Serikali ya CCM yazidi kumwandama Mbowe!

Serikali ya CCM yazidi kumwandama Mbowe!

Bawacha wote mnapotoshana kila kukicha nani kakwambia kuwa mbowe ni marufu kwenye nchi hii,kwa tarifa yako umarufu wa mbowe pengine upo kwenye uharifu na uendeshaji wa disco za usiku.

Basi maarufi wewe ambaye pamoja na kuwa hufahamiki humu jf kwa kutumia id feki lakini bado unamjadili mbowe ambaye kwa sasa hayupo hapa sasa sijui nani maarufu hapo.
 
Bungeni wana kinga kama hujui

Najua we ni kibaraka mzuri wa Lumumba ila Kumbuka Werema alitishia kukata kichwa nje ya bunge,na kina Rage je??!!

OCD mkoani Shinyanga alipigwa mtama na kuanguka chini na mgombea ubunge wa CCM bwana Moses Kisena ambae ni mshirika wa UDA,hakuchukuliwa hatua,unasemaje na hapo??!!!
 
Hai. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameingia matatani baada ya Mahakama ya Wilaya ya Hai kuona ana kesi ya kujibu katika mashtaka ya kumshambulia mwangalizi wa ndani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Uamuzi huo ulitolewa jana na hakimu mfawidhi wa wilaya hiyo, Denis Mpelembwa mbele ya Mbowe, wakili wake, Issa Rajabu na mwendesha mashtaka, Inspekta Marwa Mwita.

Mpelembwa alisema mashahidi saba wa upande wa mashtaka wameishawishi mahakama kuwa siku hiyo kuna tafrani ambayo ilitokea na ambayo Mbowe

atatakiwa kutoa ufafanuzi wa kuhusika kwake.

Alisema ingawa upande wa utetezi ukiongozwa na wakili Albert Msando na baadaye Rajabu, ulitoa hoja kuwa ushahidi wa Jamhuri uliacha mashimo mengi, yeye anaona Mbowe ana kesi ya kujibu.

"Katika hoja zao (utetezi) wanaona ukiacha ushahidi wa Nassir Yamin, hakuna shahidi mwingine aliyethibitisha kushuhudia Nassir akipigwa," alisema akinukuu hoja za mawakili wa utetezi.

Hakimu aliongeza kusema: "Utetezi pia walitoa hoja kuwa upande wa mashtaka ulishindwa kuwaita akina mama ambao wanaodaiwa kushuhudia, hivyo kuacha mashimo mengi katika ushahidi wao."

Hata hivyo, hakimu alisema katika hoja zao ambazo ziliishawishi mahakama, upande wa mashitaka ulijibu kuwa sheria haiwabani kuleta kila shahidi kujenga msingi wa kesi yao.

"Ni rai yao (mashtaka) kuwa mashahidi wao saba wameweza kuthibitisha shtaka dhidi ya mshtakiwa pasipo kuacha mashaka ama mianya kama utetezi walivyodai," alisema Mpelembwa.

Hakimu Mpelembwa alisema baada ya kupitia hoja za mawakili wa pande zote mbili, anaona upande wa Jamhuri umeweza kuishawishi mahakama kuwa mshtakiwa ana kesi ya kujibu.

Kutokana na uamuzi huo, Hakimu alisema mahakama inampa nafasi Mbowe kujitetea na kesi hiyo imepangwa kutajwa Julai 17, siku upande wa utetezi utakapotoa orodha ya mashahidi wao.

Katika uchaguzi huo mkuu wa 2010, Mbowe aliibuka mshindi kwa kupata kura 28,585 akifuatiwa na Fuya Kimbita (CCM), kura 23,349, Hawa Kihogo (UDP) 258 na Petro Kisimbo (TLP) 135.

Chanzo: Mwanachi

 
Tumeshazoea hayo mashitaka ya ccm dhidi ya viongozi wa upinzani!Mh.Mbowe ilipaswa amvunje kiuno kabisa huyo mwangalizi.NO LONGER AT EASE
 
Waraka wa katibu mkuu wa ccm wa enzi hizo baba yake myoa upara ulitoa maagizo kuwa zifunguliwe kesi nchi nzima kwenye majimbo ya uchaguzi yote yaliyoyakuliwa na vyama vya upinzani hasa chadema na hilo lilifanyika kwa nchi nzima ila chadema walipangua kesi nyingi na bado wakalinda ushindi wao

Sasa kesi ya mh mbowe ya 2010 ije kukufufuliwa leo? Kwa vile mmekosa namna ya kumdhofisha?

Bahati nzuri sio mkaidi kwa mahakama,akiitwa anataenda na kwa vile mahakama imeona anakesi ya msingi ya kujibu basi sawa yote kheri ila kama kuna lolote nyuma ya pazia mjue kabisa tutalibaini very soon
 
Hamjambambikizia ya ugaidi mnasubiri nini na ndiyo siasa pendwa za ccm

Mwigulu yupo anaandaa ushahidi ili safari hii akibambika kesi ushahidi awe nao hahahahaaaa!!!!
 
Kumbe Albert Msando Wakili wa Zitto ndio wakili wa Mbowe pia?!
 
Laana ya marehemu chacha wangwe imemkalia kooni Mbowe
 
Bawacha wote mnapotoshana kila kukicha nani kakwambia kuwa mbowe ni marufu kwenye nchi hii,kwa tarifa yako umarufu wa mbowe pengine upo kwenye uharifu na uendeshaji wa disco za usiku.

Wakati mwingine ona aibu kwa kile unachoandika.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Chadomo mna utitiri wa watu wasiojitambua....hizo haki mnazovunga kuzipigania kila kukicha ni kwa ajili ya makundi fulani ya watu tu, ama ? wakiguswa mnaowaabudu basi haki ipindishwe ndio mseme hewala ?

Aliyepigwa apatiwe haki yake, hata kama Chadomo wote mtampinga, wapo wenye mapenzi mema watamshika mkono hadi kieleweke.

Kwa dalili hizi mkipata madaraka nadhani hamtoishia tu kutwanga wenzenu na matofali, mtaanza kutumia miguu ya kuku kabisa.
 
Bawacha wote mnapotoshana kila kukicha nani kakwambia kuwa mbowe ni marufu kwenye nchi hii,kwa tarifa yako umarufu wa mbowe pengine upo kwenye uharifu na uendeshaji wa disco za usiku.
ni kweli boss wewe tu ndio maarufu nchi hii
 
Inatakiwa wamkamate na kumsafirisha kwa chopa kama walivyofanya wakati ule wa ile kesi ya Arusha
 
Katika kile kinachoonekana kumweka bussy Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe tayari kesi iliyofunguliwa miaka minne huko nyuma imefufuliwa.

Kesi hiyo iliyoratibiwa na CCM alifunguliwa Mbowe kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita kwa madai kwamba alimshambulia msimamizi wa Uchaguzi huko HAI.

Hapo jana kesi hiyo iliibuka na Hakimu akasoma kile kilichosemwa ni hukumu ya awali kwa kusema kwamba Mbowe ana kesi ya Kujibu na anapaswa kujitetea.

Ikumbukwe kwa sasa Mbowe mbali ya kuwa Mwenyekiti wa Chadema ndiye Mwenyekiti pia wa Ukawa na ndiye kinara wa mapambano ya Katiba ya wananchi.

=================================



Chanzo: Mwananchi

kesi ipo siku nyingi pinda alkuwa anaipoza tu aliepigwa sasa kachachama anaona hatendewi haki ccm wanataka kumbeba mbowe
 
sheria ni msumeno
sheria gani kipofu ya kukandamiza upinzani ccm wanahangaika bure wameshakaribia kufa ukawa ndo sumu ya kuuwa ccm pamoja na vibaraka wake wote kamanda mbowe kila la heri ushindi uko karibu
 
Back
Top Bottom