Serikali yafanya kufuru, Yatumia milioni 50/- kumlipia Waziri Hoteli

Mimi nafikiri swala la ajira kwa viongozi wetu kama mawaziri, majaji, makatibu wa kuu na wengineo liwekewe utaratibu kwa kuwalipa mishahara na posho ya malazi kisha wao watajijua na liwekwe kikatiba ili viwango vya posho visije kuwa janga tena la kitaifa
 
kama nyumba hazitoshi mh. Nahodha ataishi hotelini hadi lini? ni vema kama nyumba hakuna atafutiwe hoteli nyenye hadhi ya chini huku hizo pesa tukizitumia kujenga nyumba!

CCM na mawazriri wake hamna kitu: kuenda kazini na kutoenda hamna tofauti, hivyo kama nyumba hazitoshi mimi sioni kwa nini asikae tu nyumbani kwake mpaka nyumba itapopatikana. Nafuu mshahara alipwe tu hata kama haendi kazini, kuliko hasara atazoingiza kwa kukaa hapo hotelinii.

Hivi wanapendea nini kukaa na kula misosi ya hotelini, halafu mke kamwacha Z'bar ili iweje - ale peke yake? hajisikii mpweke? au ndio mwanya wa kujitafutia changudoa.
 
Biashara ya real Estate in tz haijachukuliwa serious kabisa. watu wanajifanyia wanavyota ana hakuna anayewauliza chochote. Wenye majumaba hawalipi kodi yeyote huku wakiendelea kuwaumiza wananchi wa hali duni.

Nimekuwa nikihangaika sana kutafuta mkopo kwa ajili ya kujenga nyumba, ukienda benki unaambiwa dhamana na ni lazima iwe ni mali isiyohamishika. Ningependa kujua kama kuna benki zinazotoa mikopo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba and then use the same hse as collateral. Hii ingetusaidia wengi kuachana na hizi adha za wenye nyumba.

Jambo jingine ambalo lingewasaidia wananchi wanaofanya kazi ni mifuko ya hifadhi ya jamii (nssf,ppf) ni kuruhusu wanachama wake watumie michango yao kama dhamana kwa ajili ya kuomba mikopo ya ujenzi wa nyumba za kuishi. Watu wengi sana wanastaafu na wanajikuta hawana mahali pa kuishi, ingekuwa jambo la hekima kama watu wangeweza kutumia fedha zao ili kubadilisha maisha yao badala ya kuwafaidisha mafisadi ambao hawafanyi lolote jema kwa ajili ya taifa hili.
 
hii sio haki kabisa c bora ata wangempangishia nyumba,wana2mia hela nyingi sn kwa mambo yasio ya maana
 
Kwa hiyo ulitaka awe anaishi Namnani Guest House??

Tuseme hiyo ndio the only alternative ulonayo kwamba ukiondoa New Africa Zinazofuatia ni Guest? Hiyo aloikataa kwa kudai haina Samani... Yaani inakuingia akilini kuwa waziri mzima anataka hadi kitanda cha kulalia na mkewe anunuliwe na serekali?? Hadi stuli ya kukaribisha wageni? sasa na hili la ulinzi anachekesha kweli. Ye si ndo ana mapolisi wote?? Aun nyumba yenyewe ilikuwa manzese?? Si ndo vizuri alinde na majirani zake?? Ama kweli sisiem inatuzika hai!
 
Katika maisha yangu, nimeshakaa mahoteli mengi sana, ya kila hadi; 5-Star, Luxury Resorts hadi Guest Houses na hata nyumba za watu. Hoteli zote kubwa pale Dar nimeshakaa at one time or the other.

Kwa kweli, siwezi nikaelewa ni mtu wa aina gani ataweza kupenda kuishi kwenye hoteli kwa muda wa miezi saba! Nashindwa kusema ni ulimbukeni. Nashindwa kusema ni kiwewe cha cheo. Nataabika kuelewa thought process inayoweza kumfanya mtu apende kukaa kwenye chumba cha hoteli na kula yale machakula ya plastiki siku zote hizo.

Jamani, nyumba zote zilizopo Dar, zote ni mbaya kuliko chumba cha hoteli?
 
niliwahi kumsikia waziri wa nyumba akisema kodi ulipwa kwa miezi mi3 mwanzoni mwa mkataba na baada ya hapo malipo kila mwezi! lakini kaka emma,hakuna mwangalizi na sabab kubwa hata wao huko ndo wenye nyumba wanaotutesa sisi.! KAMA Vp NHC ipewe pia kazi ya kuregulate soko holela la nyumba sasa..au sivyo basi waunde chombo huru cha kuregulate na kikusanye kodi kwa kila mwenye nyumba MPANGISHAJI..Hii itasaidia. hali ni mbaya sana.!

Sheria inaweza kuwepo tena ni nzuri tu,tatizo huwa ni ufuatiliaji wa hizo sheria.Who cares wakati "wao" siyo waathirika wa hizi rents za ajabu ajabu?Inakera kwa kweli
 
Nani atufanyie taathmin ya gharama tulizo ingia kama taifa kwa kulipa gharama za makaazi ya viongozi akianzia kipindi kile cha uuzwaji wa nyumba za selekali.
 
nasikia hata makinda akiwa dar hiishi hotelini na ndio maana akaongeza kasi ya kujenga nyumba yake binafsi ili ahamie kuokoa hela za serikali!! na baraza lenyewe la mawaziri kila awamu linakuwa kubwa zaidi ya awamu iliyotangulia!!

Mkuu, mama Makinda labda amejenga nyumba ingine Dar kwasababu alipohama Upanga miwshoni mwa miaka ya tisini alikwenda kununua nyumba Kijitonyama.

Sasa labda hakai pale isipokuwa familia yake kutokana na sababu za kiusalama.
 
Biashara ya real Estate in tz haijachukuliwa serious kabisa. watu wanajifanyia wanavyota ana hakuna anayewauliza chochote. Wenye majumaba hawalipi kodi yeyote huku wakiendelea kuwaumiza wananchi wa hali duni.

Nimekuwa nikihangaika sana kutafuta mkopo kwa ajili ya kujenga nyumba, ukienda benki unaambiwa dhamana na ni lazima iwe ni mali isiyohamishika. Ningependa kujua kama kuna benki zinazotoa mikopo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba and then use the same hse as collateral. Hii ingetusaidia wengi kuachana na hizi adha za wenye nyumba.

Jambo jingine ambalo lingewasaidia wananchi wanaofanya kazi ni mifuko ya hifadhi ya jamii (nssf,ppf) ni kuruhusu wanachama wake watumie michango yao kama dhamana kwa ajili ya kuomba mikopo ya ujenzi wa nyumba za kuishi. Watu wengi sana wanastaafu na wanajikuta hawana mahali pa kuishi, ingekuwa jambo la hekima kama watu wangeweza kutumia fedha zao ili kubadilisha maisha yao badala ya kuwafaidisha mafisadi ambao hawafanyi lolote jema kwa ajili ya taifa hili.

Hili ni tatizo la kihistiria kwani biashara ya real estate ingeshamiri tangia kulipokuwa na benki ya nyumba ambayo ilifilisiwa mbele ya macho ya Basil Mramba.

Benki nazo haziwezi kukopesha hasa vijana fedha ili wajenge nyumba kwa sababu bado inaonekana ni risk kubwa.

Pia mfumo wa miundo mbinu kwa katikati ya jiji la dar ni mibovu sana labda nyumba nyingi zibomolewe.

Kinachotakiwa kwa serikali ijayo ni kuhakikisha kwamba yanatengwa maeneo mahsusi kwa ajili ya real estate development na nyumba zingine za watu binafsi lakini tu halafu kabla ya ujenzi kunakuwa tayri mahitaji yote muhimu kama umeme, maji, mifereji ya maji mchafu, taa za barabarani, hifadhi za maji na mambo menigne ya msingi yapo.

Si hivyo tu bali meudnelezo huo unakuwa unakwenda sanjari na ujenzi wa huduma zingine muhimu kama maduka, shule, hospitali, maofisi, mabenki na mengine hjiyo ndio inaitwa urban regeneration.
 
Wandugu kuna tetesi kuwa waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania anaishi hotelini yeye pamoja na familia yake. Analipiwa kila kitu na serikali, kisa hakuna nyumba za watumishi wa umma. Nipo busy kidogo sijaweza kuchunguza na kufahamu kwa undani, kuna mtu anaijua hii ishu atupe details? Maana naona huu ni sawa na ufisadi tu

ufisadi huu umesababishwa na Magufuli baada ya kuwauzia magabacholi nyumba zote za serikali kwa bei chee. katika huu UFISADI nadiriki kusema kwamba MAGUFULI ndiye mhusika mkuu, wala tusimlaume waziri aliyekubali kukaa hotelini na kuteketeza hayo mamilioni ya watanzania...tatizo ni bwana MAGUFULI.
 
hivi national housing zimejaa??

Hio ni ndoto sasa hivi kuwaza kuhusu nyumba za NHC

Lakini wanajenga mpya ambazo ni ghali na ukichukua mkopo zina riba kubwa sana.

Uporaji wa nyumba za NHC ulianzwa na viongozi wa serikali na BWM akaja kuuimarisha kwa kuanza na ile aliokuwa akiishi pale Upanga.

Sasa kama yeye alianzisha kampeni si ndio magufuli akaja kumalizia?
 
Kwa kweli dhambi ya kuuza nyumba za serikali ni kubwa kuliko hata ya EPA! Hakika atakayezirudisha nyumba hizo nitamheshimu mpaka naingia kaburini!

Mwaj si wewe peke yako.
Mimi atayerudisha ,atayeahifi kurudisha atapata kura z watanzania wengi sana ambao mpaka sasa hawajui wampigiani kura.
Hii dhambi y uuzaji ni zaidi ya KADHFA YA RADA,EPA NA ESCROE.

Kama Mungu aishivyo ,so long as viwanja haviamishiki kwenda nje n mabenki ya Uswisi,ninaapa lazma nyumba zirudi.

Waandishi wa habari naombeni hayavmaneno muweke reserve,nasema nyumba Zilizouzwa na magufuli kwa bei ya VITS NA IST zitarudi tuuu.

Nyumba zetuuu uuuuwi,zirudi zirudi zirudi!


Zilipouzwa hata ibilisi alikuja mezani akawashauri msiuze mkauza,malaika alishashauri mpak akachoka sasa ,wananchi tunasema Nyumba za serikali.zitarudi tu
 
Back
Top Bottom