Serikali ya China na Tanzania zatofautiana ujenzi wa bandari Bagamoyo

mjingamimi kwani magari ya usafiri yanamilikiwa na Serikali. Unajua kwamba serikali nyingi tu duniani haziendishi bandari zao badala yake zinaendeshwa na watu binafsi na serikali inatoza kodi. Hayo mambo ya mali za umma yalishakufa enzi za ubinafsishaji zama za utawala wa Mwinyi na kukamilishwa na Mkapa!
 
chige unatwanga maji kwenye kinu ndugu yangu. Hata hivyo nakupongeza kwa uliyoyaeleza kwani huo ndiyo Uzalendo. Tatizo letu ni makengeza ya akili tuliyonayo kwamba utajiri ni laana. Kuna watu watasema "waende zao hatuna shida na bandari Bagamoyo" lakini wanasahau kwamba uwekezaji huo hautachukua hata senti ya mtanzania tofauti ya kile kiwanja cha ndege na duka madawa vilivyojengwa la kule nyumbani!!
hivi huwezi kuandila bila kuhushisha hivi vitu vya kijinga mkuu
 
wachina waliingia mkenge wakasaini mikataba 17 na jk kwa sababu wanazojua wao ila magu kawastukia atapiga chini mikataba yote kwa maslahi ya nch na sio wauza unga,kama hawakumnyonga shauri yao
Zungumza mambo yenye ushahidi wacha majungu.... Nchi tajiri lkn miaka nenda miaka rudi tuko pale pale kutokana na fitna zenu na majungu
 
hivi huwezi kuandila bila kuhushisha hivi vitu vya kijinga mkuu
Ndiyo umeandika lugha gani hapo sasa? "kuandila" na "Kuhushisha" ndiyo nini. Uandishi wako umejaa mikingamo ya uandishi na mantiki hadi haieleweki ulitaka kuandika nini!
 
Tatizo la Tanzania viongozi wanaona hakuna mwenye eneo kama tanzania hivo hata wakiacha watakuja wengine.
Mshindani wetu kenya tayari ana viwanda vya magari na vimeshaanza uzalishaji sisi ni blablaa tu sababu alianzisha Kikwete.
Tutajenga Bandari ya nchi kavu chato,nduhu tabu ngosha.
 
Mkuu Chige nakushukuru, hata hivyo ukichukulia sababu zote kwa ujumla wake na hiyo proximity ya bagomoyo port to Dar port as a seperate project, it does not make economic sense.
Ukiangalia dar kuna industrial zone nyingi tu ,kule mandela road ,kule pugu road, n.k lakini hazikuwa planned kusupport maendeleo ya viwanda vikubwa kama tunavyoongelea sasahivi, imagine kuna mtu anataka kuwekeza kiwanda cha magari, ameshaomba heka nyingi sana za ardhi, na kiwanda chake kitavuta viwanda vingine 200 kumzunguka, hii haiwezi kuwekwa mikocheni industrial zone kwa kina mengi(ipp), maendeleo makubwa yanahitaji maandalizi ya nafasi kubwa,ndio maana zinaanzishwa industrial zone za kisasa, dar port pia kwa maana ileile is outdated kusupport such goals, ni kama ile reli ya kati ,haifai tena,
 
Rest In Peace Bagamoyo Port!!

Nadhani wapwa zetu Wakenya wakiongozwa na bepari lililokubuhu Uhuru Kenyatta; hivi sasa wanasema "Yes! yes! Tifuaneni tu!"

Kenya walikuwa wanaulilia sana huu mradi uende Lamu!!

Ama kweli, asiyejua maana haambiwi maana!!!

I hope watendaji wa serikali wanasimamia maslahi ya umma lakini sio kwamba ni kutokana na uzumbukuku wao ndio chanzo cha yote hayo!!!

Wanashangaa nini kuona Wachina wanawaleta wa-Oman? Au ina maana hawafahamu maana ya PPP?! Ina maana hawafahamu miradi mikubwa popote pale duniani unakuta imewekezwa na kampuni zaidi ya moja?!

Tangu zamani inafahamika kwamba China ali-target bandari na reli!! Lakini pia kuna suala la industrial zone ambalo walikubaliana ni Oman ndie awekeze!!

Sasa tatizo lipo wapi hapo?! Ningeelewa endapo wangesema Oman hawana uwezo kifedha na hivyo watachelewesha ujenzi wa corridor husika lakini kusema "...baadae wakatuletea Oman, ni hoja ya hovyo!"

Mjomba Uhuru, chukua shavu hilo... Watanzania tumeshatosheka!!!
Kikubwa Maslahi yetu yazingatiwe na kama hautainufaisha zaidi Tanzania uende tu hata Mogadishu wakitaka.
Lazima tuwe na misimamo yetu sio kila cha kupewa au kukopeshwa kwa terms mbaya tubebe tu
 
Kuhusu bandari.watu hamjui.ni vizuri kuuliza wanaojua badala ya kutoa lawama.mchina anataka ajenge.alafu haendeshe yeye.faida achukue asilimia kubwa.kwa miaka 50.yaani magufuli mpaka anaondoka madarakani wanakuja marais wanne mbele yake ndo.tutakabidhiwa bandari yetu.huu ni ukoloni mambo Leo.

halafu kuna malofa huku wanashangilia , yaani wao wanataka asaini tu bila kuweka maslahi ya nchi , kama jk yeye hakuona kuna kasoro bora liende unataka na yaye MAGUFULI aweke nchi rehani
 
Kuna miradi mikubwa (mipya) mitatu ya bandari ambayo ipo kwenye pipeline!

Watu walio na interest kwenye uwekezaji wa bandari walifanya wenyewe feasibility study ili kuamua ni wapi panawafaa!!!

Mwekezaji wa kwanza, ni VIP Engineering!!! Huyu baada ya kuzunguka huku na huko akaona panapomfaa ni Tanga lakini sio kwa ordinary port bali deep sea port! Kwa maana hiyo, si kwamba Tanga hakuna mradi wa bandari bali upo chini ya VIP lakini ni deep sea!

Deep sea port ni kwamba kunakuwa na something like bandari inayoelea... kwahiyo meli hazitafika hadi ufukweni; hapana!

Huko huko Tanga kuna mradi mwingine wa bandari chini ya Mamlaka ya Bandari! Mradi huu ni bandari ya kawaida kama iliyopo Dar es salaam!

Miradi yote hiyo keyword yake ni Mwambani matokeo yake watu huwa wanaichanganya!

Kwahiyo kukujibu swali lako; Tanga kuna mradi wa bandari vile vile!!! Kufanikiwa au kushindwa kwake hakutakuwa na tofauti kama kufanikiwa na kushindwa kwa mradi wa Bagamoyo... fedha!!

Wakati VIP aliona eneo mwafaka kwake ni Tanga, Wachina waliona eneo muafaka kwao ni Bagamoyo!! Na hii ilikuja baada ya Kenya ku-lobby sana wakitaka ule mradi uwe Lamu lakini Wachina wakaamua Bagamoyo!

Lakini kwa hali inavyoendelea, kuna kila dalili Mchina akarudi Lamu!! Uzuri wa Kenya, rais alie madarakani ni bepari na mwingine mwenye uwezo wa kumshinda wa saaa nae ni bepari (Odinga)!!

Kwahiyo hawa hawatafanya kosa hata siku moja!!!

Ikumbukwe kwamba, China bado anahitaji sana bandari ukanda wa Afrika Mashariki!! Hii inatokana na target zake za kujitanua!

Amefanya kama alichotaka kufanya Bagamoyo kule Djbouti! Kajenga bandari kisha akaiunganisha na reli hadi Ethiopia ambayo ni landlocked! Lengo la bandari ya Djibout ni kuhudumia Horn of Africa!

Pia ana miradi sawa na hii West Africa na Mozambique (South)!!

Kwahiyo hata East Africa atajenga tu ili ku-save landlocked countries za nchi za Maziwa Makuu including Zambia! Kwahiyo tukizidisha longo longo; atarudi Lamu ambako bila shaka alikwepa kutokana na distance to hizo nchi kuwa kubwa!!!
Ujue serikali haijakataaa, tulikuwa tukilia kipindi cha nyuma kuwa huu mradi unaweza kuwa bonge la jipu.
Wanachofanya Serikali ni kupigania maslahi ya Tanzania mbele kama walivyofanya kwenye mradi Wa reli kwa kupunguza toka USD Billion 14.9 hadi Bill 7.4 mradi ukiwa chini ya Waturuki.
 
mjingamimi kwani magari ya usafiri yanamilikiwa na Serikali. Unajua kwamba serikali nyingi tu duniani haziendishi bandari zao badala yake zinaendeshwa na watu binafsi na serikali inatoza kodi. Hayo mambo ya mali za umma yalishakufa enzi za ubinafsishaji zama za utawala wa Mwinyi na kukamilishwa na Mkapa!
Sawa.ila tuangalie.hii mikataba iliingiwa vipi?Mimi si mfuasi wa magufuli.ila kwa ili siwezi kumlaumu.mkwere kafanya vitu vya ajabu sana.haiwezekani waendeshe bandari kwa miaka 50.
 
halafu kuna malofa huku wanashangilia , yaani wao wanataka asaini tu bila kuweka maslahi ya nchi , kama jk yeye hakuona kuna kasoro bora liende unataka na yaye MAGUFULI aweke nchi rehani
Lazma tukubali.kikwete alituumiza sana.na mikataba yake 21.
 
hao wachine na waende tu huko Kenya,Tanzania Yetu ni kimbilio la matifa yenye pesa ,kuna waturuki,waarekani,wajerumani,waingereza hao wachina ni akina nani hadi watuumbue na pesa zao za masharti magumu,

na unakuta mtu haoni hili,kama wengi ambavyo hamuoni hivi sasa hadi baadaye abapo mradi ungeshakuwa umekamilika muanze kuleta thread za mara oh serikali imeingia hasara ya matrilion mradi wa bandari bagamoyo,mara kuna ufisadi sijui wapi na wapi huko wakati awali tungekuwa makini tungeweza kuepukana na hizo gharama.

Narudia tena kusema Mchina kuinyonya tanzania sasa basi,ni heri tukae na hilo eneo letu hadi hapo serikali itakpo pata fedha binafsi za kujenga hiyo bandari
 
Ujue serikali haijakataaa, tulikuwa tukilia kipindi cha nyuma kuwa huu mradi unaweza kuwa bonge la jipu.
Wanachofanya Serikali ni kupigania maslahi ya Tanzania mbele kama walivyofanya kwenye mradi Wa reli kwa kupunguza toka USD Billion 14.9 hadi Bill 7.4 mradi ukiwa chini ya Waturuki.
Hao unaosema walikuwa wanakataa kwanza wengi wao walikuwa hawafahamu mradi wenyewe upo vipi na matokeo yake hawakuwa na hoja yoyote ya maana zaidi ya kusema Mkwele alikuwa anapeleka mradi kwao!!

Ni sawa na hapo uliposema kwamba zamani mradi wa reli ulikuwa ni USD 14.9 Billion na sasa 7.4 Billion! Huo nao ni uongo ulionezwa na watu ama kwa kutojua au walichanganya habari ambayo iliripotiwa na Reuters. Hii hapa:

Reuters.png


Kama unavyoona, hiyo habari ni ya March 2015 kabla hata JPM hatujamfikiria kwamba atakuwa rais. Sasa ni reli ipi ambayo Reuters walisema itagharimi USD 14 Billion?! Ni hii hapa chini:
The projects include constructing a 2,561 km (1,536 miles) standard gauge railway connecting the port at the commercial capital of Dar es Salaam to Tanzania's land-locked neighbours, Rwanda and Burundi at a cost of $7.6 billion, Sitta said.

Two additional lines, to cost $6.6 billion, would connect Dar es Salaam to the coal, iron ore and soda ash mining areas in the south and northern parts of the country, he said.
Kwahiyo ukisoma hapo juu, utaona kuna reli mbili... ya kwanza ni ile inayoelekea Rwanda kwa gharama ya USD 7.6 Billion na zingine ni zile ambazo, moja inaelekea Mchuchuma kwenye makaa ya mawe na ya pili inaelekea Manyara ambazo thamani yake zote mbili USD 6.6. Sasa ukichanganya zote tatu ndo unapata hiyo 14 Billion wakati ile ya kwenda Rwanda ni 7.5 Billion tofauti na watu wanavyosema 14 Billion!!'

Na hata ukipitia makarabrasha ya Wizara ya Ujenzi ambayo yalikuwa yanaelezea miaka 50 ya Uhuru, utaona walivyoielezea kwa mapana na marefu hiyo reli ya USD 14 Billion... in short sio railway bali rail network! Railiway ni reli ambayo inakuwa na matawi machache au hakuna kabisa kama hii reli ya Dar - Rwanda wakati rail network inakuwa na matawi kadhaa... ndo hiyo ya USD 14 Billion manake ukisoma ripoti ya Wizara ya Ujenzi kuna tawi lingine linatoka Arusha linakuja kukutana na ile inayotoka Tanga! Kuna lingine linatoka Musoma linakuja kukutana na la Mwanza, na lingine linatoka Bagamoyo pamoja na lile linalotoka Mchuchuma.... matawi yote haya yanakuja kuungana na main railway inayoenda Rwanda!!!
 
Bandari ya Dar wanatumia matishali pia
Nafahamu na ndio maana kuna mahali nimesema ukiona mahali yanatumika matishali ni dalili ya kina haba! Hilo tatizo lipo Dar es salaam vile vile! Na hata kuchimba, bandari ya Dar es salaam imeshawahi kuchimbwa kuongeza kina!!!
 
mjingamimi kwani magari ya usafiri yanamilikiwa na Serikali. Unajua kwamba serikali nyingi tu duniani haziendishi bandari zao badala yake zinaendeshwa na watu binafsi na serikali inatoza kodi. Hayo mambo ya mali za umma yalishakufa enzi za ubinafsishaji zama za utawala wa Mwinyi na kukamilishwa na Mkapa!
Hiki ndicho watu wengi hawajui. Kuna miradi mingi tu ya miundombinu inaendeshwa katika mfumo huo. chige yupo sahihi kwa 100%. Tatizo watu hawako informed vya kutosha na global issues kiasi kwamba tunashindwa kupanua fikra zetu na kufanya maamuzi. Bandari ya Bagamoyo ina umuhimu wa kipekee kwa uchumi wa Tanzania. Italeta multiplier effects kubwa sana kupita hata hizo direct kodi.

Mega port+standard gauge maana yake ni "kuua" bandari zote za nchi jirani kwa maana ya shehena ya meli kubwa. Hiyo ndiyo maana halisi ya "hub" and "gateway". Huwezi kuwa na gateway kwa bandari na miundombinu ya Dar port. Lakini pia ukiwa na bandari kubwa ya namna hiyo unaweza muanzisha minada ya "mazao mbalimbali" karibu na Bandari, uki target bidhaa kutoka Congo, Zambia, Uganda, nk. Kwa kweli naumia sana nikiona mradi huu unapuuzwa.

Halafu watu waelewe jambo moja, Ujenzi wa bandari si uchimbaji wa madini useme siku moja yatakuwa yameisha. Miaka 40 kama alivyosema chige ni sahihi, is peanut kwa maisha ya dunia na maendeleo. Kuna watu hawajui lakini ni wepesi, walikaidi Daraja la Kigamboni hapa, sasa hivi wao wamekuwa ndio wanaosifia mapato yake.
 
Sawa.ila tuangalie.hii mikataba iliingiwa vipi?Mimi si mfuasi wa magufuli.ila kwa ili siwezi kumlaumu.mkwere kafanya vitu vya ajabu sana.haiwezekani waendeshe bandari kwa miaka 50.
Hahahaa, kuna mambo hauko informed na sidhani kama kuna mazingira ya kukufanya uwe informed. Ila nachoweza kukushauri ni hivi:- Kwa mradi kama huu jiulize maswali manne yafuatayo.
1. Baada ya muda gani naweza kupata fedha za kutekeleza mradi huu mwenyewe? (Probably after 50 years)

2. Projection ya Mapato yangu baada ya mradi kijengwa na mwingine, yatashuka au yatapanda? (Probably will quadruple)

3. Je mradi huu utakuwa na associated benefits? Ajira, kuchochea shughuli nyingine za uwekezaji na kiuchumi nk (extensively)

4. Je uhai wa mradi utakuwa ni wa miaka mingapi kabla haujafanyiwa ukarabati mkubwa? (Probably between 100-200 years).

Haya ni baadhi ya very basic questions unaweza kujiuliza, ukiona unapata majibu positive, wala usikae na kiwanja usubiri upate pesa mwenyewe ujenge guest (ambayo kwa kipindi utachopata pesa, hiyo guest haitakuwa na faida tena). Ikitokea Kenya au Mozambique akapata wazo kama hili na akapata financier wa kujenga mradi kama huu, maana yake wewe hautakuja kujenga mradi huu kwa sababu sifa za miradi ya namna hii inatakiwa iwe na nature ya "monopoly". This is purely game theory for those interested in quantitative economic decisions.
 
Wapumbavu.wanataka waiendeshe bandari kwa miaka 50.ndo watuachie.ila mkwere nae katuachiaa majanga kweli.
We jamaa kila mahali unatoka povu kuhusu miaka 50! Umeona wapi hilo suala la miaka 50? By the way, unafahamu nini kuhusu miradi ya BOT? Yaani Build, Operate & Transfer?!

Hayo mambo ni kawaida duniani kote!!! Kabla hatujaenda mbali, soma hapa:
Building of the railway

The Asian Pacific Transport Company, a consortium of private sector companies with experience in transport, construction and related industries, won the tender for the rail project. Specifically, the company is engaged in a BOOT (Build, Own, Operate & Transfer back) scheme to build the 1420 km railway line between Alice Springs and Darwin, and to upgrade, lease and maintain the Tarcoola to Alice Springs section of line. The lease arrangement for the rail line covers 50 years of operation.
Chukua kipande chochote cha sentensi hapo juu kisha Google, utakuta hiyo habari ipo kwenye website ya serikali ya Australia! Ukitaka kusoma kwa kirefu, hapa!

Now look, Australia na utajiri wake wote ambao ukilinaganisha na Tanzania ni sawa na kulinganisha mlima na kichuguu, bado wanaingia ubia na private firms ambazo mradi unaendeshwa na private firms for 50 years! Itakuja kuwa Tanzania ambayo wananchi wake hata maji ya kunywa hawana!!!

Na kwa taarifa yako, hata kama wanaendesha miaka 50, bado faida ipo pale pale! Mapato makubwa kwa mizigo inayopitia bandarini yanatokana na kodi inayotozwa na TRA kwa mizigo inayoingia na kutoka!!

Hao China hata kama wataendesha miaka 50 bado mkusanyaji wa kodi kwa mizigo inayoingia na kutoka atakuwa ni TRA na yote itaenda serikalini na sio kwa Wachina!! Wewe ukiagiza gari ukapitisha pale bandari ya Dar es salaam, wakaochukua pesa karibu sawa na bei uliyonunulia gari yako ni TRA wakati atakachochukua bandari hakitafika hata 10% ya pesa uliyonunulia... na ndivyo itakavyokuwa hata huko Bagamoyo!!!

By the way, bahari pale Bagamoyo ipo tangu kuumbwa kwa dunia! Tangu nchi ipate uhuru, bahari pale ipo! Hadi sasa imeingiza shilingi ngapi?! Mawazo kwamba bora bahari ibaki hivyo hivyo na wala haiozi ni mawazo ambayo yamepitwa na wakati!!
 
Mkuu Mipangomingi hapo juu umeelezea suala la multiplier effect kwenye mradi kama wa bandari ya Bagamoyo! I wish watu kama akina mjingamimi wangefahamu unazungumzia nini hasa!!! Sijui kama wanafahamu, endapo mradi unaenda vizuri, Uchumi wa Bagamoyo ambao kimsingi utakuwa ni wa serikali kuu tutakuwa tunazungumzia sawa na uchumi wa California ambao huwa unalinganishwa kuwa sawa na uchumi wa baadhi ya nchi kubwa kabisa duniani! Kwamba, mradi ukishafika kwenye full operational, tena si ajabu wakati tayari mradi ushakuwa transfered kwetu; utakuta uchumi wa Bagamoyo peke yake unakuwa sawa na uchumi wa nchi kama Rwanda! Na ingawaje utakuwa regarded ni uchumi wa Bagamoyo lakini wala hautakuwa wa Wakwere na Wazaramo bali ni wa Watanzania!!

Watu hawayaoni haya!
 
Back
Top Bottom