Serikali yafanya kufuru, Yatumia milioni 50/- kumlipia Waziri Hoteli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yafanya kufuru, Yatumia milioni 50/- kumlipia Waziri Hoteli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by drgeorge, Jun 7, 2011.

 1. d

  drgeorge Member

  #1
  Jun 7, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wandugu kuna tetesi kuwa waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania anaishi hotelini yeye pamoja na familia yake. Analipiwa kila kitu na serikali, kisa hakuna nyumba za watumishi wa umma. Nipo busy kidogo sijaweza kuchunguza na kufahamu kwa undani, kuna mtu anaijua hii ishu atupe details? Maana naona huu ni sawa na ufisadi tu
   
 2. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kama pesa ipo shida iko wapi?
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Jun 7, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu hizo habari nadhani zilikuwa kwenye magazeti ya jana ama leo. Mbona viongozi wengi tu wanaishi mahotelini na wanalipiwa na serikali wakiwamo majaji!! Pia kuna Mawaziri wamegeuza nyumba zao kuwa za mawaziri hivyo serikali inawalipa mihela mingi tu kwa kuishi kwenye nyumba zao.

  Dhambi ya kuuza nyumba za serikali haitamwacha salama yeyote aliyeshiriki katika kuzigawana hizo nyumba hadi kodi zetu ziwe zinatapanywa kwa kuwalipia mawaziri wapokaa hotelini kwa kukosa nyumba za serikali.

  Nitaburudika sana kama yeyote atakayeingia madarakani atazirudisha hizo nyumba kwa wananchi. Ufisadi si kuwalipia mawaziri hoteli, hiyo ni stahili yao kama hakuna nyumba ya serikali waziri akae hotelini (yeye na familia yake pamoja na mtumishi) hadi nyumba itakapopatikana. Ufisadi ni kuuza nyumba za serikali na kwenda kujenga mabanda huko Mbwewe na kujengaa mabweni pale kijitonyama. Hii ni dhambi
   
 4. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #4
  Jun 7, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli dhambi ya kuuza nyumba za serikali ni kubwa kuliko hata ya EPA! Hakika atakayezirudisha nyumba hizo nitamheshimu mpaka naingia kaburini!
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Jun 7, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kusema kweli hapo EPA ni cha mtoto. Kwenye kugawana nyumba za serikali ilikuwa kivumbi hadi watu wanakengeuka na kugawana kambi za polisi na magereza. Hiyo dhambi ndio inayoitafuna serikali. Kusema kweli kama kuna mtu atarudisha hizi nyumba kwenye mikono ya serikali nitamheshimu daima. JK alipokuwa anagombea kwa mara ya kwanza kulikuwa na tetesi kwamba atazirudisha hizo nyumba mikononi mwa serikali, nikapata faraja lakini hadi leo sijasikia kitu zaidi ya zile nyumba za serikali kubomolewa na kujengwa mahekalu (kwa kodi zetu - si wanaiba) ambayo yanapangishwa kwa midola!!

  Hivi sera ya CHADEMA kuhusu hilo la nyumba ikoje?
   
 6. l

  lutelemba Member

  #6
  Jun 7, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usiseme hivyo huu ni ufisadi wa hali ya juu. huwezi kuishi hotelini kwenye inci kama tanzania inayo zungukwa na masikini wengi hivyo. chekecha mbongo ndugu yangu. ila kwa sababu tunaongozwa na magamba ambao ni mafisadi hatuwezi kushangaa kuona hivyo.
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Jun 7, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mimi sishangilii ufisadi ila nasema tu kwamba ufisadi si kukaa Hotelini. Tusiangalie tulipoangukia tuangalie tulipojikwaa. Kugawana nyumba za serikali ndio kumeleta yote haya ya mawaziri kuishi hotelini kwa hiyo ufisadi ni kugawana nyumba za serikali. Nyumba zingekuwepo kisha waziri akaishi hotelini ingekuwa ni ufisadi, lakini nyumba hakuna sasa waziri akaishi guest au aishi Zanzibar awe anakuja kwa ndege kila asubuhi?

  Ni dhambi kubwa sana kuuza nyumba za serikali
   
 8. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Hata za kupanga hakuna?:confused:
   
 9. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #9
  Jun 7, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hawa mawaziri si wamejengewa nyumba bomba tu pale mikocheni, inamaana haziwatoshi au hizo nazo zishauzwa kinyemela?
   
 10. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ina Maana Lau Masha kagoma kuhama kutoka kwenye Nyumba Mpya ya Waziri wa Mambo ya Ndani...

  Kwahiyo ina Maana wanajenga Mpya ya Ndugu Waziri Wa Mambo ya Ndani Mpya...
   
 11. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #11
  Jun 7, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  nasikia hata makinda akiwa dar hiishi hotelini na ndio maana akaongeza kasi ya kujenga nyumba yake binafsi ili ahamie kuokoa hela za serikali!! na baraza lenyewe la mawaziri kila awamu linakuwa kubwa zaidi ya awamu iliyotangulia!!
   
 12. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #12
  Jun 7, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Kwa hali hiyo sishangai serikali kushindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi wa serikali

   
 13. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #13
  Jun 7, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  yani jana gazeti la nipashe lilipoti ni mawaziri kibao tu wanaishi kwa zaidi ya miezi 7 nakila chumba kinalipiwa kuazia 140 -280USD per day hapo ndio utajua wizi wa hali ya juu sana fanya tu kwa mahesabu ya haraka 7*30*420000 utapata jbu la 44,100,000 - 88,200,000Tsh kwa kila waziri je kama wanaishi nafamilia zao wanamiliki vyumba vingapi? je kuna mawazri na manaibu wangapi hawana nyumba? kweli serikali imeshindwa kweli kuona hasara inayopata kwa mtu mmoja? tu angalie tu kama engineer na doctors wanalipwa takehome (420,000-600,000)Tsh. Je tungeweza ajili watumishi wangapi?
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Jun 7, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Na kinachosikisha zaidi ni kwamba JK alitumia mabillioni ya kodi za wananchi kuwajengea nyumba maeleo ya Mikocheni, nyumba hizo wamezipangisha na wengine kuweka familia zao wakati wao wanaishi ktk majumba yao binafsi. Yasemekana hizi nyumba zilijengwa kama fidia ya ahadi aloitoa kwa wananchi kurudisha nyumba za serikali ambazo ziliuzwa wakati wa Mkapa.
   
 15. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #15
  Jun 7, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Yule bwana kaja kutufirisi tu, haoni aibu? Kwanza kazi ajui, analeta vimisemo vya pwani. Hawa mwisho wao wajongea, si kitambo!
   
 16. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #16
  Jun 7, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Si kweli! Kwanza sikubalina na philosophy yako kuwa ukishafanya kosa basi endelea tu kufanya makosa kwa sababu utakuwa na excuse ya ulipojikwaa.

  Hapa tunazungumzia governance. Hii ni moja mfano wa poor governance. You would expect serikali kukodisha nyumba ya kipanga ingekuwa cheaper. Unajua ni matendo kama haya yanayoonyesha kuwa serikali ina unlimited resources yet inashindwa kutoa huduma stahiri kwa mfano maslashi na mazingira mazuri kwa waalimu wa shule za msingi.
   
 17. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #17
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu kupanga nyumba sawa. Sina tatizo na hili. Tatizo ni kwamba hata huko kupanga ni ufisadi mtupu kwa kuwa watu wamegawana nyumba za serikali kisha wataipangisha serikali. Huu ni ufisadi tu. Hoja yangu ni kwamba kama kuna mtu arudishe hizi nyumba za serikali. Katika mkataba wa kugawana hizo nyumba kuna kipengele kwamba hutakiwi kuibadili hiyo nyumba hadi miaka 25 ipite lakini karibu zote zimebadilishwa na kwa hiyo wamvunja mojawapo ya masharti ya mkataba. Zirudishwe tu ili kuokoa kodi zetu
   
 18. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #18
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  katika hotuba ya kikwete alisema tusiwabane/wakamue wawekezake kiasi cha kuwafanya waishi mahotelini kwa bei za juu,
  mfulame **** bwana, kwa wawekezaji wahapana watumie hela vizuri kwa sisi tuishi hotelini au wanamiliki hizo hoteli wamekosa watega
   
 19. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #19
  Jun 8, 2011
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Amini usiamini nusu ya zile kota za Victoria kwa Kairuki,Mikocheni Light Industries na Masaki jeshini zinakaliwa na ndugu,watoto wa Mibaka uchumi... Hayo ni ya Dar... Je ya Dodoma? CCM kiama chao chaja...
   
 20. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #20
  Jun 9, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Huyu waziri ni mwizi kabisa, nashauri arudishwe huko alipotolewa, kwanza ubunge wake ni ule wa kupewa! Then ushirikiano wake kwa wenzake watia mashaka, uelewa wa nchi hii (haswa bara) upo duni sana, kifupi ni Hopeless na nashangaa kwa nin amepewa wizara nyeti km ile?
   
Loading...