Unachafua hali ya hewa unapomtaja huyo pacha EL! Hivi maamuzi magumu ndio mambo ya Richmond?Hizo pesa kama wangejenga nyumba inelikuwa tayari imeezekwa inasubiri finishing. Tunatumia akili za namna gani watanzania? Lowasa hakukosea aliposema hatuna maamuzi kwenye mambo ya maana.CCM ni vichwa wazi. Mlilogwa na nani?
Mil 50 ingejenga zahanati 2.
Kwa mda wote aliokaa hotelini hizo hela zingetosha kumaliza uhaba wa madawati kwa shule zetu za msingi kwa ukanda wote wa pwani.
Serikali haiko makini kabisa kauli ya Pinda inajidhihirisha wazi, sijui tunakoenda. Kuitoa serikali madarakani 2015 inawezekana kabisa ila cha kuhofia ni haya mataifa ya nje wanaoitumia CCM kutuibia madini yetu na rasilimali zingine huku wanaCCM wachache wakinufaika na asilimia kumi.
Lakini kilio cha mnyonge kitasikizwa siku moja,hao wanaotumia vibaya madaraka watalia na kusaga meno ya.
Kwa kweli sijui wakati mwingine Waziri mkuu wetu Pinda anakuwaje, au ndivyo alivyo? au anafanya makusudi? kujifanya hajui kinachoendelea? tumuweke kundi gani? kila kitu kinachoendelea serikalini yeye kwake ni kigeni, inashangaza sana na inasikitisha sana Serikali hii, Waziri Mkuu kushindwa kujua kinachoendelea kwenye Serikali.
Tusubiri mwisho wake.