Serikali yaajiri walimu hewa(?) Ushahidi huu hapa...

Serikali yaajiri walimu hewa(?) Ushahidi huu hapa...

Daah! Kweli trust none. Usimwamini mtu!

Sikutegemea kama serikali hii ni ya kihuni namna hii.
 
Mkuu nimekukubali aisee,uko vizuri japo upo makini unaeza nawe pigwa ujue ahahaha mjini shule.
 
Katika ajira 4549 zilizotangazwa wiki iliyopita, baadhi ya majina yameajiriwa mara mbili katika vituo viwili tofauti. Ukifatilia katika matokeo yao ya NECTA kwa mwaka husika, unagundua kuwa namba hazikujirudia.

1.Hawa hapa walimaliza F4 mwaka 2010
View attachment 1085322
Matokeo ya NECTA ni namba moja tu
View attachment 1085323

2. Hawa walimaliza F4 2012
View attachment 1085324
Matokeo ya NECTA ni namba moja tu
View attachment 1085325

3. Hawa hapa mmoja alimaliza F4 2011 na mwingine 2015
View attachment 1085328
lakini jambo la kushangaza ni kwamba mwaka 2015 jumla ya idadi ya watahiniwa iliishia 0126 wakati huyu akionekana kuwa na namba 0131.
2011;View attachment 1085329

2015;View attachment 1085330

The Beautyful Ones Are Not Yet Born!
HAPPY MAY DAY!
Hii kitu niliiona mkuu nikashangaa tunaambiwa tumeajiri watu 100 kwa mf. Kumbe majina yako mawilimawili na yamekuwa counted kwenye hiyo 100. Na si mwaka huu tu...mara zote wanaposema wameajiri hii kitu me huwa naiona...sasa unashindwa kuelewa inakuaje mifumo ya serikali haioni hiki kitu...hii ni hewa kwelikweli.

#Muda wangu wa kuwa madarakani bado haujaisha(naripoti kutoka Sokoine-Mbeya)
 
Hongera sana mkuu...
Hongera Hongera..

Mimi nadhani hapa kuna mambo mawili ,aidha kuna wapigaji wamepiga dili ili hiyo mishahara wachukuage wao..

Au wameajiliwa watu wachache ila wanataka ionekane wameajiliwa wengi..

We ni noma, unastahili Tuzo ya mwana jF bora Mwezi huu japo ndiyo kwanza mwanzo..

Nadharia yako namba 2 ndio iko sahihi.
 
Wanaoajiriwa wanakwenda vituo gani.....?
 
Naomba ninene kidogo kwenye hizi ajira.

Kwanza kabisa niunge mkono hoja ya mwanzilishi wa huu uzi kwa kuchangia kama ifuatavyo

Hizi ajira zimetoka kwa namna ambayo kiasi kwamba ukiamua ufuatilie kiundani utapata maswali mengi kuliko majibu. Tumeona kuna watu mbali mbali wameajiriwa mara mbili tena katika vituo viwili tofauti na wengine wameajiriwa nje ya vigezo vilivyokuwa vimewekwa kwenye tangazo la ajira.

Ninachojiuliza je hawa wanaopangiwa vituo mara mbili ni hewa nyongine inaingia serikalini??

Je ni wale ambao wameajiriwa kwa michongo ndo maana imepelekea majina yao kuajirika mara mbili??

Ni kwanini katika awamu hii kipengele cha vyuo walivyosoma hakijawekwa tukajua na miaka yao ya kumaliza?? Kwanini wafiche wakati mara kadhaa wamekuwa wakikiweka hiki kipengele??

Hii yote inadhihirisha ni kwa namna gani kuna madudu kwenye hizi ajira ambayo yamefanyika.

Hapa pichani ni mmoja kati ya waliopangiwa vituo mara mbili ambapo kituo cha kwanza kapangiwa iringa kingine kigoma. Kilichofanyika wameacha majina yale yale, center number yake ya shule (O level) ile ile isipokuwa wamebadili mwaka wake wa kuhitimu masomo ambapo mwanzoni inaonyesha kamaliza kidato cha nne 2012 na kamaliza kidato tena cha nne mwaka 2013 NOTE:majina ni yale yale. Nimewawekea picha hapa ili muweze kuitazama
Naomba mrejee kwenye jina namba 3244 na 3245 kwenye ajira za waliopangiwa kwenda sekondari. Naomba pia mrejee katika jina namba 3251 alafu mje tujuzane hapa maana mhusika tajwa kwenye hiyo namba amemaliza kidato cha nne 1994 je kwa sasa atakuwa na umri gani na ataitumikia serikali kwa miaka mingapi(ikumbukwe watu wa zamani walikuwa wanasoma wakiwa wakubwa kidogo)
View attachment 1085454
MnHhh....

Kuna namna hapa aisee...!??
 
Sio siri huu ni weledi wa hali ya juu.
Sio siri, mimi nilona mismatches nyingi lakini sikuwa na interest ya kudukua index no na kutafiti haya majina, na hata ukisoma majina ya baadhi ya hizi ajira kuna alarm inalia kichwani selection na vyuo nk.
In short mamlaka wasipotoa ufafanuzi, ntaaamini kuwa kuna dhamiri flan flan nyingi tu ambazo si njema kwa ustawi wa jamii yenye usawa.
 
Kuna wengi watakua ni hewa...... Naingia mzigoni nitachambua jina moja baada ya jingine...... Soon mrejesho utakua hapa
Fanya hivo mkuu.
Ajira za uhamiaji mwaka 2014 watu takribani 75 zilikuwa hivi hivi watu na watu wao na mpaka wakaamua kuitisha upya kwa aibu.
People are enriching themselves and enjoying the National cake.
No one cares as this guy in JF
 
Back
Top Bottom