Serikali ya China na Tanzania zatofautiana ujenzi wa bandari Bagamoyo

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Messages
17,768
Points
2,000

chakii

JF-Expert Member
Joined Sep 15, 2013
17,768 2,000
Balozi wa Chinanchini, Dk Lu Youqing amesematofauti kati ya Serikali ya Tanzania na ubalozi wa China umesababisha kukwama kwa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Mchakato wa ujenzi wa bandari hiyo ulianza kipindi cha Awamu ya Nne ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete na ulitarajiwa kuhusisha Serikali za Tanzania, China na Oman.

Akizungumza katika mahojiano na baadhi ya waandishi wa habari juzi jijini
Dar es Salaam, Balozi wa China nchini, Dk Lu Youqing alisema, “Mradi wa Bandari ya Bagamoyo na ukanda wa viwanda wilayani humo ni uwekezaji mkubwa kati ya China na Tanzania katika miaka ya karibuni na umeorodheshwa katika Mpangowa Maendeleo wa Miaka Mitano(2016/17-2020/21).

“Kutokana na umuhimu wake unaohusisha Serikali za Tanzania, China na Oman, ushirikiano kati ya maofisa kutoka idara za Serikali ya Tanzania na ubalozi wa China wanazishauri pande zinazohusika kukunjua moyo nakumaliza tofauti ili uweze kuendelea kukiwa na makubaliano kwenye mambo yamsingi,” alisema Lu.

Hata hivyo, kwa sasa jitihada zinafanywa ili ikiwezekana makubaliano hayo katika nusu ya mwaka huu na ujenzi uanze ndani ya mwaka huu.Akizungumzia hilo kwa njia ya simu jana, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani alikiri kutofatiana na Wachina katika ujenzi huo.

“Unajua vitu vingine mnapenda kuvikuza bila sababu.
Sisi tuliiruhusu Serikali ya China kujenga Bandari ya Bagamoyo kwa kitu kinachoitwa PPP na uleujenzi ulikuwa na mambo mengikama maeneo ya viwanda ili kupata uhakika wa mizigo.

Wachina wakatuletea kampuni kwamba sasa ongeeni na kampuni hii, tukawa tunaongea tunaangalia terms au unataka tuwape hivi hivi? Alihoji.
Waziri Ngonyani alisema baadaye Wachina walileta Serikali ya Oman kwenye mradi huo.“Hivyo vingine vyote wanatafutatu sababu ya kutuchelewesha.

Mara ya mwisho tumewaambia lazima yale maeneo tuliyobishania tukubaliane ifikapo Februari 28. Kwa hiyo tunatarajia kupata taarifa ya mwisho ya ujenzi wa bandari hiyo kutoka kwa contractors wa China na Oman,” alisema.

Chanzo : Mwananchi Online
 
Chige

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2008
Messages
9,076
Points
2,000

Chige

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2008
9,076 2,000
Rest In Peace Bagamoyo Port!!

Nadhani wapwa zetu Wakenya wakiongozwa na bepari lililokubuhu Uhuru Kenyatta; hivi sasa wanasema "Yes! yes! Tifuaneni tu!"

Kenya walikuwa wanaulilia sana huu mradi uende Lamu!!

Ama kweli, asiyejua maana haambiwi maana!!!

I hope watendaji wa serikali wanasimamia maslahi ya umma lakini sio kwamba ni kutokana na uzumbukuku wao ndio chanzo cha yote hayo!!!

Wanashangaa nini kuona Wachina wanawaleta wa-Oman? Au ina maana hawafahamu maana ya PPP?! Ina maana hawafahamu miradi mikubwa popote pale duniani unakuta imewekezwa na kampuni zaidi ya moja?!

Tangu zamani inafahamika kwamba China ali-target bandari na reli!! Lakini pia kuna suala la industrial zone ambalo walikubaliana ni Oman ndie awekeze!!

Sasa tatizo lipo wapi hapo?! Ningeelewa endapo wangesema Oman hawana uwezo kifedha na hivyo watachelewesha ujenzi wa corridor husika lakini kusema "...baadae wakatuletea Oman, ni hoja ya hovyo!"

Mjomba Uhuru, chukua shavu hilo... Watanzania tumeshatosheka!!!
 
Chige

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2008
Messages
9,076
Points
2,000

Chige

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2008
9,076 2,000
Huo mradi Tanzania itanufaika kweli maana naona hela wanatoa china na oman, huu mradi naona bora upigwa chini
Huo mradi una manufaa sana sema watu tunauangalia kwa macho ya makengeza!!!

Kwa mfano kuna watu wanahoji suala la China kutaka kuendesha mradi kwa 40 years kabla hawajatuachia bandari yetu!!!

Hapa tunasahau bandari ya Dar es salaam ipo tangu mkoloni na bado inapiga mzigo kama kawaida!! Kwahiyo wala si kwamba baada ya 40 years haitakuwa tena bandari!!!

Lakini kubwa zaidi, hata kama wataendesha bandari kwa muda wote huo; bado kodi zetu zitakuwa pale pale!! Hata ukienda Bandari ya Dar es salaam, anayeongoza kuchukua mapato ya kufuru sio mamlaka ya bandari bali TRA ambao nao pia watakuwa bandari ya Bagamoyo kama kawaida kwa sababu, China kuendesha bandari haimaanishi hata kodi watachukua wao; no!

Na kwa kuangalia import and export targets za China, kuna uwezekano mkubwa sana bandari itakuwa busy sana kwa mizigo inayoingia na kutoka na hivyo kuzidisha mapato ya kodi maradufu!!!
 
Allen Kilewella

Verified Member
Joined
Sep 30, 2011
Messages
12,125
Points
2,000

Allen Kilewella

Verified Member
Joined Sep 30, 2011
12,125 2,000
chige unatwanga maji kwenye kinu ndugu yangu. Hata hivyo nakupongeza kwa uliyoyaeleza kwani huo ndiyo Uzalendo. Tatizo letu ni makengeza ya akili tuliyonayo kwamba utajiri ni laana. Kuna watu watasema "waende zao hatuna shida na bandari Bagamoyo" lakini wanasahau kwamba uwekezaji huo hautachukua hata senti ya mtanzania tofauti ya kile kiwanja cha ndege na duka la madawa vilivyojengwa kule nyumbani!!
 
lelooo

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2011
Messages
420
Points
500

lelooo

JF-Expert Member
Joined Jun 16, 2011
420 500
Rest In Peace Bagamoyo Port!!

Nadhani wapwa zetu Wakenya wakiongozwa na bepari lililokubuhu Uhuru Kenyatta; hivi sasa wanasema "Yes! yes! Tifuaneni tu!"

Kenya walikuwa wanaulilia sana huu mradi uende Lamu!!

Ama kweli, asiyejua maana haambiwi maana!!!

I hope watendaji wa serikali wanasimamia maslahi ya umma lakini sio kwamba ni kutokana na uzumbukuku wao ndio chanzo cha yote hayo!!!

Wanashangaa nini kuona Wachina wanawaleta wa-Oman? Au ina maana hawafahamu maana ya PPP?! Ina maana hawafahamu miradi mikubwa popote pale duniani unakuta imewekezwa na kampuni zaidi ya moja?!

Tangu zamani inafahamika kwamba China ali-target bandari na reli!! Lakini pia kuna suala la industrial zone ambalo walikubaliana ni Oman ndie awekeze!!

Sasa tatizo lipo wapi hapo?! Ningeelewa endapo wangesema Oman hawana uwezo kifedha na hivyo watachelewesha ujenzi wa corridor husika lakini kusema "...baadae wakatuletea Oman, ni hoja ya hovyo!"

Mjomba Uhuru, chukua shavu hilo... Watanzania tumeshatosheka!!!
lakin badala ya bagamoyo kwanini wasiende tanga?kumbuka tanga kukiwa na uhakika wa bandari mikoa ya tanga,kilimanjaro ,arusha na mara itakuwa na uhakika wa kutumia bandari za tanzania badala ya saiv wanatumia mombasa!alaf pia tutakuwa na uhakika wa kugawana na wakenya mizigo ya uganda! jaribu tu kutafakari.
pili bandari ya dar bado ina eneo kubwa la kutosheleza upanuzi zaidi hata ya uwezo wa saiv kwa mara tatu.na ndo mana world bank wametoa mkopo kwa ajili ya upanuzi.
 
Ndahani

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2008
Messages
16,188
Points
2,000

Ndahani

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2008
16,188 2,000

Mashairi ya mradi yakoje? Hata IPTL walisema mradi wa manufaa
 
Chige

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2008
Messages
9,076
Points
2,000

Chige

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2008
9,076 2,000
lakin badala ya bagamoyo kwanini wasiende tanga?kumbuka tanga kukiwa na uhakika wa bandari mikoa ya tanga,kilimanjaro ,arusha na mara itakuwa na uhakika wa kutumia bandari za tanzania badala ya saiv wanatumia mombasa!alaf pia tutakuwa na uhakika wa kugawana na wakenya mizigo ya uganda! jaribu tu kutafakari.
pili bandari ya dar bado ina eneo kubwa la kutosheleza upanuzi zaidi hata ya uwezo wa saiv kwa mara tatu.na ndo mana world bank wametoa mkopo kwa ajili ya upanuzi.
Kuna miradi mikubwa (mipya) mitatu ya bandari ambayo ipo kwenye pipeline!

Watu walio na interest kwenye uwekezaji wa bandari walifanya wenyewe feasibility study ili kuamua ni wapi panawafaa!!!

Mwekezaji wa kwanza, ni VIP Engineering!!! Huyu baada ya kuzunguka huku na huko akaona panapomfaa ni Tanga lakini sio kwa ordinary port bali deep sea port! Kwa maana hiyo, si kwamba Tanga hakuna mradi wa bandari bali upo chini ya VIP lakini ni deep sea!

Deep sea port ni kwamba kunakuwa na something like bandari inayoelea... kwahiyo meli hazitafika hadi ufukweni; hapana!

Huko huko Tanga kuna mradi mwingine wa bandari chini ya Mamlaka ya Bandari! Mradi huu ni bandari ya kawaida kama iliyopo Dar es salaam!

Miradi yote hiyo keyword yake ni Mwambani matokeo yake watu huwa wanaichanganya!

Kwahiyo kukujibu swali lako; Tanga kuna mradi wa bandari vile vile!!! Kufanikiwa au kushindwa kwake hakutakuwa na tofauti kama kufanikiwa na kushindwa kwa mradi wa Bagamoyo... fedha!!

Wakati VIP aliona eneo mwafaka kwake ni Tanga, Wachina waliona eneo muafaka kwao ni Bagamoyo!! Na hii ilikuja baada ya Kenya ku-lobby sana wakitaka ule mradi uwe Lamu lakini Wachina wakaamua Bagamoyo!

Lakini kwa hali inavyoendelea, kuna kila dalili Mchina akarudi Lamu!! Uzuri wa Kenya, rais alie madarakani ni bepari na mwingine mwenye uwezo wa kumshinda wa saaa nae ni bepari (Odinga)!!

Kwahiyo hawa hawatafanya kosa hata siku moja!!!

Ikumbukwe kwamba, China bado anahitaji sana bandari ukanda wa Afrika Mashariki!! Hii inatokana na target zake za kujitanua!

Amefanya kama alichotaka kufanya Bagamoyo kule Djbouti! Kajenga bandari kisha akaiunganisha na reli hadi Ethiopia ambayo ni landlocked! Lengo la bandari ya Djibout ni kuhudumia Horn of Africa!

Pia ana miradi sawa na hii West Africa na Mozambique (South)!!

Kwahiyo hata East Africa atajenga tu ili ku-save landlocked countries za nchi za Maziwa Makuu including Zambia! Kwahiyo tukizidisha longo longo; atarudi Lamu ambako bila shaka alikwepa kutokana na distance to hizo nchi kuwa kubwa!!!
 
Chige

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2008
Messages
9,076
Points
2,000

Chige

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2008
9,076 2,000
chige unatwanga maji kwenye kinu ndugu yangu. Hata hivyo nakupongeza kwa uliyoyaeleza kwani huo ndiyo Uzalendo. Tatizo letu ni makengeza ya akili tuliyonayo kwamba utajiri ni laana. Kuna watu watasema "waende zao hatuna shida na bandari Bagamoyo" lakini wanasahau kwamba uwekezaji huo hautachukua hata senti ya mtanzania tofauti ya kile kiwanja cha ndege na duka madawa vilivyojengwa la kule nyumbani!!
Upo sahihi kwa 100%!!!!
 
Chige

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2008
Messages
9,076
Points
2,000

Chige

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2008
9,076 2,000
Mashairi ya mradi yakoje? Hata IPTL walisema mradi wa manufaa
Kupanga ni kuchagua... kwamba tuachieni bahari yetu hata kama hatuna uwezo wa kujenga na kuacha opportunities ziende kwingine au kusema kwanini niache pori limejaa simba wakati kuna watu wenye uwezo wa kulima nami nitapata percent kupitia miradi husika!!

Kwa maskini jeuri, anaweza kusema "acha pori liwe makazi ya simba!"

Masharti yapoje both you and I know kwamba si rahisi kufahamu inside out ya mikataba ya serikali!! Hata hivyo ambacho watu wamekuwa wakikisema sana ni huo mkataba wa China kutaka kuendesha bandari kwa 40 years. Suala la 40 years sioni tatizo kwa sababu mikataba ya Build Operate & Transfer (BOT) ndivyo ilivyo!! Mtu anajenga, anaendesha kisha anakurudishia mradi wako!! Hii tunafanya hata kwenye maaisha ya kawaida! Mtu anakuja kwenye kiwanja chako, anajenga mjengo ambao anaufanyia kazi kwa miaka kadhaa kisha anakurudishia nyumba yako!!!
 
moudgulf

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2017
Messages
71,022
Points
2,000

moudgulf

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2017
71,022 2,000
wachina waliingia mkenge wakasaini mikataba 17 na jk kwa sababu wanazojua wao ila magu kawastukia atapiga chini mikataba yote kwa maslahi ya nch na sio wauza unga,kama hawakumnyonga shauri yao
Iweke wazi hiyo mikataba na mashart yake nasi tuone tulivyotaka kupigwa. na hiyo itatasaidia kuondokana na porojo za mtaani
 
Forum statistics

Threads 1,381,733
Members 526,184
Posts 33,810,294
Top