Dkt. Tax ashiriki Hafla ya Kufunga Mafunzo ya Utayari Dhidi ya Dharura za Kemikali na Mionzi

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
20240315_105336.jpg

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax, Machi 14, 2024 ameshiriki katika hafla ya kufunga mafunzo ya utayari dhidi ya dharura za kemikali na mionzi, ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa. Sambamba na Ufungaji wa Mafunzo hayo Waziri Mkuu alizindua miongozo ya Kitaifa ya namna ya kukabiliana na majanga yatokanayo na kemikali na mionzi nchini.

20240315_105411.jpg

Mafunzo hayo yaliyofungwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yameshirikisha washiriki toka wizara mbalimbali za serikali ikiwa ni pamoja na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Taasisi zake.

20240315_105400.jpg
 
Back
Top Bottom