Hizi ni baadhi ya ahadi kati ya 70 alizotoa Rais Kikwete alizozitoa ;
1.Kujenga barabara za juu katika jiji la Dar es Salaam ili kupunguza msongamano wa magari,
2.kujenga majengo ya biashara maarufu kama Machinga Complex mawili katika kila wilaya za mkoa wa Dar es Salaam.
3.kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya Ziwa,
4.kujenga hospitali katika kila jimbo,
5.kulipa madeni ya Chama cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)
6.Kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) Ruvuma
7.Kununua meli kubwa katika Ziwa Victoria kuliko MV Bukoba iliyozama Mei 21, 1996
8.Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa,
9.Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa, ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
10.Kuboresha barabara za Igunga Tabora, Njombe- Makete, Musoma Mto wa Mbu. 11.Kukarabati barabara ya Moshi-Arusha, na Singida-Dodoma.
Unaweza kutuambia zimefikia wapi?Au zimeota mbawa?Na naona muda wake umeisha!
Mtakuja na ngonjera zipi nyingine