamini kwa IPTL kukopa



Kwenye harakati za kukopa IPTL wali sign 'security deed' maana yake nini wakishindwa kulipa mdai anaweza kuchukua umiliki ya mali zao.



Mali walizokuwa tayari kutoa kwa security agent, wamiliki wa IPTL kwa mujibu wa mdeni ni share zote wanazomiliki kwenye kampuni.



Baada ya kupata mkopo wa kujenga na kununua mtambo wa kuzalishia umeme IPTL wakaingia mkataba wa kuuzia umeme TANESCO



Serikari ya Tanzania ichoahidi TANESCO wakishindwa kulipa hela za kununua umeme kutoka IPTL wao watalipa kwa ivyo waliidhamini TANESCO kulipia umeme kutoka IPTL iwapo watashindwa na sio udhamini wa deni la IPTL kwa bank walizokopa.



IPTL walidhamini share zao kwenye mabenki wakishindwa kulipa kampuni ichukiliwena kuendeshwa na mkopaji kama mali yao (this has nothing to do with the government) wao awajali nani mmiliki ilimradi wanauziwa umeme na kulipia.



Msisitizo ya kuwa wamiliki wa IPTL waliahidi kutoa shares zao wakishindwa kulipa deni kama makubaliano yao ya kukopa



Wakopeshaji ambae IPTL walitakiwa kuwalipa wanatajwa hapo juu na wakishindwa kampuni ni halali yao



Mwaka 2005 SCHK walipata umiliki wa hilo deni la IPTL kutoka kwa wakopeshaji na wanadai walivunja makubaliano ya malipo ivyo kwa mujibu security deed waliosaini iwapo watashindwa lipa mdeni atachukua shirika.
....................................................................................................................................................................................................

Ndio msingi wa kesi ya SCHK wao wamefungua kesi kama wamiliki wa IPTL kwa sababu wameshindwa lipa deni na wanadai serikari malipo kwa kutumia umeme wao kama walimiliki ya kampuni.

Upuuzu ni serikari kuwasikiliza badala ya kutaka kuona wanamalizana na shareholders wao waliokopa bank kwa sababu serikari aijui haswa masharti waliyokopea na watu waliokopa awajaenda mahakamani kujibizana na madai ya SCHK juu ya madai yao ya umiliki.
 
Umeisoma hukumu? Kama hujasoma nikusamehe, kama umesoma na kuandika haya unakoelekea siko wahi mapema matibabu ya...
 
Serkali hawahusiki hapo ufafanuzi mzuri sana


Yalipe yale mafisadi yaliyojificha nyuma ya IPTL
V. ◇The Government of United Republic of Tanzania◇shall;-
Pay to climant the sum of USD 185,449,440.04 together with interest thereonat the rate of LIBOR (6-Months) +2% from the 1 September 2018until the date of full and final payment....

Kuna sehemu imetaja IPTL hapo?

Huu uzuzu wa kuona watanzania mazuzu ukome!!!
 
Aisee hili swala angelizungumzia Mwanasheria Mkuu wa Serikali maana hawa baadae watakuja kuruka hukumu inasema wewe unadaiwa unaleta viswahili vya tuliunganishwa tuu kwenye kesi...
 
Kule Afrika Kusini ndege haiendi tena.
London ndege haiendi tena.

Bado wale jamaa wa Bagamoyo
Bado Symbion mmmmmh
Kweli Mabeberu si mchezo
IHiyo ya ndege na vijikesi vidogp vidogo ilikuwa rasha rasha cinema kamili ingekuja anageendelea na ujinga wake. Tuliyaona wakati wa Nyerere, mpaka sabuni ya kuongea tulikosa.

Tuwaone na Wazimbabwe walifanywa nini wakati wa Mugabe?

Hii mijitu mingine ni baraka ya kujua kufunga tai tu shingoni lakini vichwani ni zero kabisa. Tulifanya makosa makubwa sana CCM kuchagua mtu ambae hana asili ya uongozi.
 
pole bi faiza si ndo mnapenda hayamambo... mnasema kazi iendelee etiee 😂 😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…