Serikali yaainisha Mpango wa Kusaidia Wachimbaji Wadogo Nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,030
974
Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde ameainisha mpango wa serikali wa kusaidia utatuzi wa changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo nchini.

Mh Mavunde ameyasema hayo leo wakati akijibi swali la Mh Dkt. Christine Gabriel Ishengoma Mbunge wa Viti Maalum aliyetaka kujua mpango wa serikali kuwasaidia Wachimbaji Wadogo wa Madini Wilaya ya Ulanga.

Akijibu awali hilo Waziri Mavunde amesema Mpango wa Serikali kuwasaidia wachimbaji wadogo nchini wakiwemo wachimbaji wa madini wa Wilaya ya Ulanga unahusisha mambo yafuatayo:-

(i) Kuwekeza zaidi katika utafiti wa kina kugundua uwepo wa madini katika maeneo mbalimbali ili kuwaongoza vizuri wachimbaji wadogo;

(ii) Utoaji wa Leseni za uchimbaji kwa wachimbaji wadogo;

(iii) Kutoa Elimu ya matumzi ya teknolojia sahihi ya uchimbaji ili kuongeza tija;

(iv) Huduma ya uchorongaji kwa gharama nafuu kupitia Shirika la Madini Tanzania (STAMICO);

(v) Upatikanaji wa mikopo nafuu kwa wachimbaji kupitia Benki mbalimbali na Taasisi za fedha.

(vi) Fursa ya ukodishaji wa mitambo na vifaa chini ya usimamizi wa STAMICO kupitia makampuni yaliyoingia makubaliano(MoU) na STAMICO.

WhatsApp Image 2024-05-09 at 11.38.56.jpeg
 
Back
Top Bottom