Serikali ya Tanzania yatoa tamko, yamlilia Gaddafi

Mmeshasahau na hili?

article-2051361-0E74E80600000578-38_634x440.jpg



Synonymous with terrorism: A young Gaddafi, right, is seen in an undated photo with notorious Ugandan leader Idi Amin, whom he helped to attack Tanzania in 1978
 
Lakini tamko alilotoa ni tamko la Tanzania kama nchi, sio la kwake...na huo ni msimamo wa Tanzania kama nchi, na sio wa kwake yeye. Kama tamko lilikuwa lege lege, basi kwa kuwa limetoka kwenye nchi yenye msimamo lege lege, na sio waziri lege lege!

Membe is one of bogus Ministers of JK!

Membe ndiye aliyemwambia Balozi wa Libya ashushe Bendera ya Baraza la Mpito kwa madai kuwa amekiuka sheria za UN!
Kwa sasa Membe anataka kutuambia nini? Baada ya kifo cha Ghaddafy leo ndiyo anawatambua waasi wa Libya?Membe aache unafiki na longolongo zake bana!
 
Membe is one of bogus Ministers of JK!

Membe ndiye aliyemwambia Balozi wa Libya ashushe Bendera ya Baraza la Mpito kwa madai kuwa amekiuka sheria za UN!
Kwa sasa Membe anataka kutuambia nini? Baada ya kifo cha Ghaddafy leo ndiyo anawatambua waasi wa Libya?Membe aache unafiki na longolongo zake bana!

Sijakuelewa! Hakuwa sahihi kuwaambia kushusha bendera ama?
 
Inaonekana kuna kitu sikielewi hapa. Nilivyokuwa nikiangalia TV zote jana ikiwemo TV ninayoiamini zaidi ya Al-azeera niliona halaiki ya walibya wakishangilia baada ya kupata habari za kifo cha kiongozi wao aliyewatawala kwa miaka zaidi ya arobaini. Walivyoonekana hakuna aliyeshinikizwa kwenda mabarabarani kusherehekea taarifa za kifo hicho. Nikifananisha muitikio wa wananchi wakati wa kifo cha Nyerere miaka takriban kumi iliyopita napata picha tofauti kabisa kwani sehemu kubwa ya taifa letu iliomboleza kwa vilio na mpaka leo watu bado wanaomboleza.

Watetezi wa Ghadafi ambao, kwa bahati mbaya wengi ambao niwewasikia siyo walibya, wanawalaani wananchi wa Libya kwa kushangilia kifo cha kiongozi wao waliyemfahamu kwa zaidi ya miaka arobaini. Wengi wa watetezi wanajenga hoja zao kwa kutoa mifano ya maendeleo ambayo Ghadafi aliwaletea walibya yakijumuisha ujenzi wa miundo mbinu, nyumba za kuishi na urahisi wa maisha aliowaletea.

Majibu ambayo sijapata ni:-
  • Je ina maana watetezi wa Ghadafi kama Membe wanamjua huyu jamaa kuliko wale niliowaona wakishangilia habari za kifo chake kwenye mitaa ya miji mbalimbali ya Libya?
  • Je kinachowasukuma hawa watetezi wa Ghadafi ni maslahi ya walibya au ni maslahi yao na ya nchi zao?
  • Je ni kweli kuwa mtu aliye nje ya Libya anaweza kujua watu wa Libya wanataka nini zaidi ya walibya wenyewe?
  • Je ina maana wananchi wa Libya ni wajinga kiasi cha kutojua mambo mema ambayo huyu rais wao waliyemuua aliyafanya kwa muda wote ambao alitawala?
  • Je kiongozi akitumia pesa za nchi kwa maendeleo ya miundombinu na vitu kama nyumba, hospitali, shule, vyuo vikuu inatosha kumpa kiongozi uhalali wa kuwatawala watawaliwa anavyotaka yeye kwa muda anaotaka yeye?
Mimi nadhani kuna kitu ambacho hawa watu wa Libya wanakijua kuhusu kiongozi kinachowafanya washangilie kama walivyofanya jana. Haiwezekani mtu mzuri kiasi hicho kama ambavyo tunaaminishwa na akina Membe akafa halafu watu wakashangilia.
 
Membe hana lolote,ni mnafiki.anajikomba kwa watz wanaompenda gadafi,hasa wale waliofaidika na gadafi kwa kujengewa majengo ya kuabudia akifanya hvyo kwa kuomba support ili atimize malengo yake ya 2015...shame on you nyoka wa mdimu.
 
Who is Membe by the way?

Is he a significant figure? at what decimal point may be?

Is he worthy of someone's attention?

Someone HELP plz
 
Mbona hawakwenda kumsaidia huyo 'Kadafi' wao...hata bendera sijaona zikipepea nusu mlingoti (kuonesha kuguswa na kifo chake)!
 
Namshangaa sana waziri wetu. Kwa wenzetu katika masomo ambayo lazima mwanadiplomasia apitie kabla ya kuruhusiwa kuiwakilisha nchi yake sehemu yoyote, ni somo la The Price, by Niccolo Machiaveli, circa 15th Century.

Bila kujalisha kuwa Ghadaffi alikuwa ni jitu katili lililoua raia wake (Libyans reflect the cruelty of Gaddafi 2011 - YouTube), bila kujalisha kuwa alikuwa mentally unstable (Muammar Gaddafi Speech To United Nations Sept 23, 2009 pt.1 - YouTube), bila kujali kuwa alikuwa malaika au shetani - THE MAN IS DEAD!!! Libya is alive - and still a force to reccon with in African affairs.

Sasa hii strategy ya taifa letu ya kutaka afufuliwe itatufikisha wapi?

Hata juzi kwenye mazishi ya Mchina, eti "Hili ni jambo la kawaida linaweza kumtokea mtu yeyote". Kweli jamani? Haya ndiyo mambo ya kusema kwenye msiba? Alishindwa nini kusema tu kuwa "Serikali ya Tanzania haitalala mpaka wauwaji watapopatikana na kuangukiwa na nguvu zote za sheria"?

 
Membe ni bogus kabisa.
Kama Tanzania haijafurahishwa na kifo cha Ghaddafi, inamaana Tanzania ilikuwa na imeweka mkono wake pale Libya ikimsaidia Ghaddafi lakini baada ya kuzidiwa wanaanza kulalama. Membe atueleze Watanzania Ghaddafi aliwalipa kiasi gani cha pesa hadi Membe amlilie kias hicho- Damn.

Kama aliuwawa akiwa mikononi mwa Wanajeshi, atuambie yeye Gaddafi ameua wangapi kwa mikono au kinywa chake. Je ni lini Membe alishawahi kutoa malalamiko kupitia vyombo vya habari jinsi Watanzania wanavyo uwawa wakiwa mikononi mwa vyombo vya usalama. Mfano Nyamongo Tarime na migodi mingine? Aache ujinga, hayo masikitiko ni ya kwake yawezekana Membe alikuwa na masilahi binafsi.

Kama shamrashamra za waasi ni zamuda mfupi, membe apeleke majeshi kupigana na waasi.- Damn.
 
membe nae awe mkuu wa kaya hebu usituchefue na hayo majina vilaza wako km unamtaka sana mpeleke nyumbani kwako ukamuone ww na mkeo 2015 dr wa ukweli
 
Membe mlikuwa wapi kuyasema hayo kabla?Acheni unafiki kuonekana wema mbele za watu.Unafiki huo wa viongozi ndo umeifikisha nchi hii hapa ilipo.
 
Waziri we2 wa mambo ya nje,amekuwa akitoa matamko ya kutokuitambua selikari ya mpito ya Libya,na leo kasema haitambui.Hivi huu sio unafiki kweli ,ukizingatia Gaddafi mwenyewe kashauawa na haohao ambao hawatambui je yeye anapingana na nchi nyingi za Afrika ambazo tayari zinaitambua NTC na zote zikiwa katika umoja wa Afrika....tuelimishane jamani.Nawakilisha.
 
wanafiki wakubwa hao yn wasubiri apigwe hadi auwawe hlf wajidai wanamlilia, UNAFIKI KM HUO MUNGU HAPENDI. NA ZAMU YA HY M.K.WERE INAKUJA si anajidai kupimapima mafuta ngoja aanze kuyachima rasmi aone kitu atafanywa.

comoro walipeleka majeshi kumlinda raisi wa nchi hiyo na wakafanikiwa je kama kweli walikuwa na mapenzi mema kwanini hawakupeleka majeshi libya...bila shaka ni unafiki wao na wanatambua sasa ni zamu yao
 
Back
Top Bottom