Serikali ya Tanzania yatoa tamko, yamlilia Gaddafi

Waziri we2 wa mambo ya nje,amekuwa akitoa matamko ya kutokuitambua selikari ya mpito ya Libya,na leo kasema haitambui.Hivi huu sio unafiki kweli ,ukizingatia Gaddafi mwenyewe kashauawa na haohao ambao hawatambui je yeye anapingana na nchi nyingi za Afrika ambazo tayari zinaitambua NTC na zote zikiwa katika umoja wa Afrika....tuelimishane jamani.Nawakilisha.
Msimamo anaoonyesha waziri Membe ni wa serikali yake ya kinafiki na kiuwaji akijua kabisa watu wanaweza kuwageuka kama Libya. Huyo anaogopa kuvuli anajua kabisa akishabikia next on line atakuwa ni yeye, hao maghamba wana wasiwasi!!!!!!!!!!
 
Akihojiwa na clouds fm msimamo wa tanzania juu ya kuitambua au kutoitambua libya mh membe anasema hatuitambui ntc kwakuwa sio serikali bali ni kikundi cha wapiganaji, kweli huu ndio msimamo wa watanzania au wa membe?

Swali la kitoto unamuuliza nani? Wewe unadhani watanzania msimamo wao ni upi na je, msimamo wa Tanzania hutolewa na nani kama siyo na serikali? Sasa serikali imetoa msimamo unaanza kuendesha propaganda kwa kuuliza maswali tasa. Sisi watanzania msimamo wetu umeshatolewa na serikali ambayo msemaji wake halali katika suala hili ni Waziri Membe. Kama una msimamo wako tofauti hatuna cha kukusaidia maana unazungumzia kile ambacho wewe binafsi ungetaka kitokee na siyo kwa maslahi ya taifa.
 
Hili swali nimejiuliza siku nyingi sana Kwa nini hakuondoka watu wake walipotoka barabarani kuonesha kutaka reforms? Alikuwa jasiri kiasi gani hadi kutothamini maisha yake alioona hawezi tena kupambana?

Mimi ninapenda wazo la kuwa na United States of Africa ili tuwe na nguvu za kiuchumi na kuwa na sauti moja yenye nguvu tofauti na sasa lakini approach inayotumiwa na viongozi wetu ndio inatuangusha tusifike huko ni imani yangu siku moja tutaungana.

Kuhusu tamko bado tuna matatizo ya kuyumba kimtazamo hilo linatugharimu na wenzetu wanatumia sana udhaifu wetu huu kutunyonya.
Sala yangu kwa Mungu waafrika tuungane haraka ili tujikomboe kiuchumi.
 
Marehemu Gaddafi aliwahi kutupatia Tanzania masaa 24 tuondoe majeshi yetu Uganda vinginevyo angetupatia
kipigo ambacho tusingekisahau wakati wa vita dhidi ya Nduli Idd Amin Dada.

Nimeona documentary ya uongozi wa Gaddafi iliyotengenezwa na TBC1, hawaku-mention hili tukio muhimu
sana katika historia ya nchi yetu na udhalimu wa Gaddafi. TBC1 wame-copy kila kitu Al Jazeera.

Gaddafi was a tyran he deserve what he got, viongozi wa kiafrika lazima waanze kuambiana ukweli huko AU.
 
Akihojiwa na clouds fm msimamo wa tanzania juu ya kuitambua au kutoitambua libya mh membe anasema hatuitambui ntc kwakuwa sio serikali bali ni kikundi cha wapiganaji, kweli huu ndio msimamo wa watanzania au wa membe?

Mwacheni akae na msimamo wake, ila asituhusishe waTanzania.
 
Lakini tamko alilotoa ni tamko la Tanzania kama nchi, sio la kwake...na huo ni msimamo wa Tanzania kama nchi, na sio wa kwake yeye. Kama tamko lilikuwa lege lege, basi kwa kuwa limetoka kwenye nchi yenye msimamo lege lege, na sio waziri lege lege!

Na hapo kwa tamko hilo linalotudhalilisha ndio mataifa mengine yanapothibitisha kuwa watanzania ni vihiyo tusioelewa mambo. Viongozi wetu wanatudhalilisha kitaifa na kimataifa. Inasikitisha
 
He had too many masters to serve at the expense of his own people. How could he be able to support almost all rebel movements in Africa? What was he thinking about power and the rule of law? As a matter of fact am not celebrating his death but He created chaos and unfortunately,the same chaos he created has made him fall down.
 
Gaddafi-%26-Amin-in-Gulu-1973.gif



An original photograph; backside text reads: Al Haji Amin (centre) is introducing senior militaryofficers to his brother Col. Gaddafi, Chairman of the Revolutionary Command of Arab republic of Libya, shortly on arrival at Gulu Airfield [northern Uganda] to perform the official handing over of aircrafts to Uganda Airforce, March 3, 1974,to be used for attacking Tanzania.
 
Magazeti ya leo ya An Nuur na Al huda hayajaripoti chochote kuhusu kifo cha Gaddafi, kama vile hawajui kilichojiri!
 
NTC, Imetakiwa iunde serikali ya umoja wa kitaifa itayohusisha pande zote zinazohasimiana hilo ni agizo la AU, hivyo kwa vile Tanzania ni mwanachama wa AU hawazi kupingana na AU.
 
Inaonekana kuna kitu sikielewi hapa. Nilivyokuwa nikiangalia TV zote jana ikiwemo TV ninayoiamini zaidi ya Al-azeera niliona halaiki ya walibya wakishangilia baada ya kupata habari za kifo cha kiongozi wao aliyewatawala kwa miaka zaidi ya arobaini. Walivyoonekana hakuna aliyeshinikizwa kwenda mabarabarani kusherehekea taarifa za kifo hicho. Nikifananisha muitikio wa wananchi wakati wa kifo cha Nyerere miaka takriban kumi iliyopita napata picha tofauti kabisa kwani sehemu kubwa ya taifa letu iliomboleza kwa vilio na mpaka leo watu bado wanaomboleza.

Watetezi wa Ghadafi ambao, kwa bahati mbaya wengi ambao niwewasikia siyo walibya, wanawalaani wananchi wa Libya kwa kushangilia kifo cha kiongozi wao waliyemfahamu kwa zaidi ya miaka arobaini. Wengi wa watetezi wanajenga hoja zao kwa kutoa mifano ya maendeleo ambayo Ghadafi aliwaletea walibya yakijumuisha ujenzi wa miundo mbinu, nyumba za kuishi na urahisi wa maisha aliowaletea.

Majibu ambayo sijapata ni:-
  • Je ina maana watetezi wa Ghadafi kama Membe wanamjua huyu jamaa kuliko wale niliowaona wakishangilia habari za kifo chake kwenye mitaa ya miji mbalimbali ya Libya?
  • Je kinachowasukuma hawa watetezi wa Ghadafi ni maslahi ya walibya au ni maslahi yao na ya nchi zao?
  • Je ni kweli kuwa mtu aliye nje ya Libya anaweza kujua watu wa Libya wanataka nini zaidi ya walibya wenyewe?
  • Je ina maana wananchi wa Libya ni wajinga kiasi cha kutojua mambo mema ambayo huyu rais wao waliyemuua aliyafanya kwa muda wote ambao alitawala?
  • Je kiongozi akitumia pesa za nchi kwa maendeleo ya miundombinu na vitu kama nyumba, hospitali, shule, vyuo vikuu inatosha kumpa kiongozi uhalali wa kuwatawala watawaliwa anavyotaka yeye kwa muda anaotaka yeye?
Mimi nadhani kuna kitu ambacho hawa watu wa Libya wanakijua kuhusu kiongozi kinachowafanya washangilie kama walivyofanya jana. Haiwezekani mtu mzuri kiasi hicho kama ambavyo tunaaminishwa na akina Membe akafa halafu watu wakashangilia.

Membe na jk walikuwa na masilahi binafsi kutoka kwa gadafi. Tulisikia jinsi membnde alivyokuwa anataka kukwapua mapesa kutoka kwa gadafi kwa kisingizio cha kupeleka kiwanda kwenye jimbo lake la uchaguzi. Ndoto zake za kupata hizo pesa imetumbukia nyongo sasa analalama ovyo na kutoa matamko yasiyokuwa na tija kwa nchi kwa mtazamo wake binafsi na boss wake jk. Sasa sijui serikali mpya ya libya itakapopandisha bendera yake hapa nchini watajisikiaje au watatuambia nini?? Viongozi wetu wanawaza kwa kutumia masaburi
 
Moammar Gadhafi and Idi Amin : Lessons From History Specifics:

In 1972, Idi Amin and Moammar Gadhafi struck up a friendship. The result was a downward spiral.

Following Idi Amin's government overthrow in Uganda in 1979, Moammar Gadhafi welcomed him and his entourage into Libya in which the Libyan government took care of them for a number of months. On the little acknowledged occasion relating to Idi Amin threatening to walk to the Kingdom of Saudi Arabia if Moammar Gadhafi did not supply him safe passage to the holy land of Sunni Islam, Idi Amin had felt betrayed by Moammar Gadhafi simply because Moammar Gadhafi needed to be the Chairman of the OAU (Organization of African Unity) in 1979. To boost his chances of finding elected to the Chairmanship of the OAU, Moammar Gadhafi had to "befriend" Julius Nyerere, the President of Tanzania who was accountable for Idi Amin's ouster from power in Uganda.In 1972, Idi Amin and Moammar Gadhafi struck up a friendship. The result was a downward spiral.
 
Waoga wakubwa hawa hata aibu hawana,kipindi vita inaendelea mbona hatukuona ambaye alijitokeza kumsaidia dhidi ya NTC? Leo wanaona umuhimu gani wa kuongea huo upuuzi wao? Nasubiri tamko la BAR-KWATA.
 
Haya sijui kwetu itafika lini! yani watu wa dar wanatuangusha sn! yani wapo baridi kama maji ya mto ruvu hawafurukuti (uswahili tu)
 
Mzee Mwanakijiji, with due respect, kuishi kwenye nchi za watu kwa muda mrefu sio justification of thinking like them!. Naamini unakijua kilichomtoa Ghadafi na sio Western symphathy kwa watu wa Libya, I'm very sure you know better the games people play on us!.

Beggars kama Tanzania cannot be chooses, bendera tumezishushia mioyoni kwa kuwahofia mabwana zetu (UK, US na hao mabwana wa vita) wasije wakatushukia!.

Ndio maana nikacomment sijapenda Ghadafi alivyouwawa, so do Saddam na hata Osama!.

All the same. Wewe na membe mna mawazo yanayofanana. mnawaza kwa masaburi. endeleeni kumtambua gadafi
 
Sina masikitiko yoyote kwa kifo cha Gaddafi,alichagua kuuwawa kama kibaka alipokataa matakwa ya wananchi wake kuachia madaraka. Hakuwa na busara kabisa,amemwaga damu nyingi ya walibya kwa uroho wake wa madaraka. Ni funzo pia kwa vyama vikongwe kama CCM,kwamba uroho wao wa kutumia hila,wizi wa kura na vitisho,siku tukiingia mtaani tutamaliza mchezo kama walivyomuona Gaddafi jana anageuzwa mpira wa kona!
 
Huyu jamaa si ndiye aliyemsaidia Idd Amini kwenye Vita yetu na Uganda - kwa maneno mengine alitaka kuangusha Dola yetu chini ya Mwalimu? au tumesahau watanzania kama ilivyo kawaida yetu? Leo hii huyu jamaa anakuwa mzuri kiasi cha kuzuia tusisherekee anguko lake na utawala wake wa udikteta?
 
Back
Top Bottom