Serikali yailipa PSSSF tsh Trillion 2 kati ya Trilion 4, wastaafu kulipwa mafao yao kwa wakati!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,924
141,891
Katibu mkuu wa wizara ya fedha Emmanuel Tutuba amesema serikali imeipa PSSSF kiasi cha tsh trillion 2.

Naye Mkurugenzi mkuu wa PSSSF Hosea Kashimba amesema kuanzia sasa wastaafu wote watalipwa mafao yao kwa wakati bila kuchelewa

Source: ITV habari

=====

Serikali, PSSSF wafikia muafaka juu ya deni la trilioni 4.66

December 22nd, 2021
*Kwa kuanzia wasaini makubaliano ya trilioni 2.17

*Katibu Mkuu: Deni linalipwa kwa utaratibu wa hati fungani maalum

*PSSSF: Tutaendelea kutoa huduma bora kwa Wastaafu

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Wizara ya Fedha na Mipango imetoa pongezi kwa serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa maelekezo ambayo yamepelekea kuhitimisha suala la muda mrefu kwa deni la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).

Kauli hiyo ilitolewa na katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Emmanuel Tutuba Desemba 22, 2021 jijini Dodoma katika sherehe ya utiaji sani makubaliano ya ulipaji wa shilingi trillioni 2.17 kwa PSSSF.

Bw. Emmanuel Tutuba alisema, “Sisi kama Wizara tumekuwa na majadiliano mara kadhaa na uliokuwa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) na sasa PSSSF juu ya kulishughulikia deni hili, baada ya kufanya uchambuzi wa kina juu ya suala hilo na kwa maslahi mapana ya wanachama wa Mfuko, Serikali imeamua kulipa deni hilo kwa kuanzia na shilingi trilioni 2.17, na deni hilo litalipwa kwa utaratibu wa hati fungani zisizo taslimu”.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Emmanuel Tutuba (wa pili kutoka kulia waliokaa) na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba (kushoto waliokaa) wakisaini hati za makubaliano ya ulipaji wa shilingi trilioni 2.17, anayeshuhudia kulia ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya waziri Mkuu, Prof. jamal Katundu.

Bw. Tutuba alisema katika hotuba ya Bajeti ya serikali ya mwaka 2021/2022 Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba alibainisha umuhimu wa wastaafu wa taifa letu ambao wamelitumikia taifa kwa uzalendo na uadilifu wa hali ya juu kupata stahiki zao kwa wakati. Katika kufanikisha hilo Waziri wa fedha aliahidi kuendelea kulipa madeni ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa kutenga fedha kwenye bajeti na kutoa hatifungani maalum.

Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa Jamal Katundu alitoa pongezi kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kulisimamia vyema na ukaribu suala la deni la PSSSF, ambalo linatoa faraja kwa wanachama wa PSSSF wakiwemo Wastaafu.
1-1.jpg

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Emmanuel Tutuba (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba (kushoto) wakionesha hati za makubaliano ya ulipaji wa shilingi trilioni 2.17, anayeshuhudia kulia ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya waziri Mkuu, Prof. jamal Katundu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba alisema, “Kwa niaba ya Bodi ya Wadhamini, tunatoa shukrani nyingi kwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali yake kwa kuweza kushughulikia suala hili ambalo limekuwepo kwa muda mrefu na kupatiwa ufumbuzi chini ya utawala wake. Kwa upande wetu tunaahidi kuendelea kufanyakazi kwa weledi katika kutoa huduma bora kwa wanachama wetu”.

CPA.Kashimba alisema, makubaliano hayo ya 2.17 trilioni ambayo ni sehemu ya deni la Pre 1999 la 4.6 yatasaidia Mfuko kupata mapato yanayotokana na hati fungani hizo takribani shilingi bilioni 120 kwa mwaka ambazo zitauwezesha Mfuko kupata unafuu wa deni la pre 1999 na pia kuuwezesha kutimiza jukumu lake la msingi la kulipa mafao.

Katika sherehe hizo Serikali iliwakilishwa na Katibu Mkuu wa wizara ya Fedha Bw. Tutuba na kwa upande wa PSSSF iliwakilishwa na CPA. Kashimba. Pia ofisi ya Waziri Mkuu iliwakilishwa na Naibu Katibuy Mkuu, Prof. Jamal Katundu.
 
Katibu mkuu wa wizara ya fedha Emmanuel Tutuba amesema serikali imeipa PSSSF kiasi cha tsh trillion 2.

Naye Mkurugenzi mkuu wa PSSSF Hosea Kashimba amesema kuanzia sasa wastaafu wote watalipwa mafao yao kwa wakati bila kuchelewa

Source: ITV habari
This is good news!. Kwa vile sijaisikia habari yenyewe, ni serikali kutoa fedha hizi kama wema fulani hivi au hisani!. Kiuekweli hiyo trilini mbili, yes ni something, better than nothing, ila watu mngeyasikia thamani ya madeni ya serikali kwenye huu mfuko wa PSSSF toka ulipokuwa PSPF, hiyo trilioni mbili ni punje tuu ya mchele kwenye gunia la PSSSF!.

Serikali iliwahamishia PSPF wastaafu wote waliokuwa walipwa pension na hazina, bila kuhamisha michango yao, hivyo kuibebesha PSPF zigo kubwa la kulipa pensheni nene, nono kwa wastaafu ambao michango yao haikuletwa!.

Tuipongeze serikali yetu kuanza kulipa madeni chechefu ya mifuko ya hifadhi za jamii!, ila kila inapolipa serikali pia should come clean and very transparent kuwa sio serikali wameipa bali waseme ukweli, wamelipa. Kiwango cha deni la serikali kwa PSSSF kitajwe, deni lililopunguzwa litajwe, kiasi kilichobaki kitajwe!.
Ila pia hawa PSSSF si mchezo!, washuhudie hapa...


P
 
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni!. Deni la PSSSF kwa serikali ni deni la muda mrefu tangu PSPF , msimsingizie marehemu ni utajichumia dhambi za bure!.
P
Watu wanachuki tu na mwendazake, huskii wakilaumu Mkapa aliewahamisha wastaafu kutoka hazina kwenda PSSF bila kupeleka michango yao...PSSF ilikua hoi bini taabani bin kukata roho in term of liqudilty, Benefit formula ya kifisadi(watu walikua wanapokea mafao manono while wamechangia kidogo) & ufisadi ktk miradi(yale ma ghorofa yao posta watu wamepiga hela za kutosha)
wasingeunganisha ile mifuko ule mfuko ungekua umesha collapse...na ule ndo ulikua na wafanyakazi wengi wa serikali.
Nway wanasema alieshikwa na nyama ndo mwizi ht km wezi walipita wakakuachia tu uwashikie nyama yao.
 
Hii inaitwa tengeneza tatizo uje ujisifu kRais msikivu kalitatua "KATIBA Ndiyo itatoa mzizi wa fitina"
Leo hii tungewakamata wote walio vuruga mfuko huu
Heb nipe uhusiano wa katiba na Halmaahauri au shirika la serikali kuwasilisha michango ya wafanyakazi wake...
 
Trillion 2 kwa wastaafu ni ndogo sana

Ila kama ni mpango endelevu kila baada ya muda mfupi watoe tena itasaidia
Ht ezi za JPM walitoa ma tirioni km haya.
Watatoa leo then miaka michache mbele tatzo litajirudia, maana watu hawasilishi michango ya wafanyakazi...couple of month ago kamati ya bunge iligundua halmashauri ya Shinyanga inadaiwa bilioni 40+ za michango ya wanachama. Na hilo ni halmashauri moja tu...unless waweke sheria inayowabana kuwasilisha michango ya wanachama hii kitu hitakuja kuisha...itakua ni game a cat and mouse.
 
Izo mbwembwe tu wazee wanakonda kwa mawazo na misongo mwaka wa pili sasa toka astafu anafatilia mafao yake anapigwa chenga Mimi kuwaamin mpaka nione izo pesa
 
Pesa zinachotwa kwa maelekezo au kusingiziwa mfalme kasema Katiba imara itaondoa mfalme power
Ukisoma report za hii mifuko tatzo sio pesa kuchotwa...maana ht wakichota wanachota kwa riba hazichukuliwi hivi hivi, na ht ukiangalia reports mikopo ya serikali kuu ni % ndogo sana ukilinganisha na michango ambayo haijawasilishwa...
Tatzo ni michango kutowakilishwa.
Tofauti na NSSF ambako ina deal na private km kampuni yako haijawasilisha michango yako hupati mafao huko PSSPF ina deal na wafanyakazi wa serikali, huko unapewa tu ht km michango yako haijafika then wao wanaendelea kuidai serikali na hapo ndipo deni linpoongezeka.
 
Back
Top Bottom