Serikali ya CCM yazidi kumwandama Mbowe!

Hai. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameingia matatani baada ya Mahakama ya Wilaya ya Hai kuona ana kesi ya kujibu katika mashtaka ya kumshambulia mwangalizi wa ndani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Uamuzi huo ulitolewa jana na hakimu mfawidhi wa wilaya hiyo, Denis Mpelembwa mbele ya Mbowe, wakili wake, Issa Rajabu na mwendesha mashtaka, Inspekta Marwa Mwita.

Mpelembwa alisema mashahidi saba wa upande wa mashtaka wameishawishi mahakama kuwa siku hiyo kuna tafrani ambayo ilitokea na ambayo Mbowe

atatakiwa kutoa ufafanuzi wa kuhusika kwake.

Alisema ingawa upande wa utetezi ukiongozwa na wakili Albert Msando na baadaye Rajabu, ulitoa hoja kuwa ushahidi wa Jamhuri uliacha mashimo mengi, yeye anaona Mbowe ana kesi ya kujibu.

“Katika hoja zao (utetezi) wanaona ukiacha ushahidi wa Nassir Yamin, hakuna shahidi mwingine aliyethibitisha kushuhudia Nassir akipigwa,” alisema akinukuu hoja za mawakili wa utetezi.

Hakimu aliongeza kusema: “Utetezi pia walitoa hoja kuwa upande wa mashtaka ulishindwa kuwaita akina mama ambao wanaodaiwa kushuhudia, hivyo kuacha mashimo mengi katika ushahidi wao.”

Hata hivyo, hakimu alisema katika hoja zao ambazo ziliishawishi mahakama, upande wa mashitaka ulijibu kuwa sheria haiwabani kuleta kila shahidi kujenga msingi wa kesi yao.

“Ni rai yao (mashtaka) kuwa mashahidi wao saba wameweza kuthibitisha shtaka dhidi ya mshtakiwa pasipo kuacha mashaka ama mianya kama utetezi walivyodai,” alisema Mpelembwa.

Hakimu Mpelembwa alisema baada ya kupitia hoja za mawakili wa pande zote mbili, anaona upande wa Jamhuri umeweza kuishawishi mahakama kuwa mshtakiwa ana kesi ya kujibu.

Kutokana na uamuzi huo, Hakimu alisema mahakama inampa nafasi Mbowe kujitetea na kesi hiyo imepangwa kutajwa Julai 17, siku upande wa utetezi utakapotoa orodha ya mashahidi wao.

Katika uchaguzi huo mkuu wa 2010, Mbowe aliibuka mshindi kwa kupata kura 28,585 akifuatiwa na Fuya Kimbita (CCM), kura 23,349, Hawa Kihogo (UDP) 258 na Petro Kisimbo (TLP) 135.

Chanzo: Mwananchi

*****************
Hapa ndio Gongo haijahahalishwa rasmi sijui ikihalalishwa itakuwaje?

Wenu
Tume ya Katiba
 
Hajafungwa bado?Vunjaji sheria
 
Kumbe Mbowe ndio mwenyekiti wa Ukawa!!
Kwa hiyo mwenyekiti wa Ukawa anaruhusiwa kuvunja sheria?

Katika kile
kinachoonekana kumweka bussy Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe tayari
kesi iliyofunguliwa miaka minne huko nyuma imefufuliwa.

Kesi hiyo iliyoratibiwa na CCM alifunguliwa Mbowe kipindi cha uchaguzi
mkuu uliopita kwa madai kwamba alimshambulia msimamizi wa Uchaguzi huko
HAI.

Hapo jana kesi hiyo iliibuka na Hakimu akasoma kile kilichosemwa ni
hukumu ya awali kwa kusema kwamba Mbowe ana kesi ya Kujibu na anapaswa
kujitetea.

Ikumbukwe kwa sasa Mbowe mbali ya kuwa Mwenyekiti wa Chadema ndiye
Mwenyekiti pia wa Ukawa na ndiye kinara wa mapambano ya Katiba ya
wananchi.
 
Mbowe ni mharifu kama wahalifu wengine tu hivyo lazima sheria ichukue nafasi yake kwa watu wahalifu kama yeye.
Tuwekee ushahidi. Uhalifu wake unafanana na wa Razalo Nyalandu, Change, Riziwani, Lowasa, Werema na Magamba wote.
 
Mbowe ni mharifu kama wahalifu wengine tu hivyo lazima sheria ichukue nafasi yake kwa watu wahalifu kama yeye.

Wakati mwingine turuhusu ubongo ufanye kazi yake na tusilazimishe uendawazimu. Aliyekuambia Mbowe ni mhalifu ni nani?Hamuoni uhalifu unaofanywa mchana kweupe na Magamba mnabaki na Mbowe. CCM wanaendeshwa ulaghali na utesaji. Mnadhani mbowe ndo target ya kuiuwa chadema lakini mjue he is a Grain of wheat inayoendelea kuzaa mamilioni ya matumaini kwa wanaoteswa since uhuru. mtabakia na uzamani wenu wa kutumia akili butu huku wenye sharpen mind walishagundua njama zenu ovu na wameshaweka protection.
 
Kama nyie sio vibaraka na watumwa wa mabwana zenu,yule mwanasheria Mkuu kachukuliwa hatua gani kwa kumtishia kumkata kichwa Kafulila na kumkata mangumi ndani ya bunge??!!

Rage na wenzie pale Dodoma walichukuliwa hatua gani kwa kumpiga kwa miti na mawe kada wa CHADEMA??!!
Mnalipwa bure tu hapo Lumumba,bora wote mngekuwa na jinsia kama ya Juliana Shonza tungewavumilia uhalali wa malipo yenu!!!
 
kama ndivyo wezi wa fedha za IPTL-Escrow wangeshitakiwa

NA kama hao IPTL wangekuwa na Hake aliyesababisha ufedhuli huuu angewajibika. Mnahangaika na Mbowe mnaaach mambo mazito ya taifa hili yanayoangamiza mabilioni ya fedha huku nchi ikibaki masikini. Mbona CCM mnajidhalilisha? Kuweni na modern mind. Kupiga au kupigwa ni wangapi walipigwa na kuuliwa na CCM lakini mambo yalimezwa? Mpaka wanaccm wanafikia hatua ya kumpiga mkuu wa polisi kule SHinyanga kwa jambo la haki mmesahau?
 
miaka yote4 walikiwa wapi?

Sheria wameijua leo? UKAWA hawatorudi bungeni kwa style hii ng'o

Hata mimi nimestaajabu kidogo!

Nijuavyo mimi, kesi au shitaka likisha funguliwa, likasikilizwa, likisimama lazima kuwepo sababu za kusimama kwake na kama mlalamikaji akishindwa kuhudhulia kwa kipindi Fulani au mara kadhaa kesi inafutwa! Na hapa mlalamikaji anaweza kudai au kufungua shitaka jipya dhidi ya mlalamikaji wa kwanza kwa kumpotezea muda, fedha na kuchafuliwa etc... Sasa kwa kesi hii, kwa nni ifufuliwe tena na kwa muda huo wote. Watalaamu tiririkeni tafadhali.
 
Kama nyie sio vibaraka na watumwa wa mabwana zenu,yule mwanasheria Mkuu kachukuliwa hatua gani kwa kumtishia kumkata kichwa Kafulila na kumkata mangumi ndani ya bunge??!!

Rage na wenzie pale Dodoma walichukuliwa hatua gani kwa kumpiga kwa miti na mawe kada wa CHADEMA??!!
Mnalipwa bure tu hapo Lumumba,bora wote mngekuwa na jinsia kama ya Juliana Shonza tungewavumilia uhalali wa malipo yenu!!!

Bungeni wana kinga kama hujui
 
Back
Top Bottom