Serikali yailipa PSSSF tsh Trillion 2 kati ya Trilion 4, wastaafu kulipwa mafao yao kwa wakati!

Wastaafu wwliokufa na hawakulipwa naona jamaa kuni zinaongezeka huko
Dhulma mbaya sana

Mungu atamlipa Mama kwa kuwahurumia wastaafu
Tunajua ni haki yao ila wengi walinyimwa hiyo haki na hela zao kuchotwa tu
 
Hivi wastaafu kwa kila mwezi wanazidi 500 kweli?, Maana hizi nafasi za kisiasa watu wanafanya kazi hadi miaka 70,huku serikalini katika wilaya nzima unakuta kwa mwezi wamestaafu watu kumi tu,,
Kiufupi hata kwa mwaka kufika 10,000 ni ngumu sana

Tanzania ina wilaya zaidi ya 170, kama kwa mwezi mmoja kwenye wilaya moja wanastaafu watumishi10
Basi kila mwezi tuna wastani wa wastaafu wapya 1,700
Kwa mwaka wastani wa wastaafu 20,400
Hapa swala ni kuweka sawa namba na muda
 
Hivi wastaafu kwa kila mwezi wanazidi 500 kweli?, Maana hizi nafasi za kisiasa watu wanafanya kazi hadi miaka 70,huku serikalini katika wilaya nzima unakuta kwa mwezi wamestaafu watu kumi tu,,
Kiufupi hata kwa mwaka kufika 10,000 ni ngumu sana
58,000
IMG_20211223_095642.jpg
 
Serikali ndio inadumaza mashirika ya PSSSF na NSSF;
  1. Serikali kukomba fedha za wastaafu ktk mifuko hii tena bila ukomo na kushindwa kulipa fedha hizo na kusababisha wastaafu kuishi kwa shida, mateso na mahangaiko makubwa wakati fedha zao zilikusanywa.
  2. Viongozi wa mashirika haya kuwekeza ktk miradi mikubwa na isiyo na tija kwa wastaafu kisa tu viongozi kuweka maslahi yao mbele kwa % wanazolipwa na makampuni yanayopewa kandarasi za ujenzi (hili nalina ubishi na wanafahamika)
 
Ni jambo jema, maana Jiwe alikwangua hela zote za wastaafu akazipeleka anapojua yeye, yule jamaa angepiga miaka mingine 5 hadi 2025 TZ tungekuwa kama Afghanistan
Hivi ni kwamba serikali inachukua hela au HUWA HAWAPELEKI MICHANGO kiasi wanakuwa na deni kubwa? Miaka na miaka serikali wanasuasua kupeleka michango sio awamu iliopita tu. Ni jambo jema wameamua kulipa shirika litapumua.
 
Hakuna kitu hapo kitakacho wasaidia wastaafu suluhu ni walipwe mzigo wao wote.

Hii mifuko hadi ije kukaa sawa ni 2050 na inawezekana isije kukaa sawa. Serikali njaa hawawezi vumilia
 
Hili shirika livunjwe na kuwa kama mwanzo, mashirika ya PSSF,LAPF, NSSF..ingawa yalikuwa chini ya serikali lakini kulikuwa na ushindani wa kihuduma
wapuuuzi sana hawa PSSSF utafikiri wao hawatastaafu.wanaikopeshaji fedha serikali bila kuwahusisha wafanyakazi ambao ndio wenye fedha?wajinga sana hao jamaa na hilo shirika livunjwe kabisa kuna wastaafu wamekufa bila kupata pesa zao.hao ni washenzi tu.
 
Trilion 2 ni sehemu tu ya deni, na hailipwi kwa mkupuo mmoja,, hiyo hela haipo,, labda tuamue kuchapisha zingine,, nilivyoelewa malipo ni 120 bilions per year.
Ila trilion 2 ni pesa ndefu sana , inaweza kulipa wastaafu wote wa africa mashariki na kati
Wemeamua kuilipa kwa njia ya hati fungani.. hio 2T ni kwa miaka 8 ambapo watakua wanalamba 120B per year...
Habari kamili.
 
Hivi ni kwamba serikali inachukua hela au HUWA HAWAPELEKI MICHANGO kiasi wanakuwa na deni kubwa? Miaka na miaka serikali wanasuasua kupeleka michango sio awamu iliopita tu. Ni jambo jema wameamua kulipa shirika litapumua.
Sometimes wanachukua Chief, mambo yakiwa tight
 
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni!. Deni la PSSSF kwa serikali ni deni la muda mrefu tangu PSPF , msimsingizie marehemu ni utajichumia dhambi za bure!.
P

Mkuu Pascal Mayalla Sijui kwa UPande wa wwngine wanashabikia au wanaelewa? Naomba Kuuliza Nipewe Elimu Kaka!
1.Hivi hayo Malipo ni Kwamba Tangu Mwaka 1999 walipostaafu watu hawakulipwa? Au walilipwa Mapunjo?
2.Ina Maana Kama hawakulipwa walikuwa wanaishije?
3.Ina Maana Ni Kuanzia Mwaka 1999 to date
Waliostaafu au 1999kurudi nyuma?
4.Ina Maana Waliostaafu Miaka hiyo Hawakupata Malipo Yeyote? Kwa hiyo sasa hivi ndio wanawalipa? Au walipata Kidogo sasa wanataka Kuwalipa Mapunjo?
Naonba Nieleweshwe!
 
Mkuu Pascal Mayalla Sijui kwa UPande wa wwngine wanashabikia au wanaelewa? Naomba Kuuliza Nipewe Elimu Kaka!
1.Hivi hayo Malipo ni Kwamba Tangu Mwaka 1999 walipostaafu watu hawakulipwa? Au walilipwa Mapunjo?.
  1. Kwenye watumishi wa umma, kuna kada ya wastaafu wa serikali ambao walikuwa wanalipwa na Hazina , mwaka 1999, serikali ikawahamishia wastaafu hao kutoka hazina na kuwapeleka mfuko wa PSPF, bila kupeleka michango yao.
  2. Wastaafu wa serikali ndio kada inayolipwa mafao manono na manene kwasababu ya formula ya michango. Watumishi wa serikali, mtumishi anachangia asilimia 5% ya mshahara wake, mwajiri serikali anachangia asilimia 15%. Kada nyingine zote mwajiriwa anakatwa 10% na mwajiri anachangia 10%.
  3. Hivyo serikali ikawahamishia PSPF hao wastaafu wa hazina, bila kuhamisha michango yao ya zaidi ya bilioni 4.
  4. PSPF ikabebeshwa mzigo mzito wa madeni kuendelea kuwalipa wastaafu ambao ambao hawajachangia hata senti tano.
  5. Walilipwa malipo kamili bila mapunjo yoyote na mafao ya PSPF ni mafao bora, makubwa, manene, manono na mazuri.
2.Ina Maana Kama hawakulipwa walikuwa wanaishije?.
Kama nilivyoeleza hapo juu, wastaafu hao wakiendelea kulipwa mafao ya PSPF ambayo ni mafao bora, makubwa, manene, manono na mazuri.
3.Ina Maana Ni Kuanzia Mwaka 1999 to date
Waliostaafu au 1999kurudi nyuma?.
Yes ni wastaafu wote wa kuanzia mwaka 1999 kurudi nyuma. Watumishi wa serikali serikali waliopo kazini sasa walianza kuchangia mfuko wa PSPF, hivyo kwa wastaafu wapya, michango yao ilikuwepo
4.Ina Maana Waliostaafu Miaka hiyo Hawakupata Malipo Yeyote? Kwa hiyo sasa hivi ndio wanawalipa? Au walipata Kidogo sasa wanataka Kuwalipa Mapunjo?
Naonba Nieleweshwe!
Kama nilivyoeleza hapo juu, walilipwa malipo yao yote. Swali labda liwe kama walihamishiwa PSPF bila kuletwa michango yao, jee walilipwa na fedha kutoka wapi?. Walilipwa kwa fedha kutoka vitegauchumi vya PSPF.
P
 
  1. Kwenye watumishi wa umma, kuna kada ya wastaafu wa serikali ambao walikuwa wanalipwa na Hazina , mwaka 1999, serikali ikawahamishia wastaafu hao kutoka hazina na kuwapeleka mfuko wa PSPF, bila kupeleka michango yao.
  2. Wastaafu wa serikali ndio kada inayolipwa mafao manono na manene kwasababu ya formula ya michango. Watumishi wa serikali, mtumishi anachangia asilimia 5% ya mshahara wake, mwajiri serikali anachangia asilimia 15%. Kada nyingine zote mwajiriwa anakatwa 10% na mwajiri anachangia 10%.
  3. Hivyo serikali ikawahamishia PSPF hao wastaafu wa hazina, bila kuhamisha michango yao ya zaidi ya bilioni 4.
  4. PSPF ikabebeshwa mzigo mzito wa madeni kuendelea kuwalipa wastaafu ambao ambao hawajachangia hata senti tano.
  5. Walilipwa malipo kamili bila mapunjo yoyote na mafao ya PSPF ni mafao bora, makubwa, manene, manono na mazuri.

Kama nilivyoeleza hapo juu, wastaafu hao wakiendelea kulipwa mafao ya PSPF ambayo ni mafao bora, makubwa, manene, manono na mazuri.

Yes ni wastaafu wote wa kuanzia mwaka 1999 kurudi nyuma. Watumishi wa serikali serikali waliopo kazini sasa walianza kuchangia mfuko wa PSPF, hivyo kwa wastaafu wapya, michango yao ilikuwepo

Kama nilivyoeleza hapo juu, walilipwa malipo yao yote. Swali labda liwe kama walihamishiwa PSPF bila kuletwa michango yao, jee walilipwa na fedha kutoka wapi?. Walilipwa kwa fedha kutoka vitegauchumi vya PSPF.
P

Umeeleza Vizuri sana na Kisomi,
Kwa Maana Kika Hoja na Jibu lake,
Ingependeza Wengine pia wajifunze!
Ahsante sana Nguli Pascal Mayalla
Uko Vema Mnoo pamoja na Vibwagizo/Vikolombezo vya hapa na Pale
 
Katibu mkuu wa wizara ya fedha Emmanuel Tutuba amesema serikali imeipa PSSSF kiasi cha tsh trillion 2.

Naye Mkurugenzi mkuu wa PSSSF Hosea Kashimba amesema kuanzia sasa wastaafu wote watalipwa mafao yao kwa wakati bila kuchelewa

Source: ITV habari

=====

Serikali, PSSSF wafikia muafaka juu ya deni la trilioni 4.66

December 22nd, 2021
*Kwa kuanzia wasaini makubaliano ya trilioni 2.17

*Katibu Mkuu: Deni linalipwa kwa utaratibu wa hati fungani maalum

*PSSSF: Tutaendelea kutoa huduma bora kwa Wastaafu

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Wizara ya Fedha na Mipango imetoa pongezi kwa serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa maelekezo ambayo yamepelekea kuhitimisha suala la muda mrefu kwa deni la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).

Kauli hiyo ilitolewa na katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Emmanuel Tutuba Desemba 22, 2021 jijini Dodoma katika sherehe ya utiaji sani makubaliano ya ulipaji wa shilingi trillioni 2.17 kwa PSSSF.

Bw. Emmanuel Tutuba alisema, “Sisi kama Wizara tumekuwa na majadiliano mara kadhaa na uliokuwa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) na sasa PSSSF juu ya kulishughulikia deni hili, baada ya kufanya uchambuzi wa kina juu ya suala hilo na kwa maslahi mapana ya wanachama wa Mfuko, Serikali imeamua kulipa deni hilo kwa kuanzia na shilingi trilioni 2.17, na deni hilo litalipwa kwa utaratibu wa hati fungani zisizo taslimu”.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Emmanuel Tutuba (wa pili kutoka kulia waliokaa) na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba (kushoto waliokaa) wakisaini hati za makubaliano ya ulipaji wa shilingi trilioni 2.17, anayeshuhudia kulia ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya waziri Mkuu, Prof. jamal Katundu.

Bw. Tutuba alisema katika hotuba ya Bajeti ya serikali ya mwaka 2021/2022 Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba alibainisha umuhimu wa wastaafu wa taifa letu ambao wamelitumikia taifa kwa uzalendo na uadilifu wa hali ya juu kupata stahiki zao kwa wakati. Katika kufanikisha hilo Waziri wa fedha aliahidi kuendelea kulipa madeni ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa kutenga fedha kwenye bajeti na kutoa hatifungani maalum.

Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa Jamal Katundu alitoa pongezi kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kulisimamia vyema na ukaribu suala la deni la PSSSF, ambalo linatoa faraja kwa wanachama wa PSSSF wakiwemo Wastaafu.
View attachment 2054092
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Emmanuel Tutuba (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba (kushoto) wakionesha hati za makubaliano ya ulipaji wa shilingi trilioni 2.17, anayeshuhudia kulia ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya waziri Mkuu, Prof. jamal Katundu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba alisema, “Kwa niaba ya Bodi ya Wadhamini, tunatoa shukrani nyingi kwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali yake kwa kuweza kushughulikia suala hili ambalo limekuwepo kwa muda mrefu na kupatiwa ufumbuzi chini ya utawala wake. Kwa upande wetu tunaahidi kuendelea kufanyakazi kwa weledi katika kutoa huduma bora kwa wanachama wetu”.

CPA.Kashimba alisema, makubaliano hayo ya 2.17 trilioni ambayo ni sehemu ya deni la Pre 1999 la 4.6 yatasaidia Mfuko kupata mapato yanayotokana na hati fungani hizo takribani shilingi bilioni 120 kwa mwaka ambazo zitauwezesha Mfuko kupata unafuu wa deni la pre 1999 na pia kuuwezesha kutimiza jukumu lake la msingi la kulipa mafao.

Katika sherehe hizo Serikali iliwakilishwa na Katibu Mkuu wa wizara ya Fedha Bw. Tutuba na kwa upande wa PSSSF iliwakilishwa na CPA. Kashimba. Pia ofisi ya Waziri Mkuu iliwakilishwa na Naibu Katibuy Mkuu, Prof. Jamal Katundu.
Hii sio hisani na wala sio jambo la kushangilia. Pesa hizi zilipaswa kutolewa miaka mingi iliyopita lakini serikali imeacha kwanza wastaafu wateseke, mwishoni kabisa ndio watoe hela wakati kuna baadhi ya wastaafu wamefuatilia mafao yao hadi wamefariki bila mafanikio yoyote. Ndio maana nchi hii imelaaniwa kwa sababu ya kudhulumu haki za msingi za wastaafu waliolitumikia taifa hili kwa uaminifu mkubwa ✍️
 
Back
Top Bottom