Serikali ya Marekani izuie mara moja uzinduzi wa Kipindi cha ROYAL TOUR cha Rais Samia nchini humo kushinikiza Utawala Bora nchini

The lost

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
2,695
8,209
Nipo katika hatua za mwisho za kuweka zuio la kisheria la kuitaka Serikali ya Marekani kuzuia Uzinduzi wa kipindi cha ROYAL TOUR ambapo uzinduzi huo utafanywa na Rais Samia mwenyewe huko Marekani.

Katika malalamiko yangu yatakuwa kuikumbusha serikali ya Washington DC kuwa uvunjaji wa Demokrasia nchini umefikia hatua mbaya zaidi katika utawala huu.

Mazingira ya siasa kwa vyama vya upinzani yamekuwa ya kukatisha tamaa na kuogopesha zaidi chini ya utawala wa Samia. Kama mtanzania nina wajibu wa kukemea mabaya ambayo nayaona yanaweza kuvuruga amani ya taifa letu. Mambo makuu ambayo Jumuiya ya kimataifa inapaswa kujua kuwa yanatendeka Tanzania ni pamoja na:

(1) Uzuiwaji wa mikutano na mikusanyiko ya ndani ya vyama vya upinzani kinyume na taratibu na sheria za nchi.

(2) Serikali na Bunge la JMT kutoheshimu Katiba ya vyama vya upinzani na sheria ya uwakilishi Bungeni ambapo Serikali imekataa kuwaondoa Wabunge wasio na chama Bungeni.

(3) Serikali kukamata na kuwabambikia makosa yasiyo na dhamana viongozi wa upinzani.
 
Jaji Mutungi yule Msajili ametangaza mazungumzo kutafuta muafaka lakini! Hope mambo yatakaa sawa tu.
 
Minyanyeni, uaeni, ilimradi nchi mmefungua, beberu hana shida! Huwa wanaanza choko choko pale tu mnaposhikana mikono kwenye sahani moja.

Ilimradi nchi iko wazi, beberu hana shida na haswa zinapochotwa huku kupelekwa kwake kwa ziara hiyo, bado milango imefunguliwa kwa wazee wa kuhifadhi minoti huko pia, beberu haimhusu mikutano wala mikusanyiko, utawala bora ili iwe nini?

Hili ni mimi sasa, hawa wapinzani sio wanasiasa?
 
Who cares. In this modern world is all about interests.
Americans are the world "champion" of democracy ----- in this case we expect them not to be mum, Atleast they have to take their influential opportunity while she is in there to tell her the truth obout deteriorating democracy in Tz by her Government.
 
Kampuni inayofanya recording ni PBS ambayo inatumia pesa za walipa kodi wa Marekani na mhusika mkuu kwenye hili zoezi anaitwa Peter Greenbeck na mashinikizo Twitter Republic yameanza rasmi. Sijajua hayo mashinikizo yatakuwa na mafanikio gani.
Asipokubali basi kwa jinsi ninavyowajua wazungu wataanzia hapo hapo na mpango mzima wa "tour ya kimalkia " itakuwa imechafuka na hivyo kuwa meaningless.
 
Kampuni inayofanya recording ni PBS ambayo inatumia pesa za walipa kodi wa Marekani na mhusika mkuu kwenye hili zoezi anaitwa Peter Greenbeck na mashinikizo Twitter Republic yameanza rasmi. Sijajua hayo mashinikizo yatakuwa na mafanikio gani.
Tusubiri na tuone.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom