Vyombo vya habari USA vina haki kikatiba kutangaza lolote umewahi kusikia gazeti lolote au chombo chochote kimefungiwa ! hakuna kitu kama hichoNipo katika hatua za mwisho za kuweka zuio la kisheria la kuitaka serikali ya Marekani kuzuia Uzinduzi wa kipindi cha ROYAL TOUR ambapo uzinduzi huo utafanywa na Rais Samia mwenyewe huko Marekani.
Katika malalamiko yangu yatakuwa kuikumbusha serikali ya Washington DC kuwa uvunjaji wa Demokrasia nchini umefikia hatua mbaya zaidi katika utawala huu.
Mazingira ya siasa kwa vyama vya upinzani yamekuwa ya kukatisha tamaa na kuogopesha zaidi chini ya utawala wa Samia. Kama mtanzania nina wajibu wa kukemea mabaya ambayo nayaona yanaweza kuvuruga amani ya taifa letu. Mambo makuu ambayo jumuiya ya kimataifa inapaswa kujua kuwa yanatendeka Tanzania ni pamoja na:
(1) Uzuiwaji wa mikutano na mikusanyiko ya ndani ya vyama vya upinzani kinyume na taratibu na sheria za nchi.
(2) Serikali na bunge la JMT kutoheshimu katiba ya vyama vya upinzani na sheria ya uwakilishi bungeni ambapo serikali imekataa kuwaondoa wabunge wasio na chama bungeni.
(3) Serikali kukamata na kuwabambikia makosa yasiyo na dhamana viongozi wa upinzani.