Serikali ya CCM yazidi kumwandama Mbowe!

Serikali ya CCM yazidi kumwandama Mbowe!

Greenwhich

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
1,337
Reaction score
968
Katika kile kinachoonekana kumweka bussy Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe tayari kesi iliyofunguliwa miaka minne huko nyuma imefufuliwa.

Kesi hiyo iliyoratibiwa na CCM alifunguliwa Mbowe kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita kwa madai kwamba alimshambulia msimamizi wa Uchaguzi huko HAI.

Hapo jana kesi hiyo iliibuka na Hakimu akasoma kile kilichosemwa ni hukumu ya awali kwa kusema kwamba Mbowe ana kesi ya Kujibu na anapaswa kujitetea.

Ikumbukwe kwa sasa Mbowe mbali ya kuwa Mwenyekiti wa Chadema ndiye Mwenyekiti pia wa Ukawa na ndiye kinara wa mapambano ya Katiba ya wananchi.

=================================

Hai. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameingia matatani baada ya Mahakama ya Wilaya ya Hai kuona ana kesi ya kujibu katika mashtaka ya kumshambulia mwangalizi wa ndani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Uamuzi huo ulitolewa jana na hakimu mfawidhi wa wilaya hiyo, Denis Mpelembwa mbele ya Mbowe, wakili wake, Issa Rajabu na mwendesha mashtaka, Inspekta Marwa Mwita.

Mpelembwa alisema mashahidi saba wa upande wa mashtaka wameishawishi mahakama kuwa siku hiyo kuna tafrani ambayo ilitokea na ambayo Mbowe

atatakiwa kutoa ufafanuzi wa kuhusika kwake.

Alisema ingawa upande wa utetezi ukiongozwa na wakili Albert Msando na baadaye Rajabu, ulitoa hoja kuwa ushahidi wa Jamhuri uliacha mashimo mengi, yeye anaona Mbowe ana kesi ya kujibu.

"Katika hoja zao (utetezi) wanaona ukiacha ushahidi wa Nassir Yamin, hakuna shahidi mwingine aliyethibitisha kushuhudia Nassir akipigwa," alisema akinukuu hoja za mawakili wa utetezi.

Hakimu aliongeza kusema: "Utetezi pia walitoa hoja kuwa upande wa mashtaka ulishindwa kuwaita akina mama ambao wanaodaiwa kushuhudia, hivyo kuacha mashimo mengi katika ushahidi wao."

Hata hivyo, hakimu alisema katika hoja zao ambazo ziliishawishi mahakama, upande wa mashitaka ulijibu kuwa sheria haiwabani kuleta kila shahidi kujenga msingi wa kesi yao.

"Ni rai yao (mashtaka) kuwa mashahidi wao saba wameweza kuthibitisha shtaka dhidi ya mshtakiwa pasipo kuacha mashaka ama mianya kama utetezi walivyodai," alisema Mpelembwa.

Hakimu Mpelembwa alisema baada ya kupitia hoja za mawakili wa pande zote mbili, anaona upande wa Jamhuri umeweza kuishawishi mahakama kuwa mshtakiwa ana kesi ya kujibu.

Kutokana na uamuzi huo, Hakimu alisema mahakama inampa nafasi Mbowe kujitetea na kesi hiyo imepangwa kutajwa Julai 17, siku upande wa utetezi utakapotoa orodha ya mashahidi wao.

Katika uchaguzi huo mkuu wa 2010, Mbowe aliibuka mshindi kwa kupata kura 28,585 akifuatiwa na Fuya Kimbita (CCM), kura 23,349, Hawa Kihogo (UDP) 258 na Petro Kisimbo (TLP) 135.


Chanzo: Mwananchi
 
Mbowe asijali kwani anazo kesi kibao.Hii moja haitamfanya kushindwa kutekeleza majukumu ya ukawa
pamoja na kumuongezea umaarufu kwa sababu atashinda kesi hiyo pia ndivyo ccm wanavyozidi kujivua ngozi na wanachi wa kada ya chini wanazidi kuufahamu mzimu wao unaowala taratibu ingawa miaka ya hivi karibuni wamepongeza kasi
 
pamoja na kumuongezea umaarufu kwa sababu atashinda kesi hiyo pia ndivyo ccm wanavyozidi kujivua ngozi na wanachi wa kada ya chini wanazidi kuufahamu mzimu wao unaowala taratibu ingawa miaka ya hivi karibuni wamepongeza kasi
Bawacha wote mnapotoshana kila kukicha nani kakwambia kuwa mbowe ni marufu kwenye nchi hii,kwa tarifa yako umarufu wa mbowe pengine upo kwenye uharifu na uendeshaji wa disco za usiku.
 
Bawacha wote mnapotoshana kila kukicha nani kakwambia kuwa mbowe ni marufu kwenye nchi hii,kwa tarifa yako umarufu wa mbowe pengine upo kwenye uharifu na uendeshaji wa disco za usiku.
sibishani na haja kubwa mimi! na wala sijashikiwa akili kama wewe unapanukwa tu
 
Mbowe alimpiga vibao wakala wake kwa kuhisi kuwa anapanga kumsaliti.
 
Kwa hiyo kama kweli alimshambulia mlitaka asishitakiwe? Tena aliyemshambulia ni mwanamke!
 
Hata baada ya uchaguzi wa 2015 kesi nyingi sana zitaanza kusikilizwa.
 
katika kile kinachoonekana kumweka bussy mwenyekiti wa chadema freeman mbowe tayari kesi iliyofunguliwa miaka minne huko nyuma imefufuliwa.

Kesi hiyo iliyoratibiwa na ccm alifunguliwa mbowe kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita kwa madai kwamba alimshambulia msimamizi wa uchaguzi huko hai.

Hapo jana kesi hiyo iliibuka na hakimu akasoma kile kilichosemwa ni hukumu ya awali kwa kusema kwamba mbowe ana kesi ya kujibu na anapaswa kujitetea.

Ikumbukwe kwa sasa mbowe mbali ya kuwa mwenyekiti wa chadema ndiye mwenyekiti pia wa ukawa na ndiye kinara wa mapambano ya katiba ya wananchi.
sheria ni msumeno
 
Back
Top Bottom